Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Lowassa na wewe JITANGAZIE USHINDI ILI UCHAGUZI URUDIWE na huku BARA.
 
Hapa ndipo tuone itavyokuwa ni vipi; maana:-

1. Ikiwa ni kweli uchaguzi wa rais wa JMT unasimamiwa na NEC na si ZEC, tuelezwe kulikuwa na daftari tofauti la wapiga kura wa kura za urais wa JMT?

2. Je, kulikuwa na wasimamizi wawili tofauti katika kila kituo na jimbo mmoja kwa ajili ya kura za rais wa JMT na mwingine rais wa SMZ?

3. Je, kulikuwa na vituo tofauti kabisa kwa ajili kupigia kura za rais wa JMT na rais wa SMZ?,

4. Je, kura hizi zilipigwa siku tofauti kwa kura za rais wa JMT siku yake na rais wa SMZ siku yake?

Kama jibu ni HAPANA kwa angalau swali moja katika hayo; ni wazi kwamba "uchaguzi huu na matokeo yake yote" yafutwe (kama nilivyonukuu katika taarifa ya ZEC si mimi)
 
Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.

Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi YOYOTE ?? ?? ?? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.... Wao wanapiga kote, sisi tunapiga ya kwetu tu kama Jimbo lolote, kura zinapigwa hierarchical ..kijimbo na kitaifa, ARUSHA WAMEPIGA KURA ZA RAISI BARA LAKINI UBUNGE BAADAE. Kwahiyo Zanzibar za PAMOJA URAISI BARA ni sawa ila majimbo yaani RAISI wao ndio zinarudiwa.

Mkuu mi ndio sijakuelewa au malezo yako ndio hayaeleweki ...!?

Muungano huu unaufahamu vizuri... na athari zake umeziona au una tongo ...!?

Ni aina gani ya Muungano tulionao hapo...!?

Suali linalofuata linatokana na jibu hapo juu... 👇

Zanzibar ni Nchi au ni Mkoa katika Mikoa ya Tanzania ...!?
 
Tunaomba ututajie mikoa ambayo uchaguzi wa RAIS umeahirishwa??

Chaguzi nyingi mkoani zilizoahirishwa ni za UDAWANI na KATA. Lakini kila jimbo tanzania BARA wamepiga kura za RAISI. Mfano Kimara Stop Over hawajapiga kura za DIWANI. ARUSHA MJINI, LUDEWE hawajapiga kura za MBUNGE.

Nadhani hukunielewa, nimesema maeneo kama Arusha hawakupiga Ubunge, wamepiga ya Raisi na Ubunge utapigwa baadaye. Ni sawa na Zanzibar watarudia ya Raisi wao tu, sio Raisi wa MUungano.
 
Mbona kuna mikoa mingi uchaguzi umehairishwa, kwanini USIRUDIWE ZANZIBAR ??? ..Hii ni internal matter ya wana Zanzibar sio swala la kila mtu. Leo hii Ubungo wakitaka kurudia uchaguzi utafutwa na waanze upya, HAUWEZI kusema TANZANIA nzima WARUDIE UCHAGUZI.

Kwani Bara mliona picha ya MAALIM SEIF kwenye karatasi YOYOTE ?? ?? ?? Hili tatizo ni LOCAL jimboni Zanzibar sio TANZANIA nzima.... Wao wanapiga kote, kama Jimbo lolote, kura zinapigwa hierarchical ...(sijui kiswahili wanaitaje).

Mkuu hapo kwenye kuiregard Zenji km kajimbo ka uchaguzi ni matusi makubwa kwa wanavisiwani na ni kebehi kwa washirika wote wa Muungano.
Uchaguzi wote urudiwe si zenj wala Bara, na kiranja wa uchaguzi awe huru!
 
Ugomvi upo kwa Urais na sio kwa wabunge,, madiwani etc!
Mmetuangusha hamkumtilia kura Lowassa basi sisi hatuna tena tamaa ya kuupata Urais wa Zanzibar. Hawatupi, hawatupi, hawatupi n'go!!!!!

tumeshakosea
 
Mbona bara hawafuti, kwao wao hawakupiga kura za rais wa muungano?
ZEC wamejichanganya tayari na NEC wameshaonyesha dalili za kuchakachua kura lakini Wananchi wamenyamaza japo wanaelewa. Kosa kubwa ni kutangaza huku bara na hizi irregularities zote.
Inaweza kumchukua mtu masaa yasiyozidi kumi kusoma vitabu au makala na kuelewa ni jinsi gani amani ilitoweka Congo, Liberia, Libya ambako walikuwa wanalipiwa hadi mahali nk!
Watawala wetu hata kama hamna uwezo na skills za kuongoza, hebu shughulisheni vichwa vyenu kidogo msituingize kwenye matatizo.
 
