Tumeambiwa Shilingi Trilioni 1 itajenga Madarasa, ni vema tozo ipunguzwe

Tumeambiwa Shilingi Trilioni 1 itajenga Madarasa, ni vema tozo ipunguzwe

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,649
Serikali yetu inajikanganya sana. Tuliambiwa lengo la tozo ni kujenga madarasa nchi nzima. Kwenye hotuba ya Rais wetu mpendwa, akasema kunakifedha kakipata mahala. Cha ajabu serikali inakuja na mpango wa kujenga madarasa kila jimbo kwa fedha ya mkopo wa corona! Imenishangaza sana! Hivi kweli hatuna fedha za ndani hadi tuchukue mikopo kujenga madarasa? Hii ni aibu kubwa! Hivi huyu Kikwete aliwezaje kujenga shule kila kata, na hakukopa IMF wala Benki ya Dunia kukamilisha hizo shule.

Serikali ilijisifia kuwa tozo ndo suluhisho pekee kumaliza shida ya madarasa, leo huo mpango umesitishwa? Basi serikali ondoeni tozo, au punguzeni asilimia kubwa ya tozo kuwapa unafuu watanzania ambao hawafaidiki na nchi yao. Kila kitu kwao imekuwa mzigo. Hivi kodi ya ndani inafanya nini? Hayo makusanyo yanaenda wapi? Hivi mnaona raha na hiyo mikopo, badala ya wizara ya fedha na waziri wake kutumia akili kutafuta vyazo vya mapato, ninyi mnakimbilia kuchukua mkopo uliotokana na Corona kujenga madarasa. Viongozi wa ajabu sana.

Ni heri hata huo mkopo kwa kuwa ni wa corona, ungetumika katika uboreshaji wa huduma za afya nchini, mfano ununuzi wa vifaa tiba, hospitali nyingi hazina vifaa, madawa bado ni shida, mitungi ya gesi, kwa sababu swala ili ni changamoto kwa vituo vya afya hata hospitali kubwa. Kuliko kukimbilia madarasa, wakati mlituhakikishia madarasa yatajengwa kwa tozo, na kumaliza shida ya upungufu wa shule.

Tuambiwe Fedha ya tozo, inaenda wapi? Wapinzani mko wapi, naona CCM imechoka kabisa na imefikia mwisho wa kufikiri. Na watanzania hatuoni mabadiliko ya kweli kiuchumi na kijamii. Ebu vyama vya upinzani, tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo wa kufikiri kidigitali, amkeni, iondoeni hii CCM. Acheni kususa, acheni kujijenge ninyi binafsi kwa umaarufu, tangulizeni uzalendo wa nchi, ondoweni kutumiwa na CCM, Ondoeni fikra za tunaibiwa, pambaneni, mbuni mbinu za ushindi, acheni kulalamika kila wakati, na uhakika watanzania watawapa ushindi!
 
Hizo fedha za mkopo ni kwa miezi 9 tu,na hazigusi maeneo yote na wala hazitamaliza shida zote,tozo unaziondoaje?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Walidai tozo itamaliza shida ya ujenzi wa shule sasa kwanini fedha ya corona ikajenge madarasa? Sijui unaelewa kile nachokieleza? Ni heri fedha ya corona itumike kwa mambo ya afya tu. Na pia hapa swala si miezi? Ni kiwango cha fedha iliyokopwa kutumika isivyo.
 
Tutatumia dola kubaki madarkani
Tuache uoga na hofu. Nakumbuka uchaguzi wa 2010, Mwanza walichoka na CCM majimbo yote mawili wakaipa upinzani. Nakumbuka jimbo la Nyamagana lilikuwa na upinzani mkubwa Wenje akichuana vikali na alie kuwa waziri wa mambo ya ndani Masha.

Siro akiwa kamanda wa Mwanza, alizuia askari kupiga wananchi, ilifikia sehemu nae akaonesha alama za vidole viwili. Watu walijazana Jiji, na walitoa onyo, atakae geuza matokeo halmashauri ya JIji itateketezwa kwa moto. Wenje alikuwa anunuliwe, watu wakapata nyepesi, wakamwambia tutateketeza wewe, Mkurungezi akiwa Kabwe, na Kamati ya uchaguzi, ofisi yote bila kujali wewe humo.

