Hii imekaaje?! Tume ya uchaguzi ya Kenya imekataa kuwaruhusu wataalm wa Odinga (NASA) kukagua computer yao kwa madai kuwa server yao iko Ulaya! Hii ni kinyume na amri ya Mahakama ya Rufaa iliyowataka Tume kuwaruhusu NASA kukagua computer hizo!
My take: Tume inataka kuficha nini?
Walichotakiwa kukifanya NASA ni kukagua mfumo wa kupokelea na kutangazia matokeo na kujiridhisha kama haukuingiliwa!
Mapema wakati wa kumalizia kuwasilisha madai yao, nimemuona na kumsikiliza wakili wa NASA akikiri kuruhusiwa kufanya ukaguzi huo ingawa amedai kutokana mfumo huo kuwa strong na masuala ya kuzuia kudukuliwa, iliwachukua muda kuweza kuingia kwenye mfumo na kukagua,na matokeo hawakuona dalili za kudukuliwa matokeo!
Suala la kutaka kukagua server sio jambo waliloelekezwa na mahakama kulifanya!
Ikumbukwe kwamba systems kubwa kama hizi za uchaguzi kwa kiasi kikubwa huwa zinaandaliwa, kusimamiwa kwa ukaribu sana na watengenezaji wa system husika! Suala la server ya Tume ya uchaguzi Kenya kuwa ulaya ni jambo la kawaida! Inategemea na walivyoamua wao!
Ukweli tume ya uchaguzi Kenya imetoa ushirikiano mkubwa sana kwa wadai ambao ni NASA, hili hawawezi kulipinga. Na kuna uwezekano mkubwa sana Raila akashindwa kesi hii kwani madai yao mengi yanajikita katika kasoro ndogo ndogo sana ambazo kiuhalisia haziwezi kusababisha uchaguzi kurudiwa!
Raila alimalizwa na waangalizi wa Kimataifa ambao comments zao wote zilisifia mwenendo wa uchaguzi na matokeo yake!
Changamoto ipo kwa tume yetu ya uchaguzi Tanzania, ukweli ni kwamba kwa kulinganisha na Kenya, tume yetu inabaki kuwa Tume ya uchaguzi mbovu kabisa kwa jinsi inavyojiendesha!
Yetu ni tume ambayo kwa kiasi kikubwa ilikalili matokeo kutoka katika midomo ya akina January na Nauye!
Ni aibu!