Uchaguzi 2020 Tume ya uchaguzi na CCM wainajisi katiba, Deo Mwanyika hastahili kuteuliwa wala kugombea ubunge kwa sababu ya kesi ya kukwepa kodi

Uchaguzi 2020 Tume ya uchaguzi na CCM wainajisi katiba, Deo Mwanyika hastahili kuteuliwa wala kugombea ubunge kwa sababu ya kesi ya kukwepa kodi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Tuweke rekodi sawa, Deo Mwanyika alihukumiwa kwa kukwepa kodi.

Michango ya NSSF ya Deogratius Mwanyika, aliyekuwa Rais wa migodi ya Pangea, North Mara Exploration na Bulyanhulu, imelazimika kulipa sehemu ya fidia ya makubaliano maalum kwa Serikali baada ya kukiri kufanya makosa.

IMG_20200831_130923.jpg

Fedha kiasi cha TSh bilioni 1, kilichotwa na kuingizwa kwenye akaunti ya maalum ya fedha za serikali inayosimamiwa na Hazina iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mnamo Mei 11, 2020.

Makubaliano ya faini yaleta utata hadi Ikulu kuhusishwa
Juni 17, 2020 Mwanyika aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, pamoja na wenzake wawili, baada ya Serikali kueleza kwamba Mwanyika amekubali kulipa fidia ya TSh bilioni 1.5. Mwanyika na wenzake wawili, Assa Mwaipopo.

KATIBA INASEMA IVI
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-👇🏽

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
 
Tume ya TAIFA ya UCHAGUZI, Kama hamkuliona hilo kosa la Mwayika wa Njombe ni HAKIKA HAMTAONA DOSARI YOYOTE KWENYE UCHAGUZI WA 28/10/2020.

USHAURI:-
WAGOMBEA WOTE WAREJESHENI KWENYE KINYANG'ANYIRO ILI SANDUKU LA KURA LIAMUE.

SUALA LA ULINZI WA KURA, WAACHIWE WAPIGA KURA WENYEWE.
 
Warudishe majina yanayostahili kurudi waondoe watu kama akina Mwanyika na yule mchunga kondoo wa raha yake
NEC ikataaeni dhambi hii vinginevyo hamtajisamehe mpaka Yesu atakaporudi kulichukua Kanisa Lake
 
Bado kuna majinga yanaamini Luna mtu eti anachukia wizi,rushwa na ufisadi kumbe ni tapeli tu kama wenzake.
 
Sasa hilo Jina lilipitaje kwenye kamati kuu na Halimashauri kuu ya CCM ambayo kiongozi wake mkuu anadai ni mpingarushwa. Au ina maana ukilipa unakua msafi kesho yake....!!?
 
Hatari kumbeeee !!!! hivi alitiwa hatiani na kuhukumiwa ? nilipitwa na hii issue alipewa fine au kifungo cha miaka mingapi. Weka humu copy ya hukumu maana kwenye kuweka pingamizi hatuendi na maneno tu mwaga ushahidi huku tupate kukuelewa.
 
Hawa watu wa NEC na CCM, Mungu awape maisha tu. Kuna siku watakaokuwa hai watawaona wamesimamishwa mahakamani.
 
Hivi inakuwaje?Mtu anatajwa Kwenye orodha ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ..anaitwa polisi anakaa siku kadhaa akihojiwa...anaachiliwa.
Anakuja kupewa nafasi ya kugombea ubunge na serikali hiyo hiyo iliyo wahi kum arrest Kwa madawa??..umakini uko wapi?
Kama alisingiziwa je wale wengine hawakusingiziwa?
Na why serikali iwasingizie watu?
Kama hakusingiziwa why mumlete agombee ubunge?..mnaeleza wananchi kitu gani???
 
Mkuu inasikitisha sana..
Yule Mwanyika wa BARRICK/ACACIA alikutwa na kosa la kukwepa kodi..na Mahakama ikamtia hatiani na kumuhukumu..
Leo hii ni mgombea wa CCM Njombe.
 
CCM ni kikundi cha uhalifu. Majangili wote wako ccm! Wachawi wote wako ccm! Mafisadi wote wako ccm! Wavuta bangi wote wako ccm! Wanafiki wote wako ccm! Wahujumu uchumi wote wako ccm!! Wauza madawa ya kulevya wote wako ccm! Wakwepa kodi wote wako ccm!

Hakika ccm hawana tofauti na wanyama aina ya FISI.
 
Ni ushamba kama ule wa kina Lisu 2015 walipoamua kumsafisha EL waliemuita fisadi kwa miaka 8
 
Back
Top Bottom