Tumeachana rasmi

Tumeachana rasmi

Ulichokosea ni kumdanganya, ni bora umuambie ukweli ili ajue, kwa hiyo kesho ukipata hela utataka urudishe majeshi
 
Nimekua pamoja na huyu binti kwa miaka miwili na ziada. Marafiki na baadhi ya ndugu kila upande wanajua mahusiano yetu. Kilichopelekea kuachana nae ni hali yangu duni kiuchumi. Kwa kipindi cha takribani mwaka na nusu sasa napitia hali ngumu sana.

Kwa mwanaume ni ngumu kudumisha mahusiano kama haupo stable kiuchumi, sio binti muomba hela akiniomba basi najua kabisa huyu ana shida kweli tatizo hata hizo mara chache anapoomba msaada wangu nakua sina kitu.

Baada ya kujitafakari nimeona ni bora tuachane uenda akakakutana na mwingine mwenye hali nzuri. Sijamuambia sababu nipo broke nimetafuta sababu nyingine. Kama kawaida kaniaga kwa maneno makali kidogo lakini nilishajiandaa kwa ilo.

Vijana wenzangu usiwe commited kwenye mahusiano kama bado uchumi unayumba. Hata kama mwanamke anakupenda kwa hali yako hautakuwa sawa kisaikolojia. Siku ya pili sasa bado najilaumu kwa nilichokifanya lakini maisha lazima yaendelee. Nimelazimika kumuacha kwa sababu nampenda.
Akili yako ndogo sana..
 
2020 niliacha binti kwa style hiyo kwa sababu hiyo hiyo ya kupigika na najua asinge weza nivumilia mashida zangu na sikumwambia kuwa nimekuacha ila nilijiweka sipo-nipo ahadi nikaisogeza mbele ili aamue kusepa au kubaki akasepa zake. Last conversation yetu alinitukana kipuuzi saana eti kama ni pesa basi niwe freemason nitapata kwa kebehi lukuki kedekede nikanyong'onyea kiasi ila nashukuru nilijiandaa kwa kila kitakacho tokea baada ya maamuzi yale. Mungu ni mwingi wa rehema nimehangaika angalau nipo njia yenye uelekeo wakujitafuta zaidi. Aliolewa now sijui maisha yake ila tia maji kachoka walio mwona wanavyosema. This is life. Hakuna wakukuvumilia pambania kombe lako mapenzi waachie wahindi wale waigizaji
Kwa hiyo tia maji na kuchoka kwake wewe kunakufurahisha maana ni kama umeandika kipande hicho kwa bashasha sana.

Muombee afanikiwe na awe na maisha mazuri huko aliko bana. Kufurahishwa na maisha magumu ya ex wako siyo ishara nzuri....
 
Tafuta tu hela mwaya, penzi bila hela ni kama uji usio na sukari wala maziwa wala limao....haunyweki!!!
Atafutie wapi mtafanya ajiingize kwenye vitendo viovu aridhike tu na alichonacho akubaliane na umaskini uwe kama pambo kwake ila asimuache mpenzi coconut oil au baby care mpaka pale atakapofariki..hela sio zakila mtu unaweza kupambana na ukazikosa
 
Kwa hiyo tia maji na kuchoka kwake wewe kunakufurahisha maana ni kama umeandika kipande hicho kwa bashasha sana.

Muombee afanikiwe na awe na maisha mazuri huko aliko bana. Kufurahishwa na maisha magumu ya ex wako siyo ishara nzuri....
Hapana mkuu sijafurahishwa na huwa sipendi kumfuatilia wanaonipa taarifa nimewakataza wasinipe taarifa za kumhusu yeye. Na huwa sikuwa na ubaya wowote na yeye sema alishindwa kuonesha kunisupport kwenye hz hustle za mtaa so akaona anitukane kuwa kama nipesa niwe freemason. Mkuu mm sina kinyongo wala kisasi nae maana i was real 100%
 
Nimekua pamoja na huyu binti kwa miaka miwili na ziada. Marafiki na baadhi ya ndugu kila upande wanajua mahusiano yetu. Kilichopelekea kuachana nae ni hali yangu duni kiuchumi. Kwa kipindi cha takribani mwaka na nusu sasa napitia hali ngumu sana.

Kwa mwanaume ni ngumu kudumisha mahusiano kama haupo stable kiuchumi, sio binti muomba hela akiniomba basi najua kabisa huyu ana shida kweli tatizo hata hizo mara chache anapoomba msaada wangu nakua sina kitu.

Baada ya kujitafakari nimeona ni bora tuachane uenda akakakutana na mwingine mwenye hali nzuri. Sijamuambia sababu nipo broke nimetafuta sababu nyingine. Kama kawaida kaniaga kwa maneno makali kidogo lakini nilishajiandaa kwa ilo.

Vijana wenzangu usiwe commited kwenye mahusiano kama bado uchumi unayumba. Hata kama mwanamke anakupenda kwa hali yako hautakuwa sawa kisaikolojia. Siku ya pili sasa bado najilaumu kwa nilichokifanya lakini maisha lazima yaendelee. Nimelazimika kumuacha kwa sababu nampenda.
Kosa kubwa umefanya,Kwa hiyo ukipata hela ndio utatafuta mke?utapata Malaya tu
 
Back
Top Bottom