PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ukomo huo wa maigizo unafikikaje mwisho Kwa aina ya mfumo uliopo serikalini?
Ni wakati wa waTanzania kuchukuwa hatua.
Taifa hili haliwezi kuendelea kunajisiwa kiasi hiki na watu wa aina hii.
Ni lazima tuseme sasa basi, inatosha.
Yeye ndio alichoma vituo mwa mwendokasi na ofisi cha chama ,limtu lipo Marekani kwa shemeji yake linapost ujinga ujinga tu hapa

USSR
Hivi unapoandika namna hii kweli akili zako huwa zimekaa sawa, au hupoteza ufahamu kwa muda kama mtu mwenye kifafa?
 
Sitashagaa endapo hiyo tume itaupa umuhimu zaidi upotevu wa mali kuliko mauaji waliyoyafanya.

Watawaeleza nini waTanzania kwa nini kuzuia uharibifu wa hizo mali njia sahihi iwe ni kuua watu na siyo kutumia njia zinazofahamika kwenye maswala kama hayo.

Waandamanaji walitishia maisha ya mtu yeyote hadi ilazimu kuua?

Watawaeleza waTanzania waliouliwa wote walikuwa kwenye kazi hiyo ya kuharibu mali; hakuna waliouliwa nje ya makundi hayo ya uharibifu?
 
Waliua hadi watoto waliokuwa wanaangalia mpira huko Mwanza.

Waliua watoto kwenye sehemu zingine nchini.

Sijawahi kuona uovu wenye ushahidi usiopingika kama hayo mauaji waliyoyafanya.

Hii kesi ICC wakiichukua ni ushindi mapema sana.
 
SEHEMU YA MPITO: SAUTI JUU YA TAIFA NA FUMBO LA KUPONYWA

Kabla ya kufunguka kwa hatua inayofuata, kulikuwa na jambo zito lililonijia—si kwa kelele, bali kwa uzito wa ndani usioepukika.

Maono haya hayakuwa ya mtu mmoja, wala ya mahali pa siri pekee. Yalikuwa juu ya taifa.

Nikaona juu ya Tanzania, kana kwamba anga limebeba kumbukumbu ambayo haijasemwa wazi kwa vinywa vya wengi, lakini imeandikwa katika kilio kisicho na sauti.

Kulikuwa na rejea ya tukio—tarehe iliyopita, lakini isiyoisha ndani ya roho za walioguswa nayo.
29/10/25.

Siku ambayo ardhi ilibeba damu, na ukimya ukafunika ukweli wake.

Lakini katika maono, siku hiyo haikuonekana kama mwisho—bali kama mbegu.

Mbegu ya kilio.

Imeandikwa:

“Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.” (Mwanzo 4:10)

Na hapo ndipo nilipoanza kuona kwamba si kila tukio linaishia pale linapotokea. Mengine huanza kufanya kazi chini kwa chini, hadi wakati wa kujibu unapofika.

Katika picha iliyoonyeshwa, taifa lilionekana kama mjusi aliyekatika mkia—si kwa kushindwa, bali kwa kujilinda.

Sehemu inakatika ili mwili uendelee kuishi.

Lakini kilichokatika hakifi mara moja—kinatetemeka, kikitoa ishara kwa wanaotazama kwa makini.

Hivyo ndivyo ilivyoonekana.

Jaribio la kujitoa, kujisitiri, kujiponya kwa njia ya muda mfupi.

Lakini ndani yake kulikuwa na jambo jingine likianza.

Sio kwa kelele.

Sio kwa matangazo.

Bali kwa wale wanaoitwa ndani kwa ndani—wale wanaobeba mzigo wa taifa bila kutambulika.

Na hapo nikaonyeshwa muda:

Asubuhi.

Saa kumi na mbili kamili.

Mwanzo wa mwanga, lakini si mchana kamili.

Wakati ambao wachache huamka, na wengi bado wamelala.

Ndipo nilipoona kitu kikianza.

Sauti zisizo na vipaza sauti.

Maombi yasiyoandikwa.

Mioyo inayobeba mzigo bila kuonekana.

Na hapo ndipo neno lilikuja:

“Nimeyasikia.”

Kwa maana imeandikwa:

“Nimeona mateso ya watu wangu… nami nimesikia kilio chao… kwa maana nayajua maumivu yao.” (Kutoka 3:7)

Lakini pia:

“Kama watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba… ndipo nitasikia kutoka mbinguni, na kuisamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” (2 Mambo ya Nyakati 7:14)

Hapa ndipo fumbo linakuwa gumu zaidi.

