Tumegundua ushirikina/nguvu za giza unaofanywa na kijana kwenye biashara

Sasa hapo kuna shida gani? Mimi kama kazi inafanyika na hakuna hasara kama ulivyosema hayo mengine sio shida zangu.

Halafu ulitakiwa kujiongeza kwanini dogo anasema ataongea na boss wake, pengine ni mpango kazi wao huo wewe unaleta ujuaji.
Usikute dogo alikuwa anaporwa na kina chuma ulete na boss anakata hela ilio pungua. Dogo kaona ajiongeze nae kwa sangoma, ila dini hairuhusu ingawa mwana anapiga kazi balaaa😂😂
 
Usikute dogo alikuwa anaporwa na kina chuma ulete na boss anakata hela ilio pungua. Dogo kaona ajiongeze nae kwa sangoma, ila dini hairuhusu ingawa mwana anapiga kazi balaaa😂😂
Kigezo cha uvumilivu ni kwavile anapiga kazi....🤣🤣biashara ngumu sana, unawez kumsalit anaekupa pumz
 
Acha atimize jadi.
Jadi haina ugomvi nawe kwann usumbue mtu
 
Nyoya na kitu cheusi vilikua viashiria vya nguvu za giza. Labda angekubali kusema vinamaanisha nn
Mkuu, mimi naona wewe ndiwe mwenye imani za kishirikina. Unyoya na kitu cheusi ni vitu vya kawaida tu. Huenda anavitumia kuchezea na aliona aibu kusema mbele yako maana angeonekana mtu mzima mwenye michezo ya kitoto.

Halafu unasema ulienda 'kujifunza biashara', sasa umeenda umeyakuta hayo madogo umeyafungulia uzi. Je, ukioneshwa na misukule yake inayovuta wateja?

Hadi hapo umefeli mafunzo. Na huenda huyo nduguyo alipanga njama na kijana ili waone kama una kifua wakupe siri nyingine au la.
 
Umesema umegundua lkn sijaona uliposema ulichokigundua.
 
Kiherehere tu, mambo ya watu unayaleta huku sisi tukusaidie nini sasa? Hakika nchi hii tuna uhaba wa vijana! Kaka kama binti!
 
Binafsi siwezi kuvumilia ushirikina kwenye eneo langu la makazi au biashara.Muda huu huyo dogo angekuwa kwao Ifenkenya huko.
Bado yupo, lkn kwa vile sii jambo langu kufanyia maamuzi. Nipo nimetulia tuu
 
Kiherehere tu, mambo ya watu unayaleta huku sisi tukusaidie nini sasa? Hakika nchi hii tuna uhaba wa vijana! Kaka kama binti!
Kupitia mambo ya watu unaweza kujifunza. Huna adabu😡
 
🤣Humu JF mnatia watu ujasiri. Yani kwa mimi sio kitu cha kawaida
Tulia kijana, huko madukani kwetu ni misukule ndio inahudumia wateja....karibu dukani kwangu, karibu sana.
 
umewaza mbali saana, kijana kabisa yule(20s) sio mtoto useme anafanya michezo. Lakini nisikukatalie inawezekana kuna jambo, muda utanipa vya kujifunza
 
Tulia kijana, huko madukani kwetu ni misukule ndio inahudumia wateja....karibu dukani kwangu, karibu sana.
Utanikosa...bora nije kama sijui. Ukifunguka sitii mguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…