Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Wakuu.

Kwa niaba ya wapenda demokrasia namuomba mwanasheria msomi Tundu Lissu na Kibatala Peter wajitokeze kutoa ufafanuzi wa uhai wa kura za muungano baada ya ZEC kufuta uchaguzi visiwani
 
Kama wamesema Zanzibar uchaguzi haukuwa huru na haki,na.watu waliopiga kura kwa wawakilishi na rais wa zanzibar ndio haohao na katika vutuo hivyohivyo basi hata kura za mgombea urais wa jamuhuri na za.wabunge hazikuendeshwa kwa njia ya uhuru na haki.
 
Na pia swala la theluthi ya kura za zanzibar kwa mgombea uraisi
 
Haiwezi kushinda au haiwezi kutangazwa mshindi?
 
Hapa tukubali tuna mgogoro wa kikatiba. Tukae chini tuteue rais wa mpito tuandae katiba mpya na tume mpya ndio twende kwenye uchaguzi. Hii demokrasia ya kushinda ccm haitatupeleka popote.
 
Kila siku nalia humu kuhusu tume uhuru.

Kwamba, hizi tume zinazoundwa na CCM kamwe haziwezi kumtangaza mgombea asiye wa CCM kuwa ndo mshindi.

Na haya ya leo ndo ushahidi wenyewe sasa.

The Boss where ya at?
 
Last edited by a moderator:
Wanajua matokeo ya bara yatawa influence wapiga kura Zanzibar. Na vile vile inategemea uchaguzi utarudiwa lini, Kama ni baada ya Magufuli kuanza kazi anaweza kuanza kwa moto ika influence wapiga kura wa Zanzibar pia.

mkuu unawajua vizuri wazanzibar au unawasikia? wazanzibar hawawezi kuwa INFLUENCED na kitu chochote hata kama uchaguzi ukifanyika mwaka mmoja kuanzia sasa. chezea wazanzibar wewe!

hiyo "infuence" unayosema inawezekana huko bara tu lakini sio hapa zanzibar.
 
Nyie futeni ya kwenu, tupeni kura za rais wa jamhuri ya muungano tufunge kazi. Sisi huku mshindi anakaribia kupatikana
 
Sasa Kama Mchakato Wa Uchaguzi Wa Zenji Ni Batili, Sasa KURA Za Urais Wa Muungano Zinakuwaje!!?? Ni Halali Au Batili!!!!??? Kisheria Ikoje Hiyo!!!!?
 
Napenda kuelemishwa Ndugu zangu. Je kufutwa kwa kura za Urais Tanzania Bara kunaweza kuathiri matokeo ya kura ya Urais Tanzania Bara?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…