Kwa sababu si kila kilio huleta mabadiliko.

Lakini kuna kilio kinachofika.

Na kilichoonyeshwa si mwisho wa jambo, bali mwanzo wa mchakato.

Sio uponyaji wa ghafla.

Bali kazi ya polepole—kama mvua ya kwanza kabla ya mavuno.

Taifa halikuonyeshwa likianguka.

Lilionyeshwa likipitia.

Na kati ya kupita huko, kulikuwa na mgawanyiko wa wale wanaoona na wasioona.

Wapo watakaosema: hakuna kilichotokea.

Na wapo watakaojua: kitu kimeanza.

Kwa maana imeandikwa:

“Bwana hatatenda neno lo lote, asipowafunulia watumishi wake manabii siri yake.” (Amosi 3:7)

Lakini siri haifunuliwi kwa kelele.

Hufunuliwa kwa wale wanaosikiliza kati ya mistari.

Hivyo basi, si kila mtu ataelewa mwanzo huu.

Lakini wale walioonyeshwa, watajua kuwa:

Kilio kimefika.

Na kazi imeanza.

Polepole.

Kwa utaratibu usiotambulika kirahisi.

Mpaka pale ambapo matokeo yake yatakuwa wazi kuliko mwanzo wake.

Nitaendelea…

Karibu kwenye uzi huu wangu

Upumbavu mtupu hela iliyotumika ingeenda hata kujenga nyumba za walimu vijijini imetumika kulipa tume ambayo majibu tayari walikua nayo...Yaan jambazi linajiundia tume lijichunguze km liliiba na kuna wapuuzi eti wanaamini kabisa tume dah....???
 
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?
Mimi naamini haki ipo kwa Muumba siku ya hesabu, maana mdomo utazuiwa kusema, yatayosema ni macho, miguu, mikono, masikio na mdomo utasema pale utapotakiwa kusema, hapa duniani kila mmoja anapigania tumbo lake- MAONI YANGU HAYA
 
Muda ni saa ngapi nataka leo kwa mara yangu ya kwanza toka uchafuzi mkuu wa October 29 2025 kufanyika niwashe tv niangalie ingawa najua na huu ni uchungutu huru
 
Ikifika mahala mwenyekiti wa tume akitaja neno HADIDU ZA REJEA

zima tv ukafanye issues zingine.

Kwa lugha rahisi hadidu za REJEA ziliwataka wakachunguze chanzo na sababu zilizopelekea na sio nani alipewa AK47 na order ilitoka kwa nani ili aue watoto wa kitanganyika waliiokuwa wanaenda mashineni kusaga mahindi na wengine kufuatwa majumbani .
Umemaliza Mkuu, wewe ndio umeiweka vzr, kifupi hao walienda kuchunguza fujo na wafanya fujo
 
Waliua hadi watoto waliokuwa wanaangalia mpira huko Mwanza.

Waliua watoto kwenye sehemu zingine nchini.

Sijawahi kuona uovu wenye ushahidi usiopingika kama hayo mauaji waliyoyafanya.

Hii kesi ICC wakiichukua ni ushindi mapema sana.
Hao ICC naona wako kimya sana, wanatuvizia au wametutupa ? Ndio tumaini pekee naliona
 
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?
well done
 
Tukumbushane mauaji aliyoyasimamia Samia.

IMG_8710.jpeg
IMG_8639.jpeg
IMG_8626.jpeg
IMG_8622.jpeg
IMG_8616.png
 
Hao ICC naona wako kimya sana, wanatuvizia au wametutupa ? Ndio tumaini pekee naliona
Nadhani wanatoa kwanza nafasi kwa vyombo vya ndani kuona kama vinaweza kulishughulikia hilo suala.

Ila binafsi sioni ni kwa namna gani ICC haitofungua mashitaka kwa sababu ushahidi upo mwingi sana na vyombo vya ndani havina kabisa credibility.

Kwa kuanza tu na tume ya Chande, tayari hapo unaona kabisa hakuna u seriousness wowote ule.
 
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?
Tunaisubiria kwa hamu ilete majibu ya
  1. Nani alitoa amri ya shoot to kill?
  2. Idadi ya vifo walikufa watu wangapi?
  3. Walizikwa wapi?
  4. Chanzo ni nini?‽
  5. Uwajibikaji
P
 
Back
Top Bottom