HUU NI MTAZAMO WANGU MIMI JUU YA KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI
Tanzania ni nchi iliyo tokana na muungano wa Nchi mbili yaani Zanzibar na Tanganyika, Nchi hizi zimefanikiwa kusimamisha historia ya amani tokea Muungano mwaka 1964. Na mpaka sasa ni takriban miaka 50 , Watanzania tunavumiliana na kusheshimiana.
Zanzibar imekuwa chini ya CCM tokea kpindi hicho na Maraisi wake kwa Awamu zote walitokana na ushindi wa kura kwa kupitia chama cha Mapinduzi CCM. Na mpaka leo hii Zanzibar inaongozwa na Raisi aliye tokea chama cha CCM.
Mwaka huu Wazanzibari walikuwa na shauku kubwa ya kufanya mabadiliko, wakitana atleast Wapate Raisi kutokea chama kingine. Chama kikuu cha upinzani Zanzibar ni CUF. Ambacho kipo chini ya mgombea wa Uraisi ndugu Maalim Seif, aliye kuwa makamu wa Kwanza wa Raisi wa Selikali ya mapinduzi Zanzibar, baada ya kuunda selikali ya umoja wa kitaifa mwaka 2010.
Mtazamo wangu katika matokeo ya mwaka huu baada ya ndugu Maalim Seif kuamua kujitangaza kuwa ameshinda na idadi ya kura anazo kulingana na vituo vilivyo piga kura na nyaraka zilizo sainiwa na mawakala wa vituo kutoka vyama vyote vilivyo shiriki uchaguzi, huku akilalamika kuna rafu zimechezeka katika matokeo yanayo tangazwa na NEC.
Cha kushangaza Watanzania tunaambiwa uchaguzi unarudiwa. unarudiwa kwasababu kuu tatu kama sio nne. Kujitangaza kwa Maalim Seif kabla uhesabuji wa kura haujamalizika, idadi ya kura kuzidi idadi ya wapiga kura kwa baadhi ya vituo, pia uchaguzi huo haukuwa huru na haki, naweza sema nikwlei....
MTAZAMO WANGU MIMI : kurudia uchaguzi sio jambo sahihi. NA KAMA TUNAAMUA KURUDIA UCHAGUZI, BASI TURUDIE TANZANIA NZIMA, NA SI KIPANDE KIMOJA TU CHA ZANZIBAR. Ninaamini, sehemu zilizo zidi kura kuliko wapiga kura, zipo kura za wagombea wa uraisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania. Na kwakuwa Zanzibar ni kipande kimoja wapo cha Tanzania, sioni sababu kwa nusu ya Tanzana irudie uchaguzi halafu Nusu nyingine isirudie uchaguzi.. hii ni Jamuhuru ya Muungano ya Tanzania, sote ni watanzania, sote tunachagua Raisi wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania.
GHARAMA ZA UCHAGUZI
Tunafikiria gharama za kuwalipa mawakala, kuchapisha ballot papers, kuwalipa wasimamizi, na pia vifaa vingine vya stationaries, gharama za mafuta na magari kusafirisha vifaa hivyo katka vituo mbalimbali, na kurudisha sehemu ya kuhesabia na gharama za ulinzi, nani atazicover. Je ni uzembe wa nani aliye sababsha kura feki ziingie kwenye asanduku ya kura? Hao wazembe watachukuliwa hatua gani?
Musichukulie hili suala kiwepesi sana lakini Watanzania tuawaaminisha vipi kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki na sio kujaribu kukwanyua haki ya chama Fulani kilicho shinda?
Napenda kuwaomba Watanzania kuwa na moyo wa subira, wavumilivu, lakini ikitokea idadi ya wapiga kura ikapungua zaidi tume ishangae, kwani watanzania wamekuwa waoga kwa vitisho vilivyo fanywa kipindi hiki kifupi cha kuchagua viongozi wao.