Kuna mwenzio ameoa mke kwa Mali kauli ikiwa hata kushika 500 kwa uwezo Hana akamtoa bush akaja nae town chumba cha Giza mwananyamala kwa makoma kwa mwezi 7000/- kachukua chumba akaanza kutafuta vibarua amemchukua mke 2017 akaanza piga saidia fundi beba sana zege jichanganya mapori ya ulinzi shirikishi usiku na kwenye makampuni ya ulinzi si haba mke akamwelewa 2020 akamtunuku mtoto wa kwanza msoto na wewe 2022 mke akamtunuku mtoto wa Pili sasa ni baba Ila kula yake na ya familia yake anaijua yeye na Mungu wake Ila maisha yanasonga Leo kapata kesho kakosa Ila alichobahatika alipata mwanamke mvumilivu sijapata kuona wangekua hawa maslay queen wanaotutunishia matako yaan siku 2 nyingi kashakimbiwa 2023 sasa ni baba wa watoto wawili anaishi chumba cha Giza Kodi inakata Mwezi ujao na hajui atamlipa nini mwenye nyumba lakini hajakata tamaa anakomaa na mkewe mpaka kieleweke , wewe unashindwaje mwanaume Simba toka lini akamwacha Swala aende?