Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Elections 2015 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yafuta Matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu

Kagame aliliona hili mapema akawa anasubiri tu litimie, kweli kuhubiri demokrasia si kutenda demokrasia, ccm aibu hii mtapeleka wapi?
 
Habari wanajamvi
Taarifa kutoka Zanzibar ni kuwa Tume ya Uchaguzi (ZEC)Visiwani humo imefuta matokeo ya Urais.



source TBC1
 
lubuva na ccm yake wanataka kuingiza nchi katika machafuko yasiyo ya lazima, sasa huyo rasi ya jmt atapatikanaje bila kura za zanzibar lakini?? Matokeo yote zanzibar yamefutwa including yakina magufuli na lowasa sasa, huyo lubuva halijui hili..... Huyu mzee asilete utani na maisha ya watu
 
Tanzania tuifanye nchi ya amani jamani!

Mbona mwkt hajafuta pia tanganyika ambako baadhi sehemu kuligubikwa na kasoro nyingi?
 
Nadhani hukunielewa, nimesema maeneo kama Arusha hawakupiga Ubunge, wamepiga ya Raisi na Ubunge utapigwa baadaye. Ni sawa na Zanzibar watarudia ya Raisi wao tu, sio Raisi wa MUungano.

Mkuu wewe ndo hautaki kuelewa. ZEC wamesema uchaguzi Zanzibar ulikuwa na kasoro nyingi sana. Inamaana hizo kasoro pia zime affect kura za rais wa Muungano. ZEC wangeweka wazi kuwa KURA zenye kasoro ni za RAIS wa Zanzibar tu hapo ingekuwa wazi.


Nimekuomba kwa tanzania bara nitajie Jimbo lipi halijapiga KURA za RAIS? PIA JE

 
Last edited by a moderator:
Hivi akisema "kutofahamiana kwa wajumbe wa tume" ana maana wajumbe wa tume hawakukubaliana na hivyo kupelekea kupigana? Hapa anakiri jitihada kubwa za kuchakachua zilifanyika ila baadhi ya wajumbe wa tume wakakomaa. Hili linadhihirishwa pia na ukweli kwamba wajumbe wa tume waliweka itikadi zao za kisiasa mbele kama alivyoeleza. Kwa kuwa Tume ya Uchaguzi si halali na huru, uchaguzi utakaosimamiwa na tume hiyo hauwezi kuwa halali, huru na wa haki.

Na haya aliyoeleza Mwenyekiti wa ZEC ni mapungufu ya NEC pia. Wakati ZEC ina wawakilishi wa CUF pia,NEC inaundwa na makada wa CCM pekee. Kwa hivyo, hali ni mbaya zaidi kwa upande wa Tanzania bara.

Kuweka record sawa, ZEC imefuta uchaguzi uliofanyika Jumapili na matokeo yake yote. Si matokeo ya urais tu kama mleta taarifa JamiiForums alivyoeleza.
 
NEC ni tume ya uchaguzi inayosimamia uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa Serikali ya Muungano wakati ZEC ni tume ya uchaguzi wa Zanzibar inayosimamia uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Raisi wa Zanzibar na wajumbe wa baraza la wawakilishi.

ZEC haisimamii uchaguzi wa Raisi wa muungano wala wa wabunge wa muungano.Hivyo uchaguzi wa Raisi wa muungano na wabunge wa muungano uliofanyika zanzibar kwangu mimi nauona ulifanyika vizuri chini ya usimamizi wa Jaji Lubuva.Zoezi la kutangaza matokeo liendelee.Ya ZEC wabaki nayo ZEC wenyewe
 
Ndugu zangu watanzania, nawasalimu!

Najitokeza hapa kutoa mawazo, maoni uelewa na uchambuzi wangu wa kisheria na kiuhalisia juu ya Tamko la ZEC kufuta uchaguzi wa Zanzibar. Natumai watanzania wengi wameshaona au kusikia kauli hiyo ya ZEC iliyotolewa na Mwenyekiti wake Mh. Jecha. Nitakwenda taratibu ili ukianza mjadala uwe umenyooka na wenye mashiko.

Kwanza kabisa nikiri kutokuona kifungu chochote cha Sheria kinachompa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kutoa tamko/taarifa aliyoitoa kuhusu kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Ingawa ni kwa haraka, nimepitia the Zanzibar Electoral Commission Act, 1992 (inayoanzisha na kuipa kazi ZEC) na the Election Act No. 11 of 1984 (inayoratibu chaguzi za Zanzibar) lakini sikuiona mamlaka ya Mwenyekiti wa ZEC ya kufuta uchaguzi mzima.

