Mrs Kharusy
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 1,244
- 671
Matokeo yaliyofutwa ni URAISI WA ZANZIBAR na WAWAKILISHI.
Matatizo ni KARATASI ZA URAISI ZANZIBAR sio BARA!!! ..hivi jamani watu wa UKAWA kwanini mnataka kuleta vurugu ??
uchaguzi zanzibar haukuwa huru na haki na kuna kura za muungano kwenye same ballot boxes, so tunaamini kura za bara pia hazikusimamiwa kwa uhuru na haki.
either raisi wa muungano asitangazwe mpaka zenji warudie au na huku matokeo yafutwe.
Zilizofutwa ni Matokeo Ya Urais na Sio Ya Wabunge, madiwani wala Wawakilishi. Kwa hiyo Kura za Ubunge ziko pale pale
ni ngumu sana kuproove kwamba kura za urais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania hazijaathirika na hizo sababu za zec. Ikiwa mpiga kura ni yule yule, kituo ni kile kile, msimamizi wa kituo ni yule yule na mazingira ni yale yale.
rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania anatokana na kura za urais za bara na visiwani, hivyo kama kura za kura za kule zanzibar ni batili-ndio maana uchaguzi umefutwa, means hata kura za urais za jamuhuri ya muungano wa tanzania ni batili pia.
Kura zote ni batili, other wise tume-nec ihesabu tu kura za huku bara, na isubiri mpaka zanzibar watakapo fanya uchaguzi wao tena, ndipo matokeo ya urasi wa jmt yajumlishwe upya. Hivyo kikwete by that time ataendelea kubaki madarakani
wale waliosema tareh 29 oktoba watamuapisha rais basi wasitukane mamba na huku hawaja vuka mto. Haki ya mtu huwa haipotei.
Asante mungu
Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.
Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi YOYOTE ?? ?? ?? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.... Wao wanapiga kote, kama Jimbo lolote, kura zinapigwa hierarchical ...(sijui kiswahili wanaitaje).
Muda si mrefu jf itapotea hewani.
Kwa akili zako fupi unahisi mamvi angeongoza. Ndio maana muliambiwa malofa.
Tatizo ni nini hasaa?? Vimetumika vktuo hivyo hivyo na wasimamizi ndio hao hao na wapiga kura ni hao hao...yakibatilika yabatilike kote
Wanasheria tusaidieni:
Kuna jurisdiction mbili hapa..moja inasimamiwa na ZEC na nyingine na NEC.
kwa kuwa ZEC imesema uchaguzi haukuwa huru na wa haki, je ni nini kitahalalisha uchaguzi uliosimamiwa na NEC? Kumbuka, ni sehemu ileile, wasimamizi walewale na wapiga kura wale wale, waliopiga kura chini ya ZEC na NEC.
Je, kitendo cha kuahirisha uchaguzi huu wa ZEC kitasababisha ucheleweshwaji wa matokeo ya NEC? Kumbuka, tayari NEC imeshatoa matokeo yaliyosimamiwa na ZEC lakini ni kwa ajili ya NEC.
Au kila tume ilikuwa na wasimamizi wake?