Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Status
Not open for further replies.
Katiba mpya itakuwa ni mkombozi ni vema tume wakafanya kweli.
 
bora iwe hivyo hakuna mbunge kuwa waziri,halafu uteuzi wa mawaziri ufuate uwiano wa jinsi vyama vimechukua viti vingapi vya ubunge,na waidhinishwe na bunge.

yàni unamaanisha wanachama wa vyama ndio wawe mawaziri? you must be joking. Tumepoteza dira, tumeanza kubahatisha kipi chaweza kuwa sahihi. Dhana ya kuwa na mawaziri wanasiasa hasa wabunge ni uwezekano wa kuwawajibisha kisiasa na kupunguza gharama pamoja na kuwapa mikataba mifupi ya kazi.
 
Aiseee! Ngoja tusubiri, Kinana kawaruhusu? Na fastjet a.k.a msaidia mateja wenye macho mlegezo, paja zenye tattoo na kiuno chembamba NA siyo akina Ngwair?

Hawa wazee wameamua waingie katika historia ya Taifa hili.Lakini pia hata Rais Kikwete akiafiki haya mambo makubwa bila upinzani wowote naye ataingia katika historia ya aina yake.
 
wewe unamjua warioba au unamsikia anamsimamo kama jiwe atawashangaza wengi.


Duh!! Mkuu utanivunja mbavu kwa kicheko!! Msimamo Bongo!!?

Kuna mtu alikuwa na msimamo kama Lipumba!!? Ungeamini kama anaweza kuuza kura za wananchi!!? Mkuu nadhani umesahau "penye udhia penyeza rupia"!!

Umemsahau yule mwingine aliambiwa na chama chake ajitoe, alicong'aka!!? Chezea wanasiasa ndugu yangu, huwa hawaaminiki hawa!!

Btw naombea iwe kama ilivoripotiwa, pengine shetani kaokoka!!
 
umeonyesha umahiri.....ila kwenye issue ya mawaziri kutokua wabunge unasema haina logic?.....huo ni umahiri wa kipuuzi...afu we gamba sema unajitahidi kurudisha akili kichwani

mimi sio gamba ni gwanda ila mfuasi wa sera sio watu. Hilo suala la uwaziri tunabishana bila kufikiri. Makatibu wakuu ndio watendaji wakuu lakini mambo yapo hovyo. TUMESAHAU JAIRO, NYONI, RUTABANZIBWA etc. Wameharibu sana katika wizara zao tena hawakuwa wabunge. Tatizo uwajibikaji mkù
 
Kwa suala la katiba inabidi kuwa makini na tusianze kuspeculate kwani inaweza ikawa janja yao kuangalia mwitikio utakuwaje. Sio ajabu kuna rasimu zaidi ya moja na wanaweza wakachomoa yoyote kulingana na maelekezo ama matakwa ya watawala.
 
wataruhusu na uliberali uwe rasmi visiwani??

Ha ha ha! Nimeipenda hiyo. Mkuu mimi sio mtaalamu wa mambo ya katiba ila ninavyojua ideology ni suala la kichama zaidi kuliko la Katiba ya Nchi. Pamoja na Katiba ya nchi kuwa ndio msingi mkuu na sheria mama ya uendeshaji wa nchi, bado kwa kiasi kikubwa nchi huathiriwa na ideology ya chama kilichoko madarakani.

So, sio ajabu nchi ikaathiriwa na ULIBERALI kwa kiwango cha kutisha endapo chama chenye ideology hiyo kitakamata madaraka. Kwa kuwa yaliyofichika yameanza sasa kufunuliwa, ni jukumu letu wananchi kuamua tunataka nchi yetu iendeshejwe; kiliberali yaani HAKI SAWA KWA WOTE kwa kumpatia kila mmoja "ile kitu roho inapenda" au vinginevyo.
 
Ardhi inayotumika iwe mali ya mtumiaji na isiyotumika ndo iwe mali ya Taifa
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU.

Tume haitengenezi jambo jipya, inaandika mambo ambayo wananchi wameyatoa kwenye maoni yao. Rasimu sio ya Tume ni ya watanzania.
 
Hawa wazee wameamua waingie katika historia ya Taifa hili.Lakini pia hata Rais Kikwete akiafiki haya mambo makubwa bila upinzani wowote naye ataingia katika historia ya aina yake.


Mkuu Molemo,
Binafsi natamani sana kuona jambo hili likiwa kweli, lakini tatizo ninaloliona mchakato mzima tangu mwanzo ulichukua sura ya kisiasa zaidi ya utaifa!! Shetani kaokoka!!??

Pia wasiwasi wangu, wazee wanaweza kuwa wazalendo, je Rais na "wenye nchi" kule Bungeni (maana ni wengi "ndiyooo") wataukubali uzalendo huu!!?

TUZIDI KULIOMBEA TAIFA LETU DHIDI YA WANYONYAJI!!
 
Mkuu Molemo,
Binafsi natamani sana kuona jambo hili likiwa kweli, lakini tatizo ninaloliona mchakato mzima tangu mwanzo ulichukua sura ya kisiasa zaidi ya utaifa!! Shetani kaokoka!!??

Pia wasiwasi wangu, wazee wanaweza kuwa wazalendo, je Rais na "wenye nchi" kule Bungeni (maana ni wengi "ndiyooo") wataukubali uzalendo huu!!?

TUZIDI KULIOMBEA TAIFA LETU DHIDI YA WANYONYAJI!!

Mkuu wangu ninaamini Tume ya Warioba ikitoa Rasimu hii itakuwa ni kuondoa lawama hasa kutokana na kuvurugwa zoezi la uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza.

Pili ni lazima tukubali kwamba wazanzibari kwa umoja wao wanataka serikali tatu.Ndani ya tume nusu ya wajumbe ni wazanzibari.

Tusubiri tuone.
 
Tunaitaji tanzania endelevu habari za vyama vya siasa iwekwe pembeni.
 
Aiseee! Ngoja tusubiri, Kinana kawaruhusu? Na fastjet a.k.a msaidia mateja wenye macho mlegezo, paja zenye tattoo na kiuno chembamba NA siyo akina Ngwair?
Huo ni wivu unakusumbua? Kwani ulisikia mangwear alikuwa adicted kiasi cha mtu unayemtaja. Kule south afrika si alienda kikazi kuonyesha kuwa hakuwa na matatizo yoyote na tuliambiwa kuwa alipiga shoo tano
 
Kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri ni kitu ambacho hakina logic. Mambo ya umri wa uraisi sio màmuzi mazito kwan lilikuwepo hata kwenye katiba ya sasa. Mambo ya msingi na mazito ni kuhusu mamlaka ya urais kama taasisi na sio mtu, watueleze matumizi ya rasilimali zetu, muundo na uendeshaji wa muungano, uhuru, haki na wajibu wa raia wetu, mipaka ya uwajibikaji katika taasisi za kiserikali, itikadi na falsafa ya taifa letu na pia muundo na muingiliano wa nguzo kuu za dola. Hatutaki porojo.

Mkuu chukua like mia mbili natumia mchina sijaona maamuzi magumu hapo angesema tuwe na baraza la mawaziri wasio wanasiasa ( Technocrats) tungeelewa,kuweka serikali ya Tanganyika ni kutuongezea gharama za uendeshaji walipa kodi
 
Kwa mara ya kwanza Leo naomba kuunga mkono, hivi vyama kuna siku vitapotea but our country is there hata utimilifu wa dahari.

Kweli mkuu kuna mambo mengine yanayoathiri taifa kwa wakati mrefu sana sasa ukileta ushabiki wa vyama kila sehemu ni kitu mbaya sana.
 
Kama kuna kitu tume itafanya niisifu basi ni kufuta nafasi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya. Second ni kufuta mbunge kuwa waziri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom