Tume ya Uchaguzi Uganda yamtangaza Museveni mshindi, Besigye apinga matokeo

Tume ya Uchaguzi Uganda yamtangaza Museveni mshindi, Besigye apinga matokeo

"At least kwetu kwetu waliona AIBU" - Babu Sikare
ImageUploadedByJamiiForums1455979339.881031.jpg
 
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Museveni ametangazwa mshindi licha ya kwamba kuna vituo ambavyo bado matokeo hayajatangazwa. Dkt Kiggundu amesema matokeo ya vituo hivyo hayawezi kubadilisha mambo. Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.
chanzo : BBC
Imenikumbusha uchaguzi wa mwaka jana!!! AFRICA TUKO MBALI SANA!!!
 
Sioni haja ya kufanya chaguzi kwa nchi za Afrika. Mauzauza ni mengi mfano mkwamo uliopo Zanzibar nchini Tanzania baada ya kinachoitwa uchaguzi kumalizika kwa kumweka magufuli madarakani Tanzania bara na kumgomea Sharif Zanzibar, haya leo Museveni Uganda. Tujikubali tu kuwa tunajitawala kidikteta
 
Aibu kubwa kwa viongozi wa EAC.Hivi haingii akilini watu wanaona wapinzani bi RAIA halali wa nchi zao??Tatizo bi Rushwa na ufisadi.Wamezoea kula rushwa Ba ufisadi bila kuangalia wananchi wa kawaida.Sijui kwa Uganda lakini huko vita ya wenyewe kwa wenyewe anakuja.Sababu Kiiza ni Uganda yule mwingine asili ya kitutsi.Kuacha madaraka kwa watutsi siyo rahisi
 
Tanzania Uganda ea nzima hakuna haja ya Uchaguzi wa nacheza pesa ilhali wanajua wanaimba kura ili washinde
 
Kuna baadhi ya nchi za Africa ni bora tu kurudi kwenye chama kimoja.
 
Miraisi ya Afrika ndivyo ilivyo.... King'ang'anizi.
 
@Mk24 Uchaguzi Kenya ni lini? Kenya lazma kinuke tena!! Odinga hatakubali na wakenya sa hivi hawampendi Uhuru Kenyatta
 
Back
Top Bottom