Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Status
Not open for further replies.
Kuna watu humu hata hawaelewi theories wala mifumo ya governance duniani ilivyo, wanataka waibue yao wao tu wanavyoona. Hili jukwaa sasa linaanza kuharibika kwa kweli, hakuna hoja tena ni utani, kejeli na maudhi tu. Michango ya kitoto imetawala jukwaa sasa, basi ni aibu tupu...

kajipange upya
 
ha ha basi tutakushukuru mzee wetu ila usisahu matokeo ya uraisi kupingwa mahakamani pliz mzee na mahakama zetu ziwe huru na zitoe haki...tutaanza kuisoma kesho

big up haya ndiyo mambo ambayo watanganyika tunayaitaji, vile vile spika asitokane na chama chochote ili maslai ya taifa ndiyo iwe kipaumbele na si maslai ya vyama , waziri mkuu tumchague ili awe na maamuzi na si kutuletea habari za ingekuwa ni uamuzi wangu D. Jairo ninge................... HATUTAKI WAZIRI MKUU ASIYE NA MAAMUZI WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NO KUTEULIWA NA PREZIDEE
 
Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho Jumatatu.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya Katiba yenye mambo mazito na makubwa.

Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40.

Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa wameahidi awali.

Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2
Na ndoma CHADEMA wamesubili waoe rasimu we unazani tunapinga bila kuwa na hoja na unadhani tunapinga hata mambo mazuri, CHADEMA Tutaisoma rasimu hiyo kama inakidhi matakwa ya watanzania tutasapoti rakini kama haikidhi itapingwa tena kwa nguvu kari, tena ujue mambo uliyo yataja sio pekee yanayo hitajika Tanzania kuna mambo mengi sana.
 
wacha tuzidi kukuombea mzee wetu warioba haya ndio mambo tunayataka sisi wananchi wa tanzania tuko pamoja na nyinyi
 
Kesho siyo mbali, inshaalah, tutaiona rasimu hiyo!
 
Ni vizuri kabisa Tanganyika wakiwa na Nchi yao mama nchi 2 huru ndizo zilizo ungana hapo kabla na Zanzibar na wao wakiwa na nchi yao bendereza zitapepea pa pa pa pa pa pa pa pa kule New York, Commonwealth na Adis ababa
 
Mapolisi kubambikia watu kesi pamoja nda madaraka ya DPP kuingilia uhuru wa mahakama nayo imo?
 
Na ndoma CHADEMA wamesubili waoe rasimu we unazani tunapinga bila kuwa na hoja na unadhani tunapinga hata mambo mazuri, CHADEMA Tutaisoma rasimu hiyo kama inakidhi matakwa ya watanzania tutasapoti rakini kama haikidhi itapingwa tena kwa nguvu kari, tena ujue mambo uliyo yataja sio pekee yanayo hitajika Tanzania kuna mambo mengi sana.

Angalia sehemu ulizo weka R inatakiwa uweke L ha ha au unafanya makusudi...
 
Ngoja tusubiri hayo maamuzi. Hivi report anakabidhiwa Rais au itatolewa hadharani?
 
Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho Jumatatu.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya Katiba yenye mambo mazito na makubwa.

Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40.

Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa wameahidi awali.

Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2

ndo maana wengi wanajidai hawatagombea ubunge 2015
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom