Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaji warioba anaakili nyingi sana, kaamua kuwaunga mkono ccm ili baadae alianzishe la serikali 3 je! ccm mtamuunga mkono nakutengua maoni yenu feki ya katiba ya chenge na Samweli Sitta?
Hizo sio akili nyingi,hata akilianzisha hakuna atakayemuelewa
Akili za wabongo ni za kuhama hama sana!!!
Sikutegemea mzee Warioba aliyepigwa na watoto kwa maagizo ya wakubwa wao ambao wamepewa ukuu wa wilaya kwa kumpiga leo anakwenda watetea!!!
Akili za waafrika wengi bado zina vimelea vya utumwa!!!
Na hii ndiyo habari ya mjini UKAWA muda so mrefu watapokea vigogo wengine ndani ya wiki hii(note my words)Warioba kapandishwa jukwaani kuzima aibu ya kutokuwa na waziri mkuu yeyote.Ila kwa vile alivyochanwachanwa na Ma CCM akiwepo Kikwete sidhani kama Warioba akili yake ipo CCM.Huyu atasajiliwa UKAWA muda si mrefu
Kwa hiyo ulikuwa unatakaje au unashauri nini? ?? Funguka kamanda. Lakini kabla ya hapo embu tueleze mbona Chadema wametutapeli kwa kutuaminisha Lowasa ni fisadi la kutupwa, mwishowake wanamshawishi aje achukue fomu ya kugombea urais na kumtupa nje Dr Slaa. Ujinga mtupu. Kweli siasa ni si asa!
Mnategemea utapeli mlioufanya utafanya wananchi watuamini tena. Wanatuona kama wajinga tu, usione watu wanakusanyika wengi kwenye mikutano mkadhani watatupigia kura. Ni ndoto ya mchana. Turudi tukajipange tena. Na ikiwezekana baada tu ya uchaguzi tumfukuze Lowasa na kundi lake na Mbowe wake na Mbatia. Turudi kwenye zama za ukweli za Dr Slaa na Lipumba basi.
Na hii ndiyo habari ya mjini UKAWA muda so mrefu watapokea vigogo wengine ndani ya wiki hii(note my words)
Na lowassa je aliyepiga kura ya NDIOKweli Warioba amesahau kuwa katiba aliyopendekezwa ilikataliwa na CCM Akiwemo Kufuli
Wote ni mashuhuda. Wote mnajua. Mnajua ulivyokuwa msimamo na mtifuano wakati wa mchakato wa Katiba mpya. Mnayajua,kuyahifadhi na kuyakumbuka maneno na matendo ya wanaCCM kuelekea kwa Wajumbe wa Tume ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Warioba.
Tume nayo ilijibu mapigo na kuchagiza kwa midahalo wakati na baada ya mchakato. Wananchi waliamini CCM haiwapendi wajumbe wa Tume na Tume ikatetewa hasa na UKAWA. Akina Jaji Warioba waliitwa wapinzani. Mambo yalikuwa hivyo.
Sasa,Jaji Warioba,Polepole na wajumbe wengine wanaipigania CCM. Wamesahau walivyotwezwa,kutukanwa na kukandiwa. Walikuwa wanawatapeli na kuwalaghai watanzania?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Aisee hiyo nayo point,ila mie nadhani pale jukwaani alilazimishwa kupanda ili kumfunga mdomo au kuziba aibu ya kutokwepo mawaziri wakuu wastaafu.May be tetesi za mkakati wa kuhamia upande wa pili huenda zikawa zipo njiani huenda ni kweli.Lakini kusema CCM watamuelewa na serikali tatu naona atakuwa anapoteza muda.Labda kama anataka kuwachanganya hapo nitamwona Warioba geniusSuper sub;Mambo vipi!Ebu niambie, kwa nini Mzee Warioba hakuvaa vazi la chama?
Aisee hiyo nayo point,ila mie nadhani pale jukwaani alilazimishwa kupanda ili kumfunga mdomo au kuziba aibu ya kutokwepo mawaziri wakuu wastaafu.May be tetesi za mkakati wa kuhamia upande wa pili huenda zikawa zipo njiani huenda ni kweli.Lakini kusema CCM watamuelewa na serikali tatu naona atakuwa anapoteza muda.Labda kama anataka kuwachanganya hapo nitamwona Warioba genius