Sheria ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (the Zanzibar Electoral Commission Act, 1992),chini ya kifungu cha 5, inaipa ZEC kazi ya kuratibu na kusimamia chaguzi za Urais,Uwakilishi na chaguzi za Serikali za Mitaa,pamoja na mambo mengine. Ndiyo kusema, ZEC husimamia chaguzi za ndani ya Zanzibar za ngazi tajwa. Ndiyo NEC ya kule Zanzibar. Naamini kwamba hata kwa Urais wa Muungano, ZEC husimamia uchaguzi huo kwa niaba ya NEC.

Nasisitiza kuwa ZEC, kwakuwa sikuona, haina mamlaka ya kufuta uchaguzi. Ingeweza kuahirisha upigaji kura na kadhalika kama kungekuwa na hali ya sintofahamu kama inavyotakiwa na kifungu cha 74 cha Sheria ya Uchaguzi Nambari 11 ya 1984 (the Election Act No. 11 of 1984). Sasa ZEC imeshafuta uchaguzi mzima wa Zanzibar. Nini madhara yake kwa uchaguzi huu wa Tanzania hasa kwa ngazi ya Urais na Ubunge?

Inafahamika kuwa Wazanzibari walishiriki pamoja nasi kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiuhalisia, kila mpigakura Mzanzibari,siku ya kupiga kura, alipiga kura za aina nne: Rais wa JMT, Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Wabunge.

Ni kura ile ile ya mpiga kura yule yule iliyohesabiwa sehemu zote nne. Kura hii ikiwa halali sehemu moja, itakuwa halali sehemu zote na kinyume chake kitakuwa sahihi, yaani, ikiwa batili sehemu moja ni batili sehemu zote. Hii ni kwakuwa idadi ya wapiga kura wa nafasi zote nne ni ile ile;vituo ni vile vile na hata wasimamizi ni wale wale.

Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, katika uhalisia na sheria, ni kufuta kura zote zilizopigwa huko Zanzibar. Hata zilizotumwa kwa NEC kwa ajili ya Urais na Ubunge wa JMT zimekuwa batili.

Kwahiyo, kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hazitatimia kwakuwa zile za Zanzibar zinapaswa kuondolewa kwakuwa zimetamkwa kuwa si kura halali. Hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitaanza na kutimia bila Wabunge wa Zanzibar kwakuwa kura za Wabunge wa kutoka Zanzibar zinapaswa kurudiwa.

Ndiyo maana nasema kuwa ZEC, kwa tamko/taarifa ao ya leo, wanakwamisha hata uchaguzi wa Urais na Ubunge wa Tanzania nzima kwakuwa bila ya kura na Wabunge wa Zanzibar, hakutaundika hata Serikali wala kupatikana Rais wa Muungano. Niko tayari kufahamishwa vinginevyo.


 
Sheria ya kufuta uchaguzi na muda was kurudia katiba inasemaje?

Je waangalizi wa kimataifa kwakua wao ndio watoaji wa pesa zote zinazofanyia uchaguzi sheria zao zikoje?

Sheria ya Tume MTU akijitangaza haisemi kuwa uchaguzi urudiwe Bali kuna adhabu zake ambazo zimeainishwa.

1. Tume ndio ina mamlaka ya kutangaza tarehe ya lini uchaguzi unarudiwa.

2. Waangalizi wa kimataifa hawapo hapa kutoa muongozo wa nini cha kufanya ila wapo kuangalia iwapo uchaguzi umefuata taratibu na wanashauri tu na kuondoka ili ushauri huo utumike kwa ajili ya uboreshaji wa uchaguzi utakaofuata - kwa sisi ni 2020. That wasimamizi hawajafika kwa sababu eti walitoa fedha za uchaguzi!


3. Tume ndio yenye mamlaka ya kutangaza matokea, mafala na malofa ndio wanafanya huo ujinga, naamini kuna taratibu za ku deal nao.
 
Nec watasemaje kura za zanzibar ni halali wakati waliosimamia ni zec wanasema sio halali. Hii habari ya mamlaka mbili ndani ya nchi moja inatuchanganya. Uchaguzi wote ufutwe. Achaguliwe rais wa mpito tuandae katiba mpya ndio tufanye uchaguzi mwingine.
 
Kama matokeo yamefutwa, Je na kura zilizopigwa kwajili ya rais wa JMT nazo matokeo yake yamefutwa au ?.. naomba ufafanuzi kwa anaeelewa
 
Hapa wote naona mnabwabwaja tu, kura za raisi wa jamhuri wa muungano zilipigwa siku hio hio mmoja na za raisi wa zanzibar, same place. Sasa iweje za muungano ziwe sahihi na za zanzibar ziwe na kasoro ihali zilipigwa same place. Maana NEC walianza majimbo ya huko zanzibar kukutangazia matokeo ya raisi wa jamhuri wa muungano. Hvyo kwa dosari hzo, NEC hawatoweza mtangaza raisi bila uchaguzi kule kurudiwa. Lasivyo raisi hatakuwa wa muungano, bali ni wa bara tu
 
Back
Top Bottom