Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi, NEC ilikuwa kimya kwa TLP na UDP kuiunga mkono CCM iwe kimya pia kwa ACT-Wazalendo

Kweli, wacha nichutame kama sehemu ya uungwana, maana jf sio chombo cha wahalifu, kina hadhi yake. Hata hivyo hali ilivyo sasa ya uchaguzi kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha malalamiko dhidi ya TUME na Msajili kutoka kwa vyama vya upinzani. Malengo ya Msajili na Tume yana mwelekeo unaorandana dhidi ya vyama vya upinzani na chama tawala. Niliposikia kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyeenguliwa kugombea kutoka CCM Bara na Visiwani na hakuna mfanyakazi wa tume anayejisikia aibu kwa tukio kama hilo nikasema sasa hivi Tanzania inaelekea kubaya.
 
Ndani ya hii tume kuna shida na ofisi ya msajili kuna shida kubwa! Siku zote ukiwasikia wamenyanyua mdomo kukemea jambo ujwe ni kwa faida ya chama kilichoko ikulu na si vingnevyo! Baada ya huu uchaguzi mkuu, lazima tudai katiba mpya ili itakayofumua na kuziondoa taasis zote kutoka mfukoni mwa CCM na kuwa taasis huru! Sote kwa pamoja tuendelee kuelimisha watu watumie vema sanduku la kura tukaiweke kando CCM ndipo haya yote yatawezekana!
 
Dah yaani nacheka kweli. Ina maana CCM imekata pumzi hadi inatumia Ofisi ya Msajili wa Vyama kuisaidia? Inafurahisha nikiona CCM inateseka hivyo! Tundu Lissu amekamua jiwe hadi linatoka maji!
 
Haya ni matawi ya CCM,
1.Jeshi la polisi
2.tume ya uchaguzi
3.mahakama


Tume ilipoona CCM inaungwa mkono na hivo vyama walifurahi ,na walipoona chadema inaungwa mkono na ACT wakachukia .

Tume inaumia sana CCM inapozidiwa kete
Mbona umesahau na bunge?
 
Matusi ni dalili mathubuti kabisa ya kuishiwa hoja
Kuna hoja gani unaweza kuijenga kuhusu tume? Unataka tuanze kuipqmba kwa ujinga inayoufanya dhidi ya wagombea wa upinzani?
 
Hayo ndio Yale tunayosema uwepo was wazalendo maslahi no hasara kwa taifa upande wao hawaoni, kwajirani zao wanaona. Ndio maana hayo Mambo yanatakiwa fafikie mwisho na mwisho haupo mbali.
 
Naanza kuliona tatizo toka kwako mtoa mada na mashabiki wako, nakukumbusha tu Muungano au ushirikiano wa vyama liko chini ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA na sio TUME.
kuungana baada ya UTEUZI ni kosa
kuna mgombea ubunge kutoka ACT alijiondoa kwenye kampeni na kuunga juhudi, je hilo ni kosa?
 
kuna mgombea ubunge kutoka ACT alijiondoa kwenye kampeni na kuunga juhudi, je hilo ni kosa?
Act wazalendo inawaomba wapenzi wa chama au wagombea wao wampe kura Lisu, hiyo ndio msajili hataki! Anataka kuwasawishi tume wachukue hatua gani? Au msajili anaweza kuzuia wanachama wa chama chochote kumpa kura alie wa chama kingine? Naomba kujua
 
Kuna hoja gani unaweza kuijenga kuhusu tume? Unataka tuanze kuipqmba kwa ujinga inayoufanya dhidi ya wagombea wa upinzani?
Tume ilishachukua hatua dhidi ya TLP na UDP, unataka ifanye nini tena?
 
Hii Tume imejichanganya tayari....

Hata wananchi wataanza kuidharau...isipojirekebisha mapema.
 
Swali fikirishi Je rafiki yako makubaliano yenu nilazima muandikishane? nijuavyo mimi mengi huwa tunaonge na tunatimiza mfano ukimuahidi mpenzi wako kumnunulia simu je mnaandikisha? hahaa!
 
Hata kwa maandamano halali unaweza kuipata tume huru, Basi tu kwavile watu bado Wana matumaini bado na kisanduku Cha kura wakati vyama vingine vikiendelea kukomaa kisiasa.
 
Watu watakuja kukuelewa baadaye
 
Huyu mupe yure muruke....kunya anye kwio akinya bata kahara
Hivi ACT Wazalendo na CHADEMA wakikaidi huu upuuzi, NEC na Msajili wa vyama, watafanya nini? Kuna mahali wataenda kushtaki? Najua ACT na CHADEMA wana mahali pa kushtaki.
 
Na ninavyoijua Tanzania, hawa ni wengi kuliko watu wa aina yako. Na hao wakiamua mnang'oka asubuhi sana.
 
Naanza kuliona tatizo toka kwako mtoa mada na mashabiki wako, nakukumbusha tu Muungano au ushirikiano wa vyama liko chini ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA na sio TUME.
kuungana baada ya UTEUZI ni kosa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…