Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Serikali yetu inajikanganya sana. Tuliambiwa lengo la tozo ni kujenga madarasa nchi nzima. Kwenye hotuba ya Rais wetu mpendwa, akasema kunakifedha kakipata mahala. Cha ajabu serikali inakuja na mpango wa kujenga madarasa kila jimbo kwa fedha ya mkopo wa corona! Imenishangaza sana! Hivi kweli hatuna fedha za ndani hadi tuchukue mikopo kujenga madarasa? Hii ni aibu kubwa! Hivi huyu Kikwete aliwezaje kujenga shule kila kata, na hakukopa IMF wala Benki ya Dunia kukamilisha hizo shule.
Serikali ilijisifia kuwa tozo ndo suluhisho pekee kumaliza shida ya madarasa, leo huo mpango umesitishwa? Basi serikali ondoeni tozo, au punguzeni asilimia kubwa ya tozo kuwapa unafuu watanzania ambao hawafaidiki na nchi yao. Kila kitu kwao imekuwa mzigo. Hivi kodi ya ndani inafanya nini? Hayo makusanyo yanaenda wapi? Hivi mnaona raha na hiyo mikopo, badala ya wizara ya fedha na waziri wake kutumia akili kutafuta vyazo vya mapato, ninyi mnakimbilia kuchukua mkopo uliotokana na Corona kujenga madarasa. Viongozi wa ajabu sana.
Ni heri hata huo mkopo kwa kuwa ni wa corona, ungetumika katika uboreshaji wa huduma za afya nchini, mfano ununuzi wa vifaa tiba, hospitali nyingi hazina vifaa, madawa bado ni shida, mitungi ya gesi, kwa sababu swala ili ni changamoto kwa vituo vya afya hata hospitali kubwa. Kuliko kukimbilia madarasa, wakati mlituhakikishia madarasa yatajengwa kwa tozo, na kumaliza shida ya upungufu wa shule.
Tuambiwe Fedha ya tozo, inaenda wapi? Wapinzani mko wapi, naona CCM imechoka kabisa na imefikia mwisho wa kufikiri. Na watanzania hatuoni mabadiliko ya kweli kiuchumi na kijamii. Ebu vyama vya upinzani, tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo wa kufikiri kidigitali, amkeni, iondoeni hii CCM. Acheni kususa, acheni kujijenge ninyi binafsi kwa umaarufu, tangulizeni uzalendo wa nchi, ondoweni kutumiwa na CCM, Ondoeni fikra za tunaibiwa, pambaneni, mbuni mbinu za ushindi, acheni kulalamika kila wakati, na uhakika watanzania watawapa ushindi!