Mfano: Tanzania bara Jimbo la ubungo, unapewa karatasi TATU (Raisi muungano, Mbunge na Diwani) . kwa ZANZIBAR unapewa 4 (Raisi wa Muungano, Raisi wa Zanzibar, Mwakilishi na Diwani) tatizo liko kwenye hizi tatu za mwisho sio ile ya TANZANIA yote!!! TANZANIA BARA Hawana karatasi ya nne ya URAISI ZANZIBAR kwahiyo HAWARUDII.

Ndo maana tutaka serekali tatu
 
Hawa watawala wa Tz ni viroja.

Kama kurudiwa usimamiwe na UN au CommonWealth. ZEC imeshapoteza uaminifu.

Walisema Upinzani ukishinda jeshi linachukua nchi. Je upinzani umeshinda?

Ishinde CCM na Tume NEC au ZEC ifute uchaguzi wote? Haijawahi kutokea wala haitotokea.

Hii Tume ZEC imenikumbusha ufujaji wa fedha za umma uliofanyika kuunda Tume ya Warioba ili kupata Katiba Mpya.

ZEC imeiweka NEC katika wakati mgumu. ZEC ndio imesimamia kura za Magufuli na Lowassa huko Zanzibar. Nini kinafuata baada ya ZEC kufuta uchaguzi wote?
 
Hapa ndipo tuone itavyokuwa ni vipi; maana:-

1. Ikiwa ni kweli uchaguzi wa rais wa JMT unasimamiwa na NEC na si ZEC, tuelezwe kulikuwa na daftari tofauti la wapiga kura wa kura za urais wa JMT?

2. Je, kulikuwa na wasimamizi wawili tofauti katika kila kituo na jimbo mmoja kwa ajili ya kura za rais wa JMT na mwingine rais wa SMZ?

3. Je, kulikuwa na vituo tofauti kabisa kwa ajili kupigia kura za rais wa JMT na rais wa SMZ?,

4. Je, kura hizi zilipigwa siku tofauti kwa kura za rais wa JMT siku yake na rais wa SMZ siku yake?

Kama jibu ni HAPANA kwa angalau swali moja katika hayo; ni wazi kwamba "uchaguzi huu na matokeo yake yote" yafutwe (kama nilivyonukuu katika taarifa ya ZEC si mimi)

That's points! hayo ndio matatizo ya kutoa maamuzi ya kukurupuka. Tunataka Uchaguzi mpya tanzania Nzima chini ya UN na si hii tume ya CCM!
 
Mkuu mi ndio sijakuelewa au malezo yako ndio hayaeleweki ...!?

Muungano huu unaufahamu vizuri... na athari zake umeziona au una tongo ...!?

Ni aina gani ya Muungano tulionao hapo...!?

Suali linalofuata linatokana na jibu hapo juu... 

Zanzibar ni Nchi au ni Mkoa katika Mikoa ya Tanzania ...!?

Zanzibar ni nchi, lakini kikatiba ya Muungano, iko CHINI ya mwamvuli wa TANZANIA. ni sawa na Tanganyika (Bara) iko chini ya Mwamvuli wa MUUNGANO. ndio mana Bara hawapigii kura Raisi wa Zanzibar, ila SOTE tunapigia Raisi wa MUUNGANO.
 
Ya bara hayawez futwa sababu
Kura tofauti kuna karatasi ya rais JMT na karatasi ya kura ya rais WA serikali ya mapinduz znz ni vitu tofauti na mara nyingi tarehe ya kura inakuwa tofauti lkn ths Tim wameweka tareh moja
 
Hizi ni tetesi au ukweli? Vituo vya TV na radio vyote mbona kimya kuhusu habari hii?
 
WASHENZI jiti la matako liliwanganda walikuwa hawana namna kumtangaza shein noma kumtangaza aliye shinda noma sasa tufanyeje na maozaver pamoja na mabalozi waliwaambia CCM kama mutamtangaza shein na ikitokeya kuuliwa watu basi hague mutakwenda
 
Katika hali ya kushtua Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC) imetangaza kuyafuta Matokeo ya urais wa Zanzibar.

Yadaiwa Uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.

Imeahidi kutangaza tarehe rasmi ya kurudiwa uchaguzi.

====
Statement:

vU05dG9.jpg

EdIidYV.jpg

BLhdlD9.jpg

VIDEO:

Chanzo: ZBC TV

mods badilisheni kichwa cha habari matokeo yaliofutwa ni Urais na Uwakilishi. Jiongozeni basi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom