PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

PostGE2025 Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya Oktoba 29 yawasilisha ripoti leo Aprili 23, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
View attachment 3577613
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande​
Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, (Maarufu tume ya Jaji Chande) inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake rasmi leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 kwa Rais Samia Suluhu.

Siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025 kuliripotiwa kutokea kwa maandamano, vurugu na taharuki na siku chache baadaye, taarifa za vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu wa mali zilianza kuripotiwa mitandaoni.

Tume hiyo ilianza kazi zake Novemba 20, 2025 ikiwa na lengo la kukamilisha majukumu ndani ya siku 90. Hata hivyo, muda wake uliongezwa hadi Aprili 3, 2026 kabla ya kuomba nyongeza nyingine, na hatimaye ripoti hiyo kuwasilishwa leo.

Inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, tume hiyo pia inaundwa na wajumbe saba ambao ni Profesa Ibrahim Juma, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Luteni Jenerali Paul Meela, Said Mwema, Balozi David Kapya, pamoja na Dkt. Stergomena Tax.

Rais Samia aliunda tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32).

Wewe unatarajia ripoti hii ilete majibu au mwelekeo gani?


Nina imani hii tume haina majibu ya kweli maana so kwa kujihami huku... mtaani polisi kila kona
 
Jaji Chande ni nguli kweli kweli kwenye mambo haya!..

🚨Tuna imani kubwa sana kuwa ripoti hii itaeleza ukweli wa nani alikuwa nyuma ya vurugu za 29 Oktoba 2025

🚨Kwa uzoefu huu wa Jaji Chande hatukuhitaji wazungu kuja kuchunguza mambo ya 29 Oktoba 2025

#UkweliOktoba29View attachment 3577756
Sio na ukweli, sema na uwongo unaotakiwa na serekali ya majizi.
 
Nadhani wanatoa kwanza nafasi kwa vyombo vya ndani kuona kama vinaweza kulishughulikia hilo suala.

Ila binafsi sioni ni kwa namna gani ICC haitofungua mashitaka kwa sababu ushahidi upo mwingi sana na vyombo vya ndani havina kabisa credibility.

Kwa kuanza tu na tume ya Chande, tayari hapo unaona kabisa hakuna u seriousness wowote ule.

Msipende kuyategemea hayo ma ICC, walifanya nn mauaji ya Rwanda, Kenya, Palestine, libya and the like.
 
Back
Top Bottom