KERO Tume ya Utumishi wa Mahakama mnapochelewesha matokeo ya usaili mnatutesa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Vijana wameenda kwenye Mahakama za Kanda wamefanya usaili, wengine wamesafiri kwa kutoa nauli zaidi ya shilingi elfu 30 kwenda tu. Kuna wengine walifikia lodge na wengine kwa ndugu. Baada ya usaili wamesubiri mtoe matokeo wajijue wanaoendelea na usaili na wale wasioendelea wajijue warudi makwao kwa amani ya bwana.

Sasa mtu nipo hapa Mahakama ya Kanda Mbeya nikisema ninarudi kijini kule mkoani kwangu ile ninafika tu mnaniita nije usaili wa awamu ya pili, kwa maana hiyo chukua (elfu 30 x 4) + lodge (elfu 20 x 13 mpaka sasa) manake sijarudi kwetu tangu nije hapa tarehe 18 Agosti.

Ninajiuliza pamoja na kuwa kwenye kada yangu nimepata 17/20 je nisipochaguliwa awamu ya pili hizo fedha zilizopoteza kukaa hapa Mbeya mjini itakuwaje?

Jamani mahakama ni chombo cha kutenda haki, sasa mbona na nyie kama mmeshaanza kututesa sasa!

Semeni jambo jamani!
 
Bado nashauri mchakato wa ajira zote katika utumishi wa Umma uratibiwe na kusimamiwa na Sekretarieti ya AJira
 
Mkuu jitahidi uwe na kitu cha kufanya utakaa kulia lia na hizi ajira za serikali, ukiwa na kazi yako unaenda unafanya alafu unarudi unaendelea na mishe zako! Kwa sababu tangazo lao lilikuwa very clear kuwa usaili ule ulikuwa ni wa kielekronik baada ya hapo mtapangiwa oral au practical hawakusema ni lini watafanya hivyo sasa unawalaumu nini???
 
Ushauri mzuri sana! Tayari nimepanda basi ninarudi kijijini kwetu nikavune!
 
Ukiwa mtafutaji siku zote dhahama zote ni zako. Wahusika hawana hata haraka, wamesahau hizo ni ofisi za umma ipo siku watastaafu na kuja kuishi na sisi mtaani.
 
Sizan kama bado zipo hiz ,usishangae walishaita watu kwenye oral interview zamani..
 
Ukiwa mtafutaji siku zote dhahama zote ni zako. Wahusika hawana hata haraka, wamesahau hizo ni ofisi za umma ipo siku watastaafu na kuja kuishi na sisi mtaani.
Ipo siku watoto wao pia watatukuta sisi kwenye hizo ofisi, siku ni namba na zinahesabika
 
Ipo siku watoto wao pia watatukuta sisi kwenye hizo ofisi, siku ni namba na zinahesabika
Usahili wa awamu ya kwanza ulihusisha maswali yanayoshabihiana na kada husika ama ni maswali mchanganyiko kwa maana mengine ya uelewa?

Kulikuwa na maswali mangapi jumla na kama unaweza kutupa mfano wa japo maswali mawili mkuu.
 
we ushapita tayari kwa hizo 17 zako Kuna wadau Wana 5/20 ,sema tu jamaa tangu waanzage kufanya hizi saili hawajawahi ita watu wengi kiasi hiki ndo maana wanahangaika kuchakata matokeo ,but tuendelee kuvuta subra
 
Mie ninajivunia maparachichi huku kwetu! Mbeya mjini imenila kama laki 3 na ushe zangu eti kwa ajili ya kuhangaikia kazi ya Uhasibu Mahakamani. Wakiniita awamu hiyo ya pili, ninaweza nisiende kabisa!
 
Huu mchakato usiokuwa na deadline wala timetable unachosha, bora PSRS
 
Sijui sababu ya kuchelewesha nini maana wenzao wa afya written interview wamesahihisha na kutoa walioselected wao mfumo usahisha lakini bado inakera
 
Sijui sababu ya kuchelewesha nini maana wenzao wa afya written interview wamesahihisha na kutoa walioselected wao mfumo usahisha lakini bado inakera
Ndiyo maana mie hata wakiniita nimeamua siendi tena, nishaona mahakama ni mahakama tu, hawana nafuu yeyote - kote inanuka rushwa tu.
 
Jamaa wamechelewa kutoa list ya pili kiasi kwamba sina imani nao tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…