PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ni saa ngapi time inawasilisha ripoti yake..?
 
Tunaisubiria kwa hamu ilete majibu ya
  1. Nani alitoa amri ya shoot to kill?
  2. Idadi ya vifo walikufa watu wangapi?
  3. Walizikwa wapi?
  4. Chanzo ni nini?‽
  5. Uwajibikaji
P
Hiyo ya no 1 na 4 huwezi kuiona kwenye hiyo report trust me
 
Naona kuna kila dalili chama kile kilichopokea pesa za kufanya vurugu kipigwe chini daima

USSR
Mwizi na mwuaji atalindwa.ametoa oda kill and shoot haikutosha akatetea yaliyoyotokea na pemba iliwahi tokea as if ni kisasi analipa.
 
Nadhani wanatoa kwanza nafasi kwa vyombo vya ndani kuona kama vinaweza kulishughulikia hilo suala.

Ila binafsi sioni ni kwa namna gani ICC haitofungua mashitaka kwa sababu ushahidi upo mwingi sana na vyombo vya ndani havina kabisa credibility.

Kwa kuanza tu na tume ya Chande, tayari hapo unaona kabisa hakuna u seriousness wowote ule.
Binafsi nawasubiri wao,hawa akina chande Sina Iman nao
 
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?
Ukiangalia tu majina ya members wanaoiunda hiyo tume unagundua some of them ni wahusika wanaotakiwa kuchunguzwa, this is totally nonsense ever happened.
 
1776929969389.png


Ndiyo ni FUTUHI.
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel:
Ikulu Tanzania na Tovuti: ikulu.go.tz
#TanzaniaYetuSote
#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
 

Attachments

  • 20260423_101752.jpg
    20260423_101752.jpg
    135 KB · Views: 21
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?
Uzuri leo haina saa ni mwendo wa kuviziana.
 
Inaitwa tume huru kufanya matukio yaliyotokea baada ya Uchaguzi 2025, wakati huo amiri jeshi Mkuu ndiye anayenyooshewa kidole kuwa mshiriki namba moja wa kilichotokea.

Huyo anayenyooshewa kidole,ndiye aliye;

Amewalipa posho
Amewapa magari
Amewajazia mafuta
Amewapa Ulinzi n.k

Alafu tutegemee majibu ya tofauti??

Tuweni wakweli, Huwezi kuukata mkono unaokulisha
 
Back
Top Bottom