Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Ukawa toeni tamka mara moja. Tupo tayari kwa lolote. Huu ni upuuzi wa hali ya juuu
 
Uchaguzi wa muungano hausimamiwi na ZEC, ni NEC mkuu...

kumbuka masanduku ya kura yanayotumika ni yaleyale. ina maana kura zitamwagwa chini zichambuliwe za muungano zihesabiwe?
 
Wana jamvi
Ukurasa mpya wa kisiasa umefunguka nchini.
-Hivi inawezekana uchaguzi ukakosa uhuru na haki kwa kura ya urais tu?
-Hivi kasoro hizo zimeonekana baada ya Maalim kujitangazia matokeo?

Haramu n Halali havijawahi kukaa chungu kimoja. Urais haramu ndani ya chungu halali cha urais wa jamhuri, ubunge, uwakilishi, udiwani.

Hata tume ni haram

Nakubaliana na wewe, haram
 
Hii nchi ni ya maajabu sana. utadhani iliumbwa kwa aijili ya watu wachache tu. Suala kubwa na la kitaifa kama hili watawala wanaliwekea mizaha mingi utadhani wanafanya kwa hisani tu. Matokeo yake,ZEC/NEC wanatengeneza maswali mengi vichwani mwa wananchi bila kujua athali zake. Kulishindikana nini kuita vyombo vya habari kama wawakilishi wa wananchi ili kuuliza maswali na kuondoa dukuduku lote linaloenea?
Nina imani waandishi wa habari wangeuliza maswali ambayo yangewaweka wengine wazi kuhusu kurudia au kutorudia chaguzi za bara na kuondoa unsettlement miongoni mwa jamii yetu.
Yaani nchi kama ya kwao wenyewe na wanatuonjesha tu.
 
Kikwete na Mkapa ndio chanzo cha matatizo yote haya Dr.Shein alishakubali kusign kushindwa sijawahi ona kiongozi mnafiki kama kikwete chama mbele nchi nyuma sidhani hata kama anajua maana ya democracy kilaza siku zote ni kilaza tu

mjenga nchi ndo mubomoa nchi,tuna viongozi u.sh.zi
 
Wana jamvi
Ukurasa mpya wa kisiasa umefunguka nchini.
-Hivi inawezekana uchaguzi ukakosa uhuru na haki kwa kura ya urais tu?
-Hivi kasoro hizo zimeonekana baada ya Maalim kujitangazia matokeo?

Haramu n Halali havijawahi kukaa chungu kimoja. Urais haramu ndani ya chungu halali cha urais wa jamhuri, ubunge, uwakilishi, udiwani.

Hata tume ni haram


Haramu pale CCM inapochakachua halafu bado inashindwa uchaguzi.
 
Ya bara hayawez futwa sababu
Kura tofauti kuna karatasi ya rais JMT na karatasi ya kura ya rais WA serikali ya mapinduz znz ni vitu tofauti na mara nyingi tarehe ya kura inakuwa tofauti lkn ths Tim wameweka tareh moja

Moja ya sababu iliyotolewa na ZEC ni kuwa kuna watu walizuiliwa kuja kupiga kura kama walifahamika ni wafuasi wa chama kingine. Sasa kama ni hivyo kwani hao watu waliozuiliwa, waliweza kupiga kura ya rais wa muungano lakini ikashindikana kwa rais wa znz tu!
 
HUU NI MTAZAMO WANGU MIMI JUU YA KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI

Tanzania ni nchi iliyo tokana na muungano wa Nchi mbili yaani Zanzibar na Tanganyika, Nchi hizi zimefanikiwa kusimamisha historia ya amani tokea Muungano mwaka 1964. Na mpaka sasa ni takriban miaka 50 , Watanzania tunavumiliana na kusheshimiana.

Zanzibar imekuwa chini ya CCM tokea kpindi hicho na Maraisi wake kwa Awamu zote walitokana na ushindi wa kura kwa kupitia chama cha Mapinduzi CCM. Na mpaka leo hii Zanzibar inaongozwa na Raisi aliye tokea chama cha CCM.

Mwaka huu Wazanzibari walikuwa na shauku kubwa ya kufanya mabadiliko, wakitana atleast Wapate Raisi kutokea chama kingine. Chama kikuu cha upinzani Zanzibar ni CUF. Ambacho kipo chini ya mgombea wa Uraisi ndugu Maalim Seif, aliye kuwa makamu wa Kwanza wa Raisi wa Selikali ya mapinduzi Zanzibar, baada ya kuunda selikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2010.

Mtazamo wangu katika matokeo ya mwaka huu baada ya ndugu Maalim Seif kuamua kujitangaza kuwa ameshinda na idadi ya kura anazo kulingana na vituo vilivyo piga kura na nyaraka zilizo sainiwa na mawakala wa vituo kutoka vyama vyote vilivyo shiriki uchaguzi, huku akilalamika kuna rafu zimechezeka katika matokeo yanayo tangazwa na NEC.

Cha kushangaza Watanzania tunaambiwa uchaguzi unarudiwa. unarudiwa kwasababu kuu tatu kama sio nne. Kujitangaza kwa Maalim Seif kabla uhesabuji wa kura haujamalizika, idadi ya kura kuzidi idadi ya wapiga kura kwa baadhi ya vituo, pia uchaguzi huo haukuwa huru na haki, naweza sema nikwlei....

MTAZAMO WANGU MIMI : kurudia uchaguzi sio jambo sahihi. NA KAMA TUNAAMUA KURUDIA UCHAGUZI, BASI TURUDIE TANZANIA NZIMA, NA SI KIPANDE KIMOJA TU CHA ZANZIBAR. Ninaamini, sehemu zilizo zidi kura kuliko wapiga kura, zipo kura za wagombea wa uraisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania. Na kwakuwa Zanzibar ni kipande kimoja wapo cha Tanzania, sioni sababu kwa nusu ya Tanzana irudie uchaguzi halafu Nusu nyingine isirudie uchaguzi.. hii ni Jamuhuru ya Muungano ya Tanzania, sote ni watanzania, sote tunachagua Raisi wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.

GHARAMA ZA UCHAGUZI
Tunafikiria gharama za kuwalipa mawakala, kuchapisha ballot papers, kuwalipa wasimamizi, na pia vifaa vingine vya stationaries, gharama za mafuta na magari kusafirisha vifaa hivyo katka vituo mbalimbali, na kurudisha sehemu ya kuhesabia na gharama za ulinzi, nani atazicover. Je ni uzembe wa nani aliye sababsha kura feki ziingie kwenye asanduku ya kura? Hao wazembe watachukuliwa hatua gani?

Musichukulie hili suala kiwepesi sana lakini Watanzania tuawaaminisha vipi kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki na sio kujaribu kukwanyua haki ya chama Fulani kilicho shinda?

Napenda kuwaomba Watanzania kuwa na moyo wa subira, wavumilivu, lakini ikitokea idadi ya wapiga kura ikapungua zaidi tume ishangae, kwani watanzania wamekuwa waoga kwa vitisho vilivyo fanywa kipindi hiki kifupi cha kuchagua viongozi wao.
 
Zanzibar ni kama Jimbo, wao kama wamevuruga, sio Tanzania nzima warudi.

Sijui kwanini ZEC hawaelezi vizuri, naona watu wa Bara wanashindwa kutatua chemsha bongo/brain teaser ya kilichotokea.

Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, kura za zanzibar zinaathiri matokeo ya tanzania kwa ujumla.
Inshort tumepangua goli la mkono hapo Zanzibar.
 
Leo tume ya taifa ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza rasmi kufuta matokeo yote ya urais Zanzibar na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe!

Moja ya sababu mama na ya msingi ya ZEC ni kutokana na idadi kubwa ya kura kuliko idadi kamili ya wapiga kura hasa wa visiwa vya Pemba.

Kimsingi hilo lina athari hata kwa upande wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Kwa wenye uelewa wa upigaji kura wa kule watanielewa)

Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema ndugu Edward Lowassa amejitangaza kuwa katika matokeo ya vijana wa UKAWA waliokuwa wakifanya majumuisho alikuwa anaongoza kwa 60% kimsingi angekuwa ndiye mshindi.

Katika dai lingine la ZEC ni hatua ya mgombea kujitangaza mshindi huku akiwa ameingilia kazi za tume. Lowassa amefanya hivyo na Makamba kwa upande wa CCM alimtangaza mgombea wao kuwa wangemtangaza rasmi kuwa rais mteule leo!

Achilia mbali hayo, kuna malalamiko ya dhahiri kutoka maeneo mengi na yenye ushahidi usio na shaka kuwa kuna uchskachuaji mkubwa sana!

Pia NEC wanapataje mamlaka ya kuhalalisha kura za Zanzibar wakati mwenye mamlaka makuu (ZEC) amebatilisha kura hizo?

Ni muda wa kuonyesha kuwa madai ya ZEC ni ya kweli na siyo yenye msukumo maalum! NEC wachukue hatua ili kuzuia uwepo mkubwa wa sintofahamu inayoendelea kujitokeza!
 
Unafuta uchaguzi bila kutaja kifungu cha sheria kinachokupa mamlaka hayo!!!
 
Kiukweli maalim sefu wanamuonea sana kisa kaongoza yeye uchaguzi ni batili angekuwa anaongoza shein ungekuwa harali.. Hivi demokrasia mnayoihubili iko wapi jamani
 
Rasim ya warioba ilikuwa na vipengele vizuri kuhusu serikali tatu sasa Leo tutaona kikwete na NEC watakavyo haha
 
Mkuu matokeo ysliyofutwa ni ya serikali ya mapinduzi na sii ya muungano.
Tambua kwamba wazanzibar wamechagua rais wa Zanzibar na rais wa muungano.
Na kasoro zipo kwenye uchaguzi wa rais wa Zanzibar na sii rais wa muungano.
Inashangaza basi kwa sababu ukisoma sababu za kufutwa Uchaguzi ni dhairi ziliathiri uchaguzi wote. Kumbuka ni ZEC ndiyo inasimamia uchaguzi mzima ukiwemo wa wabunge na Rais wa JMT (kwa niaba ya NEC) na matatizo ya taratibu yataathiri kotekote. Na kwa jinsi hiyo Tume kwa maana ya NEC je ina uwezo wa kutangaza mshindi wa urais wa JMT wakati upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano haijapiga kura. Hata kama idadi yao haitaathiri matokeo lakini kutaleta mpasuko mwingine wa muungano wetu kwa mantiki kuwa Rais aliyechaguliwa hakuungwa mkono na upande mmoja wa muungano!
 
Back
Top Bottom