Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi, NEC ilikuwa kimya kwa TLP na UDP kuiunga mkono CCM iwe kimya pia kwa ACT-Wazalendo

Nguruka, nyangabo,bweru, itebula,mganza, Nguruka Kati,lugongoni A&B hapawezi pakatoa mtu mwenye Mawazo kama wewe. Unawaaibisha wana MAGEUZI wa Nguruka.
 
Tume inafanya kazi ya CCM, huu ni mwendelezo tu walianza na kuwajazia form wagombea wa CCM
 
Ofisi hizi mbili zinafanya mambo kama yale yaliyokuwa yakifanywa na wakoloni kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika na Uhuru wa Zanzibar wakati wa chaguzi. Kuna Uzi mwembamba Sana unaotenganisha tabia ya tume/msajili Sasa na ile tume ya wakoloni nyakati za uchaguzi.
 
Umeshawahi kuhudhuria mikutano ya tundu lissu hivi karibuni? inaonekana huna habari na kinachoendelea wewe. Tume ikiwa huru na ya haki lolote linawezekana.

juzi nmeskia anasema ongezeko la chakula sio maendeleo, daah nkasema apa bangi inahitajika kuwaelewa maaana anaongea pumba juu ya pumba! kama imefika hatua chakula nacho sio maendeleo basi walio upande wa lissu wa moyo mgumu sana
 

Hahahaaaa haya bwana! Ila Sidhani kama Tume na Msajili wanamalengo yaliyosawa.
 
Hivi ACT Wazalendo na CHADEMA wakikaidi huu upuuzi, NEC na Msajili wa vyama, watafanya nini? Kuna mahali wataenda kushtaki? Najua ACT na CHADEMA wana mahali pa kushtaki.
NEC inahusikaje hapo jamani. Najaribu kuwaelewesha lakini hamuelewi. Acheni ushabiki maandazi. Istoshe wenye chama chao nadhani watakua wameelewa.
 
Naanza kuliona tatizo toka kwako mtoa mada na mashabiki wako, nakukumbusha tu Muungano au ushirikiano wa vyama liko chini ya MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA na sio TUME.
kuungana baada ya UTEUZI ni kosa
Tlp walitangaza kuunga mkono magufuli je nao?
 
Mkuu hoja rahisi sana...unapotosha .
Wapo watu wengi tu hawapo katika makundi hayo na bado wanamuunga mkono TL .na wengine wapo sekta nyeti(siwezi kutaja humu)

Au labda ni hoja ya kujifariji!
 
Hao vijana unaowasema vibaya wa vijiweni wanatokana na kutokuwa na ajira! Ambayo kwa namna moja ni Tatizo la Uongozi uliopo madarakani.
 
Tume inafanya kazi ya CCM, huu ni mwendelezo tu walianza na kuwajazia form wagombea wa CCM
Kwakua si muelewa basi ngoja nikuache. Mimi nikumusaidia tu kutofautisha baina ya Taasisi hizo mbili. TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA. Sasa maamuzi ya Msajili halafu mahakamani Unamwita Tume. Au kosa alitende CUF halafu malalamiko unayapeleka Chadema hapo unakua umepatia kweli au umeingia porini wewe na wenzako.
 
Ninachojiuliza ni je nec wanaathirikaje na wagombea kuungana mkono🤔🤔😎😎

Mbona wabunge na madiwani walikazana kununuliwa na ccm huku wakisema wanaunga mkono juhudi nec walikemea huu uchafu?
 
NEC inahusikaje hapo jamani. Najaribu kuwaelewesha lakini hamuelewi. Acheni ushabiki maandazi. Istoshe wenye chama chao nadhani watakua wameelewa.
Mbona jazba? Wewe ushabiki wako kinyesi vipi. Sawa NEC hawahusiki, mbona husemi msajili atashtaki wapi?
 
Mnakosa hoja ya kuwashawishi wapiga kura kwa kuamini kuwa Magufuli akizushiwa, kwenye kampeni, tuhuma za matumuzi mabaya ya kodi za wananchi atachukiwa na wapiga kura.

Taratibu tuchambue aina ya wapiga kura:
1) Wasomi kindakindaki, wanajua maana na matokeo chanya ya kuwekeza kwenye vichocheo vya kukuza uchumi (economic drivers).
2) Asilimia zaidi ya 70 inayoishi vijijini kweli haijui maana ya ununuzi wa ndege, ujenzi wa flyovers, nk. Lakini hawa wakieleweshwa umuhimu wake kwa usafirishaji mazao yao au kuwaletea bidhaa muhimu kwa mahitaji yao, kwa haraka iwezekanavyo, watakuelewa.
3) Ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati, si kipaumbele kwa jamii ndogo yenye uwezo wa kumudu gharama za afya kwenye huduma za afya binafsi. Kwa mwanakijiji ambaye alilazimika kufunga safari ndefu kufuata huduma hiyo, kumwambia ni upotevu wa kodi yao, hakika hakuelewi.
4) Ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato, kwa Watanzania wasio wa huko, itakuwa vigumu kuelewa kama ni matumizi mazuri ya kodi yao. Kwa wakazi wa huko, aghalabu wanao uwanja wa ndege, kesho yumkini watautumia kwa usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao kwa haraka.
5) Bei ya bidhaa za kilimo km korosho, kahawa kuteremka inakuwa nafuu kwa mnunuzi. Kwa mkulima ni hasara tu pale anaposhindwa kupata soko la uhakika kuweza kurejesha angalau gharama zake.

Mifano iko mingi, itoshe kusema, mchambuzi makini anaweza kubaini kundi gani lina turufu ya nani ataibuka mshindi.
 
Makaburu na wareno hawakufukuzwa kwasababu hawakujenga flyovers na viwanja vya ndege South Africa na Angola, Bali walifujuzwa kwasababu waliwanyima wananchi mahitaji ya msingi Kama chakula, elimu, haki ya kusikilizwa, kujieleza , na kujiamulia mambo yao. Basic needs should come first before the secondary and tertiary needs. Kwa miaka 60 CCM ilipaswa iwe imeshafuta shida za maji, umeme, hispitali, madawa na kilimo Cha jembe la mkono na kutegemea mvua. Ni aibu kwa chama kilichotawala kwa miaka 60 kutaka kisifiwe leo kwa kusambaza umeme, maji, hospitali, barabara.

CCM ilitakiwa Sasa hivi itafute sifa kwa kupeleka satellite yetu angani, kutengeneza magari, matrectors, madawa ya binadamu na mifugo, mitambo ya kuvunia mazao mashambani combine harvesters na misitu.

Lazima
 
Tume inabidi wajifunze mtoto mmoja akifanya makosa ukimwacha na mwingine kesho atafanya kubwa zaidi ,na utashindwa kumwonya. Hicho ndicho kinachotokea hivi sasa. Na lissu anatumia udhaifu wao huo Huo. Ni kama vile na wao tume wameathirika na spana za Lissu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…