Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Tume ya Warioba yaja na Rasimu ya Katiba yenye maamuzi mazito...

Status
Not open for further replies.
Selikali isiyo na dini, tume huru ya uchaguzi, Selikali tatu (Tanganyika, Zanzibar na Muungano), mihimili mitatu iliyo huru (selikali, Bunge na Mahakama.

Lakini pia ningetarajia katiba iweke utaratibu wa kura ya maoni toka kwa wananchi husika (au hata national wide, kulingana na uzito wa jambo) hasa serikali inapoingia mikataba mikubwa na ya muda mrefu. Kwanza ipitie baraza la mawaziri, kisha Bungeni, na ikibidi wananchi wapige kura ya ndio ama hapana kwani mwisho wa siku hao ndio wenye nchi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kumekucha, ifikapo saa nane mchana leo, Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba itazindua Rasimu ya Katiba Mpya, tukio hilo litafanyika Jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Karimjee, ni wakati wako wewe Mtanzania kuhakikisha unaipata Rasimu hiyo ili uone kama maoni yako yamefanyiwa kazi kama unavyotarajia au la, lakini pia uweze kutoa maoni yako. TBC itarusha moja kwa moja uzinduzi huo.
 
I'm doubting Thomas, Let keep our fingers crossed!
 
Aiseee! Ngoja tusubiri, Kinana kawaruhusu? Na fastjet a.k.a msaidia mateja wenye macho mlegezo, paja zenye tattoo na kiuno chembamba NA siyo akina Ngwair?

Ha! Ha! Ha! Ha! Weee! Mbona kama kuna kajiukweli kwa mbaaali !
 
molemo , mimi nasubiri kwanza niisome bhana ! Maana kiukweli simuamini kabisa Sinde Warioba , hebu Chungulia na kule kunakohusu Mafao ya viongozi wastaafu , mfano Marais , Mawaziri wakuu ( ambako warioba naye yumo ) , wakurugenzi na wengine wanofanana na hao .
 
Hiyo rasimu ya katiba ije na Mwarobaini wa kumaliza kero za muungano.....bila hivyo, hiyo rasimu itaishia Chumbe!
 
Bila Shaka ukumbi wa Karimjee mida hii upo kwenye joto, ukisubiri kauli ya kuzaliwa upya kwa nchi yangu ya Tanganyika!
 
Waumini wa Serikali mbili za Muungano CCM watafanyaje kama hayo yatakuwa ndo maoni ya watu? Lakini kama wakuu wa mikoa na wilaya bado wapo mimi sitaiunga mkono hiyo katiba bado!
 
Tuna subiri kwa hamu na gamu leo mtoto aliefichwa kwa miaka 49 ataonekana leo. Mwenzake ashakuwa anakwenda mbio .
 
Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba inatarajiwa kutoa Rasimu ya Katiba kuanzia kesho Jumatatu.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya tume hiyo zinasema wajumbe wa tume hiyo wameamua kuweka itikadi za vyama pembeni na kuibuka na rasimu ya Katiba yenye mambo mazito na makubwa.

Kati ya yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ni Uanzishwaji wa Serikali ya Tanganyika,Tume huru ya uchaguzi na pia kupiga marufuku wabunge kuwa mawaziri.Pia tume hiyo imependekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40.

Wachambuzi wa mambo wanasema haya yatakuwa ni maamuzi magumu na mazito yamefanywa na tume na pia itakuwa imeondoa kabisa uwezekano wa Chama cha CHADEMA kuongoza watanzania kuipinga katiba hiyo kama walivyokuwa wameahidi awali.

Source: Tanzania Daima Jumapili UK. 2

KESHO si ndo LEO? mbona kimya?........... ila bado saa sita usiku haijafika, wacha tuwe na subira kwani huvuta kheri

 
ni saa hizi vile, na redio gani ambayo online tunaweza kuwasikia mwenye news na link atusaidie
 
Nasikia suala la mahakama ya Kadhi halijaungwa mkono na mjumbe yeyote hasa ukichukulia wajumbe walio wengi wanafanya mambo kwa weledi
 
"kisoiva kitu gani mbona hamu mwatutia" nnakumbuka katika beti moja za kitabu flani niililkisoma nikiwa shule
 
Jaji Warioba kaamua kumfunga Paka kengele
 
Majimbo yanakuja wabunge wengi wataenda benchi. Bungeni itapita hii?!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom