Tume ya Uchaguzi na suala la Wanafunzi kutolewa madarasani kuhudhuria mikutano ya kampeni

Tume ya Uchaguzi na suala la Wanafunzi kutolewa madarasani kuhudhuria mikutano ya kampeni

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Baada ya wiki moja ya kampeni tumepokea taarifa mbali mbali za mienendo ya kampeni.

Kinachonifanya niandike huu uzi ni kitendo cha NEC kufumbia macho suala la wanafunzi kuamriwa kuacha masomo kwenda kuhudhuria mikutano ya kampeni.

Ni kweli kuwa baadhi ya wanafunzi wana umri wa kutosha kupiga kura, lakini siamini kama ni busara kwao kukatiza masomo kwenda kuhudhuria kampeni.

Haya mambo yalikuwa yanafanyika zamani ambapo hata vyombo vya mawasiliano vilikuwa duni, lakni kwa sasa kama mtu hajahudhuria mkutano wa kampeni bado ana fursa ya kuwapambanisha wagombea (kama anataka) kwa kusikia taarifa zao kwenye vyombo vya habari

Naomba sana tume itoe tamko la kukataza tabia hii inayodumaza elimu za watoto wetu.
 
Ni kule moshi mgombea mwenza Samia Suluhu alikosa wananchi wa kuwapa ahadi zile zile tulizozoea akaitiwa wanafunzi.
 
Siyo mikutano ya kampeni tu, hata mwenge wanafanya hivyo hivyo na sherehe zote za kitaifa. Nafikiri unaona michezo ya Halaiki ikifanywa na wanafunzi ambao hutumia zaidi ya miezi mitatu kujiandaa huku wakikosa masomo!
 
Ngoja Lumumba band waje watoke udenda hapa kukanusha tuhuma hizi.
 
DAS masasi amewatangazia wakuu wa shule siku Magufuli akija siku ya J4, wanafunzi wote wahudhulie kiraia na kuvunja vipindi
 
CCM kipaumbele sio Elimu, ndio maana wanatafuta nyomi kwa kulazimisha watoto wa shule.

Lowassa anasema 1. Elimu 2. Elimu 3. Elimu. Huwezi kukuta wanafunzi wanatolewa darasani hapo, huo uhuni wa maccm miaka mingi. Mwaka huu wamebanwa kila kona
 
1.Wizara ya Elimu Hamlioni hili?
2. Tume ya Uchaguzi mpo?
3.Hivi na nyie waandishi wa habari hivi mnaulizaga maswali gani mkikutana na TUME?
 
Mkuu mtoa maada,hayo ni moja ya wajibu wa mtoto katika kutimiza political responsibility, hakuna anayewalizimisha Bali ni elimu tynayowapa watoto hawa hasa wale wa sekondari, na kuna elimu wanaipata na kuitumia katika masomo yao.

Tatizo chadema mnakwama kwa kukosa elimu ya uraia ndo maana Hanna uzalendo na kazi yenu ni kulia lia tu
 
Bwana! Bwana! Bwana!

Kuitofautisha Tume na CCM kunahtaji darubini Kali.
 
1. Wizara ya Elimu Hamlioni hili?
2. Tume ya Uchaguzi mpo?
3. Hivi na nyie waandishi wa habari hivi mnaulizaga maswali gani mkikutana na TUME?
Thubutuuu

Labda watoe tamko juu ya yule mtoto aliyapanda juu ya mti kumuona Lieu.
Na mataga watakata ule mti
 
Nchi hii ina mambo ya ajabu sana, chochote kinachofanywa na ccm Hakuna wa kuhoji, waandishi wa habari wa Tanzania ndo hamna kitu kabisa
 
Huu upuuzi nlishaukataa siku nyingi.
 
Back
Top Bottom