Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC) imesema imepokea malalamiko kutoka kwa wadau wa mpira wakiitaka kuchunguza udhamini uliofanywa na kampuni ya GSM kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania kama hautaathiri ushindani wa soka nchini.
Wadau hao wamewasilisha malalamiko yao kwa maandishi ndani ya tume hiyo Jumatatu ya Novemba 29, 2021 wiki hii kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa FCC, William Erio wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Malalamiko hayo yamepokelewa ikiwa ni siku chache tangu kampuni ya GSM kusaini mkataba wa Sh2.1 bilioni na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF).
Pia hilo limefanyika ikiwa ni muda mchache tangu kampuni hiyo ambayo ni mdhamini wa Yanga SC kutangaza kuzidhamini timu za Pamba na Coastal Union ya jijini Tanga.
“Tulishaanza mchakato wakutaka kujua kama kitendo hicho hakitaathiri ushindani katika soka na majibu ya suala hili yatatolewa baada ya kujiridhisha kwa kuzingatia kanuni za ushindani na kama kweli linahusiana na ushindani,” alisema Erio.
Mwananchi