Tume ya Warioba haikufanya LOLOTE

Tume ya Warioba haikufanya LOLOTE

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
735
Reaction score
191
Ndugu wanajamii, mimi naona Jaji Warioba na tume yake wametuchanganya zaidi kuliko kutuongoza.

Kwa kupendekeza tu serikali TATU wameleta balaa kubwa kuliko suruhu.

Kwanza hii katiba yao ni ya hiyo NCHI MPYAA YAANI TANZANIA mpya ambayo bado haijaundwa. Tukumbuke hiyo rasimu ni ya Tanganyika na Zanzibar na mpaka leo hii Tanganyika haipo.

Pili Jaji na tume yake wanatuambia kuwa katiba hii itatumika baada ya kuundwa nchi na katiba ya Tanganyika ambavyo hatuanza hata kuvizungumzia.

Wimbo wa MAJANGA hapa umepata chapter. Hili ni janga maana kimantiki sioni kama haya mambo yatatekelezwa hivi karibuni. SIONI KAMA WALIOBA AMEJIBU ILE KIU YA KATIBA MPYA.
 
Tume imetusaidia kutafsiri maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo.
Huu ni mwanzo tu, bado vikao vingi vinafuata kabla ya kupata katiba mpya.
 
Majanga kabisa inshort rasimu haijashughulikia mambo yanayopelekea hizi shida za sasa, kinga ya rais iko palepale, rais bado ndo anateua watendaji mpk wa vyeo vya chini
 
unadhani ni sahihi kusema haijafanya kitu?
 
Tume imetusaidia kutafsiri maoni ya wananchi na kutoa mapendekezo.
Huu ni mwanzo tu, bado vikao vingi vinafuata kabla ya kupata katiba mpya.

Lakini ukumbuke kitachojadiliwa ni hiki kilicho kwenye rasimu tu. Mara nyingi sana tumeshudia ugumu wa kubadili kipengele hata kimoja tu kwenye misuada ya sheria zetu.

Kwangu sipati picha maana kiu ya katiba ilikuwa kwa Tanganyika ambayo ni kama HAIJAGUSWA!
 
Mwanzo nilisema Tume haikufanya lolote lakini Kwa KWELI imefanya kazi kubwa kwa maana ya FOUNDATION. Kwa waliosoma rasimu utaona kuna mengi yameandaliwa kwa ajili ya Tanganyika. Ni kazi nzuri.
 
Ninachojiuliza katiba ya tanganyika ni lini itakuwa?
 
pamoja na msingi uliowekwa lakini tunahitaji kwanza kujua katiba ya Tanganyika itakuwaje? kwa misingi ya kihistoria ni vema tukatumia jina Tanganiyika kuliko tz bara.
 
Ninachojiuliza katiba ya tanganyika ni lini itakuwa?

Shida ni kuwa haya mambo yanategemeana. Huwezi kujadili Tanganyika mpaka ukubali SERIKALI TATU.

Kwa sasa Magamba wanapata ukakasi kukubali UKWELI. Tuombe Mungu na Tanganyika inarudi.
 
Rasimu ya tanganyika ipo wapi.? Muda umeende kuna miezi kumi na nane kabla ya kuingia mwaka wa uchaguzi na hakuna kitakachofanyika
 
Maoni utoe mwenyewe af usiwlewe mwenyewe, kuna mambo watu hawakuchangia kwa uelewa wao, walishinikizwa na vyama vyao bila kujua madhara yk now ndo wanaona madudu waliyoshauriwa kuyachangia
 
ndugu wanajamii, mimi naona jaji warioba na tume yake wametuchanganya zaidi kuliko kutuongoza.

Kwa kupendekeza tu serikali tatu wameleta balaa kubwa kuliko suruhu.

Kwanza hii katiba yao ni ya hiyo nchi mpyaa yaani tanzania mpya ambayo bado haijaundwa. Tukumbuke hiyo rasimu ni ya tanganyika na zanzibar na mpaka leo hii tanganyika haipo.

Pili jaji na tume yake wanatuambia kuwa katiba hii itatumika baada ya kuundwa nchi na katiba ya tanganyika ambavyo hatuanza hata kuvizungumzia.

Wimbo wa majanga hapa umepata chapter. Hili ni janga maana kimantiki sioni kama haya mambo yatatekelezwa hivi karibuni. Sioni kama walioba amejibu ile kiu ya katiba mpya.
mimi kwangu warioba ameonesha ukomavu na kwamba hawezi kutumiwa kwa maslahi ya chama kandamizi wa demokrsia. Well done warioba. Prof issa shivji anamshambulia warioba kwamba hiyo siyo kazi aliyotumwa. Je yeye ndiye aliyeandaa hadidu za rejea (tor). Hapa naona anawasilisho matamanio ya mawazo yake. Nadhani angekuwa kikwete baada ya kutoka maoni haya angewaweka ndani warioba na wenzake pasipo hatia. Anawezaje kumhukumu warioba huyu ?
 
Back
Top Bottom