Tumeanza kuishi kama wanyama, wakati wa ajali badala ya kusaidia watu waliopata ajali wanawaibia!

Halafu ndio haohao mitaani kwao wakisikia kelele za "mwizi,mwizi" hubeba matofali,mawe na shoka na kupondaponda wanaowaita vibaka na kuitwa "wananchi wenye hasira kali. Unafiki mtupu!
 
Kuna siku nilitoka saa 10 alfajiri kwenda Moshi na dereva wangu, kufika maeneo karibu na mkata tukapata ajali. Gari iliharibika vibaya ila sisi tulichubuka kidogo tu. Ilikuwa bado ni asb hakujakucha vizuri basi kijana mmoja alipoona tumepata ajali akaja pale akasema hapa sasa hivi watakuja vibaka kuwaibia kila kitu kama mtakubali kunilipa hela mimi nitakaa hapa kuwalinda na mali zenu mpaka mpate msaada. Tukakubali akakaa pale akatulinda tukamlipa na kumshukuru.

Mara nyingi ajali ikitokea wanaiba na wakati mwingine wanawaua kabisa majeruhi ili kupoteza ushahidi.

Dunia imeiasha na Kiama kimekaribia ndugu zangu tufanye kutubia
 
Hawa wanaoibia watu waliopata ajali inabidi wakikamatwa wapewe adhabu ili iwe fundisho kwa wenzao wenye tabia kama hizo
Nani awape fundisho, serikalini penyewe kila mtu ana_ba kwa urefu wa kamba zake. Watu wako biz, jitahidi/mwombe mola usipate ajali hiyo ndo pona yako. Tukutate Kizmkaz
 
Hawana huruma hata kidogo. Niling'ang'ania simu nikapigwa ngumi nzito kichwani nikaiachia pia
Cha kuchekesha kesho yake nilienda pale kwenye kituo cha mafuta nikaulizia kama naweza kurudishiwa vitambulisho Na kadi za bank. Afande wa hapo aliwatafuta nikarudishiwa ID zote na kadi za bank waliniomba nulipie elfu 50 nikachanganyikiwa. Nikarikiria hivi kwa nini tumekuwa mijitu mihuni kiasi hiki!
 
Wanaotakiwa kuwatetea wananchi nao wamekuwa wezi, karatasi na peni zimekuwa nyenzo muhimu kwenye kutekeleza wizi, huku jemedari mkuu aki endorse kuwa kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake!
 
Mbeya ndio kiboko,malori yakianguka tu tayari wanaenda kuiba mizigo na wakiwakuta wapo hai wanawamalizia na kuwaibia
 
Unatype huku uko kwenye boda boda nini?...maana makosa kama yote..."vicgtims"
"mpoaka" "hauo" "inasikitosha"
mama wa kuwarekebisha watu wewe mwenyewe Aaaaaa...
 
Hali ngumu pesa hakuna pesa
na ndiyoooo maan wanafanya hivyo
 
watu wamekua makatili sana hata kama maisha n magumu inabd tuwe na huruma hata kdg unamuibia mtu kapata ajali dah🥲
Mdogo wangu akipata Ajali ya boda alivunjika mguu katika Ajali hiyo.
Wakati anajiandaa kutupa taarifa watu wakaja wakamnyang'anya simu na kumpukutisha maokoto then wakala kona.
 
Mdogo wangu akipata Ajali ya boda alivunjika mguu katika Ajali hiyo.
Wakati anajiandaa kutupa taarifa watu wakaja wakamnyang'anya simu na kumpukutisha maokoto then wakala kona.
Pole sana. Yaani aibu!
 
Mdogo wangu akipata Ajali ya boda alivunjika mguu katika Ajali hiyo.
Wakati anajiandaa kutupa taarifa watu wakaja wakamnyang'anya simu na kumpukutisha maokoto then wakala kona.
watu wana roho za kikatili sana aisee
 
MBona unasifia ujinga
 
Hiyo ndiyo picha halisi ya jamii ya kiTz.

Uadilifu sifuri, kuanzia mabarabarani hadi maofisini.

Kuanzia kwa raia hadi kwa viongozi wakuu, ni mwendo wa kula kwa urefu wa kamba, corruption iliyokithiri yaani ni laana.

Anayeonekana ni mwema kumbe anakuwa hajapata tufursa ya kutenda ufisadi uliopo damuni!

Fursa ya kutenda uhalifu inapojitokeza, ndipo inapodhihirisha kuwa nchi yote ni ya wezi na vibaka hii.

Pole kwa waliopata ajali na kuporwa badala ya kupatiwa msaada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…