Watu wakaanza kuchoma ofisi ya CCM, kutoa onyo, kilichotokea serikali ikasarenda. Matokeo yakatangazwa Wenje ndo mshindi! So tuache kutafuta sababu, tukitishiwa tu kwa maneno, basi Oooh! CCM inasaidiwa na dola. Kama Mwanza waliweza, na Kikwete alikuwa akitaka Masha apite lkn wananchi walitamka hapatoshi. Na ikawa.
 
Una ongezewa deni la taifa afu mda huo huo una kamliwa kila kona ya kipato chako.maelezo yao hayatoshi sarakasi zina ishia kwenye ujenzi wa madarasa na afya basi
Maderu hafai hata kushika uongozi wa kitongoji.

Wasingempatia uteuzi akabakia rais wa kwenye miamba na madaraja maporini.
 
Walidai tozo itamaliza shida ya ujenzi wa shule sasa kwanini fedha ya corona ikajenge madarasa? Sijui unaelewa kile nachokieleza? Ni heri fedha ya corona itumike kwa mambo ya afya tu. Na pia hapa swala si miezi? Ni kiwango cha fedha iliyokopwa kutumika isivyo.
Kabla tozo haijapunguzwa walitarajia ku raise 1.2 Trillion. Baada ya kilio cha wananchi Serikali ilipunguza kiwango cha tozo kwa 40%, hivyo basi na makusanyo yatapungua kwa kiwango kama hicho hivyo kusabanisha NAKISI fulani.

Hiyo NAKISI ndiyo Rais SSH anajitahidi kuiziba kwa huo mkopo wa COVID-19. Nimejitahidi kufikiria NJE ya BOX
 
Nchi tajiri inapoendelea kukusanya tozo toka kwa wananchi wake inatia shaka.
 
Natarajia baada ya kupitisha stimulus plan ya miezi tisa, tozo zinaenda kuondolewa.......lakini utaona stimulus plan yenyewe imekaa kiulaji kwa watu wachache. Kuna wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi, makampuni ya watalii na wapigaji wachache kwenye maeneo niliyotaja kwenye halmashauri na kwingineko. Mimi niliutarajia hii stimulus plan ingelenga wakulima kwa kuweka ruzuku kwenye pembejeo hasa mbolea na pia kulipa increment za watumishi wa umma na wale watumishi ambao hawakupandishwa madaraja kutokana na uzembe na roho mbaya ya baadhi ya maafisa utumishi hasa wa kwenye wakala za serikali. Hivi majuzi waziri Mchengelwa kule Dodoma alielekeza hao maafisa utumishi wazembe waondolewe kwenye nafasi na kushushwa vyeo, lakini hadi leo nawaona wanapeta tu huku kwenye mawakala............​
 
Dada yangu kwenye Banda lake la M pesa alikuwa anapata kamisheni ya mpaka sh 100,000 kwa mwezi, lakini kutokana na athari za tozo sasa anaishia kupata 40,000 hadi 50,000.

Sasa je kuna Kiongozi yeyote atavumilia leo hii mshahara wake ukipunguzwa?.
 
fya

2960303_GOD_PLAN.jpg
 
Natarajia baada ya kupitisha stimulus plan ya miezi tisa, tozo zinaenda kuondolewa.......lakini utaona stimulus plan yenyewe imekaa kiulaji kwa watu wachache. Kuna wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi, makampuni ya watalii na wapigaji wachache kwenye maeneo niliyotaja kwenye halmashauri na kwingineko. Mimi niliutarajia hii stimulus plan ingelenga wakulima kwa kuweka ruzuku kwenye pembejeo hasa mbolea na pia kulipa increment za watumishi wa umma na wale watumishi ambao hawakupandishwa madaraja kutokana na uzembe na roho mbaya ya baadhi ya maafisa utumishi hasa wa kwenye wakala za serikali. Hivi majuzi waziri Mchengelwa kule Dodoma alielekeza hao maafisa utumishi wazembe waondolewe kwenye nafasi na kushushwa vyeo, lakini hadi leo nawaona wanapeta tu huku kwenye mawakala............​
Viongozi wetu hawana mipango mizuri kwa Watu wa chini.
 
Back
Top Bottom