PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
MADAI YA KUWEPO KWA MAKABURI YA HALAIKI

“Kulikuwepo na madai kupitia vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la makaburi ya Kondo, Kunduchi, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam. Tume ilifanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kutembelea na kukagua eneo lote la makaburi, kufanya mahojiano na kupata taarifa ya Afisa Msimamizi wa makaburi katika Manispaa ya Kinondoni na kuchukua ushahidi wa msimamizi wa makaburi ya Kondo.”
 
"Tume pia ilifanya ukaguzi na kubaini
kuwa eneo la makaburi ya Kondo linazungukwa na makazi ya watu, na ambalo bado linatumika kwa shughuli za kilimo cha msimu na lina ulinzi muda wote. Kutokana na ushahidi na uchunguzi wa Tume wa uwandani, na kwa kuzingatia hali iliyoonekana katika eneo la Makaburi ya Kondo pamoja na taarifa za Wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi, Tume imebaini kuwa, madai ya kuwepo kwa makaburi ya halaiki eneo la Kondo hayana ukweli."
 
jaji chande ni miongoni mwa hazina ya kipekee sana Tanzania
 
Vilevile, Tume iliwashirikisha wataalamu mbalimbali ili kufanya uchunguzi wa kisayansi kuhusu madai hayo ikiwa ni pamoja na picha ya satelaiti iliyotumika. Maoni ya wataalam hao, wakiwemo wa uchambuzi wa mbali na mifumo ya Taarifa za Kijiografia (Remote
Sensing and Geographic Information Systems) ni kuwa madai haya hayakuweza kuthibitishwa.
 
jaji chande kapiga kwenye mshono wa wazushi
 
Kama policcm wanatakiwa tu kupewa notisi, mbona huwa wanazuia maandamano, mikutano, mikusanyika pamoja na kukamata, kupiga, kujeruhi kupoteza na kuuwa washiriki??
 
Kwa kiasi chake kwa uelewa wangu mdogo nashukuru na kuipongeza serikali kwa hatua hiii ya kujibu na kutoa hofu kwa mtu kama mimi!
 
Baadhi ya wagombea waliokatwa kwenye vyama vyao walichochea chini chini machafuko: Jaji Chande
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…