Mnakosa hoja ya kuwashawishi wapiga kura kwa kuamini kuwa Magufuli akizushiwa, kwenye kampeni, tuhuma za matumuzi mabaya ya kodi za wananchi atachukiwa na wapiga kura.
Taratibu tuchambue aina ya wapiga kura:
1) Wasomi kindakindaki, wanajua maana na matokeo chanya ya kuwekeza kwenye vichocheo vya kukuza uchumi (economic drivers).
2) Asilimia zaidi ya 70 inayoishi vijijini kweli haijui maana ya ununuzi wa ndege, ujenzi wa flyovers, nk. Lakini hawa wakieleweshwa umuhimu wake kwa usafirishaji mazao yao au kuwaletea bidhaa muhimu kwa mahitaji yao, kwa haraka iwezekanavyo, watakuelewa.
3) Ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati, si kipaumbele kwa jamii ndogo yenye uwezo wa kumudu gharama za afya kwenye huduma za afya binafsi. Kwa mwanakijiji ambaye alilazimika kufunga safari ndefu kufuata huduma hiyo, kumwambia ni upotevu wa kodi yao, hakika hakuelewi.
4) Ujenzi wa kiwanja cha ndege Chato, kwa Watanzania wasio wa huko, itakuwa vigumu kuelewa kama ni matumizi mazuri ya kodi yao. Kwa wakazi wa huko, aghalabu wanao uwanja wa ndege, kesho yumkini watautumia kwa usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao kwa haraka.
5) Bei ya bidhaa za kilimo km korosho, kahawa kuteremka inakuwa nafuu kwa mnunuzi. Kwa mkulima ni hasara tu pale anaposhindwa kupata soko la uhakika kuweza kurejesha angalau gharama zake.
Mifano iko mingi, itoshe kusema, mchambuzi makini anaweza kubaini kundi gani lina turufu ya nani ataibuka mshindi.