Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho Jumatatu.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya Katiba yenye mambo mazito na makubwa.
Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40.
Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa wameahidi awali.
Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2