MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
MOSI,Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, almaarufu kama The International Criminal Court (ICC) imeanzishwa na MKATABA WA ROMA (THE ROME STATUTE), na huwa inafanya kazi chini ya kanuni iitwayo The Complementarity Principle.
Kanuni hii (The Complentarity Principle) imetajwa kwenye aya ya kumi ya dibaji (Preamble) na Ibara ya 1 ya MKATABA WA ROMA, na inasema kwamba mahakama ya ICC siyo mbadala wa mahakama za ndani. Hivyo jukumu la kwanza kabisa la kufanya uchunguzi dhidi ya uhalifu na kuwaadhibu wahalifu ni la mamlaka za ndani ya nchi ya nchi.
ICC huwa inakuja tu pale ambapo mamlaka za nchi zimefeli kuchunguza, kuwakamata na kuwaadhibu wahalifu, aidha kwa maksudi au kukosa uwezo. Kitaalamu tunasema "When the state authorities are UNWILLING or UNABLE to prosecute". Mazingira haya yakitokea basi fahamu fika kwamba kesi lazima ifike kule ICC, the Hague.
PILI, kilichotokea nchini Tanzania, hasa Tanganyika kuanzia tarehe 29th Oktoba 2025 mpaka kufika sasa ni mauaji makubwa mno, yaliyoendeshwa kitaalamu, kwa maksudi, kupitia vyombo vya usalama, ambavyo vilikuwa vinatekeleza amri kutoka juu. Tunafahamuje kwamba ni amri kutoka juu ???
Taasisi zote za kiusalama nchini Tanzania, kupitia KATIBA (CURT 1977), Sheria ya Idara ya Usalama (TISS Act 2023), Sheria ya Jeshi la Polisi (Police and Auxiliary Act 2023), Sheria ya Ulinzi (The National Defense Act 2023) na Sheria ya Usalama (The National Security), zote zinaonesha kwamba Amiri Jeshi Mkuu (Commander In Chief) wa vikosi na majeshi yote ya usalama ni RAISI.
Majeshi hayawezi kutoka kwa wingi vile wakiwa wameshika silaha bila kupewa amri na RAISI. Hata mauaji waliyoyafanya yametekelezwa na kuwezeshwa na rasilimali za Taifa ambazo serikali ndiyo inazishikilia. Silaha, Magari, Mahitaji (mafuta, mabomu na risasi) na miuondombinu (Internet Network) iliyotumika kuviunganisha vikosi Tanzania nzima ilitolewa na serikali.
Chini ya sheria za jina za kimataifa, kuna kanuni tunaita COMMAND RESPONSIBILITY, ambayo inasema dhahiri kwamba AFISA atawajibika kwa makosa ya vikosi vilivyo chini yake. Hapa aidha kwa kutoa amri zilizowataka kuvunja sheria, haki za binadamu au uharibifu mali wakati wa oparesheni, AU kuona vikosi vyake vinapanga kuvunja sheria, haki za binadamu na uharibifu wa mali lakini hachukui hatua yoyote kuvizuia.
Tukifuata mlolongo huu, basi wahusika wa mauaji ya watanganyika ni maafisa wa KISIASA na KIJESHI ambao wako kwenye mlolongo wa kuongoza vikosi hivi. Hapa tutaanza kabisa na hawa wafuatao, ambao aidha wako kwenye amri za moja kwa moja au ni wanachama wa kamati za ulinzi na usalama :
1. Officers in charge of station (Police Force)
2. Regional Police Commissioners (Police Force)
3. District Security Officers (TISS)
4. Regional Security Officers (TISS)
5. District Commissioners (Central Government)
6. Regional Commissioners (Central Government)
7. Minister of Home Affairs (Central Government)
8. Minister of Defence (Central Government)
9. Inspector General of Police (Police Force)
10. Director of Operations (TISS)
11. Director of National Intelligence (TISS)
12. Chief of Staff of Armed Forces (TPDF)
13. Head of Special Forces Units (TPDF)
14. Director of Military Intelligence (TPDF)
15. Chief of Defence Forces (TPDF)
16. Members of the National Security Council (Central Government)
17. Security and Political Advisors to the President (Central Government)
18. The President of the United Republic of Tanzania.
Tukizingatia kilichoanza kutokea Ujerumani (Nuremberg Trials 1945-1946), Tokyo (Tokyo Trials 1946), Yugoslavia (ICTY 1993), Rwanda (ICTR 1994) na Sierra Leone (SCSL 2002), ambako yalitokea machafuko na kufanyika mauaji makubwa ya raia basi fahamu fika serikali nzima inaweza kuwekwa kikaangoni na nchi ikaingia kwenye ukurusa wa giza totoro ambalo hatujawahi kutegemea.
Wakati UHURU na RUTTO wanapelekwa ICC kwa vurugu za uchaguzi za mwaka 2007-2008, mauaji yale hayakufanywa na serikali bali watu binafsi (Non-State Actors) ndiyo maana Mzee Kibaki alibaki salama na kumaliza vizuri. Hapa Tanzania hata vyama vya siasa vya kuviangushia mpira au jumba bovu havikushiriki uchaguzi na wanasiasa wao walikuwa wameshikiliwa na vyombo vya dola.
