Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 22, 2026, imekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete.
Mkutano kati ya tume na Waziri Ridhiwani Kikwete umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo kwenye Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mkoani Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, tume imejadili masuala mbalimbali ikiwemo chanzo cha matukio ya uvunjifu wa amani, athari zake kwa wananchi, mali na miundombinu, pamoja na mapendekezo ya namna ya kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo.
Soma pia: Tume ya Jaji Chande yakutana na Jaji Warioba kujadili matukio ya Uchaguzi wa 2025
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, inaendelea kukutana na makundi tofauti, yakiwemo ya waathirika wa matukio hayo kwa lengo la kukusanya taarifa 6zitakazowasilishwa kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua zaidi.
Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025