nakaribia miaka 40 ya kuishi hapa duniani, nimepitia hali tofautitofauti kiuchumi na kimahusiano kwa nyakati tofauti pia.
Kwa hiyo nina uzoefu wa nini naongea, wewe ni starter yaani hujajipata bado lakini naona unafeli mwanzoni kabisa kutokana na hatua unazochukua.
Kuachana kupo sana na hata mimi nimeachana, lakini itokee kwasababu ya jambo ambalo lipo nje ya uwezo na ni gumu kutatulika kwa urahisi.
Hili lako una uwezo nalo, pambana , mrudishe mpenzio katika himaya yako.
Halafu naona hili unalijutia hapo ulipo sema unakaza fuvu tu, ndio maana umelileta huku.