TATU, pia kwenye jinai za kimataifa hasahasa makosa dhidi ya ubinadamu (CRIMES AGAINST HUMANITY), hasahasa kwenye makosa madogo-dogo kama Extermination, Rape, Torture and Deportation, yanapotokea fahamu fika kuna kitu kitaalamu wanaitwa WIDESPREAD & SYSTEMATIC ATTACK. Kwamba its systematic because there is a pattern of conduct as a result of certain Government Policy, And Widespread because that policy has gained traction throughout the nation.
Hapa ni kwamba haya muaji ni tofauti na aina nyingine kwasababu yametendeka kama utekelezwaji wa sera maalumu ya kiserikali, jambo ambalo hufanyika kufuata mlolongo fulani (Systematic Attacks/ Pattern Attacks). Lakini pia haya mambo yanapofanywa na serikali watu wengine ndani ya vyombo vya usalama au vyama vya siasa huanza kuyatenda kwa wingi sehemu nzima ya nchi (Widespread Attacks) wakiamini kwamba wanatekeleza sera ya nchi hata kama haijatangazwa rasmi.
Ndiyo maana ni rahisi mno kukuta Polisi wa kawaida kwenye mkutano anasema wazi kabisa kwamba tutawashughulikia, au tutawapiga kipigo cha mbwa koko. AU Maafisa usalama kote Tanzania nzima wamefanya mauaji na uhalifu wa aina moja. Wamefanya hivi kimkakati (Systematic Attack), chini ya mwamvuli wa serikali wakiamini kwamba vitendo hivyo vitaisaidia serikali (Widespread Attack).
NNE, uhalifu dhidi ya binadamu (CRIMES AGAINST HUMANITY) yanapofanywa na serikali basi fahamu fika kwamba mara nyingi lazima vikao vimekaa na kuna watu ambao walisaidia utekelezwaji wa matendo hayo kufanyika. Hii kanuni kule ICTY na ICTR waliitumia na inaitwa JOINT CRIMINAL ENTERPRISE (JCE). Mauaji ya halaiki (Massacre and Extermination) kama haya hayawezi kufanywa na mtu mmoja tu, yanahitaji watu wengi, utaalamu na rasilimali za kutosha.
Hivyo hapa watu kama JAKAYA MRISHO KIKWETE, ABDALLAH BULEMBO, RAJAB LUHWAVI, ABDUL AMEIR, ROSTAM AZIZ, ANGELLAH KIZIGHA na HAJI OMAR KEIR, hawawezi kujinasua hata kidogo, mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo. Kisheria kwenye JOINT CRIMINAL ENTERPRISE (JCE) tunachoangalia ni UFAHAMU WA TUKIO (The Mental Element), kwamba uko ndani ya taasisi ya kiusalama au kisiasa na ulikuwa unafahamu kwamba kuna mipango michafu inapangwa.
JCE, haishii hapo tu, bali katika ngazi ya taasisi, idara nzima inaweza kuwekwa hatiani kwasababu wafanyakazi wake walichangia uovu kutokea (Made a Singificant Contribution). Baadhi ya kombania za kijeshi (Companies), vikosi (Brigade/Regiment) na vikosi maalumu (Task Forces) zina hatia kwa kusaidia huu udhalimu. Kule Nuremberg mwaka 1945 walienda mbali na kufanya GUILTY BY ASSOCIATION, ambapo majasusi wote kutoka Idara ya The SS walishikiliwa kama watuhumiwa wa mauaji ya watu.
JCE, pia inaweza kuwanasa hata makada na majasusi wanaoeneza propaganda za muaji ya serikali au kuyadogosha huko mitandaoni. Hili linaweza kutokea endapo itathibitika walikuwa na UFAHAMU KWAMBA UOVU UNAENDELEA au unapangwa. Hili linanikumbusha kesi ya Mwanahabari wa Rwanda aitwaye HASSAN NGENZE, ambaye hali akifahamu mipango ya uuaji, na mauaji yanaendelea dhidi ya Watutsi alikuwa kinara wa kutumia magazeti yake kuchochea. Alishitakiwa na ICTR kule Arusha.
NB: Lengo zima la kuwepo kwa THE COMPLEMENTARITY PRINCIPLE kwenye MKATABA WA ROMA, ni kuhakikisha kwamba nchi inatunza uhuru wake (Sovereignty) huku inaendelea kushughulikia makosa ya kimataifa na kutoa haki kwa wahanga. Haya ni maneno ya Proffessor Sarah H.M Nouwen.
Hivyo kitendo cha SAMIA kuifikisha nchi hapa ni dhahiri anahatarisha uhuru wa nchi na usalama wake. Kesi ikifika ICC ni dhahiri nchi itakuwa uchi wa mnyama. Taasisi zote zitachunguzwa, silaha zenu, nakala za siri na mtashurutishwa kutoa ushirikiano, jambo ambalo litaleta dhihaka kwa taifa. Yote haya kisa tamaa za kikundi cha watu wachache ambao wameamua kuumiza nchi nzima kujipanya wao na familia zao.
=================================================================Kanuni hii (The Complentarity Principle) imetajwa kwenye aya ya kumi ya dibaji (Preamble) na Ibara ya 1 ya MKATABA WA ROMA, na inasema kwamba mahakama ya ICC siyo mbadala wa mahakama za ndani. Hivyo jukumu la kwanza kabisa la kufanya uchunguzi dhidi ya uhalifu na kuwaadhibu wahalifu ni la mamlaka za ndani ya nchi ya nchi.