Uchaguzi 2020 Tumechangishwa tena michango. Nimeuchuna, sijatoa

Uchaguzi 2020 Tumechangishwa tena michango. Nimeuchuna, sijatoa

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Mkutano umeisha muda mfupi uliopita baada ya mgombea wetu kueleza sera zake.

Leo ameyameza maneno yake ya jana na hivyo ametueleza sera zake ni nzuri ila kuna sehemu anarudiarudia sana.

Kilichonisikitisha ni kuwa bado jambo lile la jana limejitokeza na leo kwa kuchangishwa michango ila leo aliyesema tutoe simu na kuchanga ni John Mrema, na sijui ni nani aliwaambia tunaokuja kwenye mkutano tuna namba za Voda tu.

Hatujachanga, kwa sauti ya unyonge sana tumesingizia tena network.

Watu ni wachache sana ila tukutane kesho Segerea.
 
Mkutano umeisha muda mfupi uliopita baada ya mgombea wetu kueleza sera zake.

Leo ameyameza maneno yake ya jana na hivyo ametueleza sera zake, ni nzuri ila kuna sehemu anarudiarudia sana...
Kwani ulisombwa na malori kwenda mkutanoni? Kama umeenda kwa hiari yako nakushangaa unalalamika nini, wanawake wa siku hizi mna tabu sana
 
Sisi tunachanga wenye roho za ibilisi moto uendelee kuwachoma, mjidhihirishe hadharani jinsi mlivyo wa shetani!
 
Tunachangishwa pesa kilazima aisee, eti toeni simu zenu wenye voda
Si mnasema wametumwa na MABEBERU? ina maana hao MABEBERU hawajawapa pesa hadi wanachangishana? Ukiwa Ccm hata uwe na PhD unakuwa mpumbavu kama mwenyekiti tu
 
Sasa iweje waseme tutoe simu? Kwani si waeke tu namba hadharani alafu tutachanga kwa muda tutaotaka? Kwa nn kila tunapokuja kwenye kampeni ndio mtuchangishe??
Ulazimishi kuchanga,kama huna basi sio lazima.
 
Sijalalamika kwenda, balj jinsi tunavyoombwa kuchanga michango
Kwani ulisombwa na malori kwenda mkutanoni? Kama umeenda kwa hiari yako nakushangaa unalalamika nini, wanawake wa siku hizi mna tabu sana
 
Sijalalamika kwenda, balj jinsi tunavyoombwa kuchanga michango
Acha upuuzi, kama hutaki kuombwa michango kaa nyumbani kwako, michango ni culture yetu ndio maana hata Lissu alitibiwa kwa pesa za michango yetu, M4C ilistawi kwa michango, wabunge walilipa faini mahakamani kwa michango yetu

Wewe kaa pembeni tu usitubabaishe, unabwabwaja kama mke mwenza
 
Back
Top Bottom