Vijana wameenda kwenye Mahakama za Kanda wamefanya usaili, wengine wamesafiri kwa kutoa nauli zaidi ya shilingi elfu 30 kwenda tu. Kuna wengine walifikia lodge na wengine kwa ndugu. Baada ya usaili wamesubiri mtoe matokeo wajijue wanaoendelea na usaili na wale wasioendelea wajijue warudi makwao kwa amani ya bwana.
Sasa mtu nipo hapa Mahakama ya Kanda Mbeya nikisema ninarudi kijini kule mkoani kwangu ile ninafika tu mnaniita nije usaili wa awamu ya pili, kwa maana hiyo chukua (elfu 30 x 4) + lodge (elfu 20 x 13 mpaka sasa) manake sijarudi kwetu tangu nije hapa tarehe 18 Agosti.
Ninajiuliza pamoja na kuwa kwenye kada yangu nimepata 17/20 je nisipochaguliwa awamu ya pili hizo fedha zilizopoteza kukaa hapa Mbeya mjini itakuwaje?
Jamani mahakama ni chombo cha kutenda haki, sasa mbona na nyie kama mmeshaanza kututesa sasa!
Semeni jambo jamani!