Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Baba pole sana kwa majukumu mazito ya kuliongoza Taifa hili, na pole sana kwa Uvushi na uvumi kuhusu Uhai na afya yako.
Mtego huu umewanasa wapinzani, wanaccm na wasio na vyama na umeacha funzo kubwa sana kwetu kama Taifa .
Mimi mwana team yako nakuomba tu uwasamehe wote maana hawakujua walitendalo
Pia nakuomba uwasamehe na usilipize kisasi maana Biblia Takatifu inatamka 'Kisasi ni cha Bwana' Warumi 12:19.
Ingawa Kuna maamuzi utafanya katika nafasi Fulani Fulani, lakini tenda kwa utulivu mkubwa tena pale inapobidi.
Kwingineko unaweza kupotezea ili wajifunze zaidi na kubadilika.
Nakuombea afya njema na nguvu, usikatishwe Tamaa na haya yaliyotokea.
Mtego huu, umekudhihirishia marafiki wa kweli na wanafiki hivyo usiutumie kuadhibu Bali kuboresha na kuimarisha palipo nyufa. Mwenyezi Mungu akubariki sana
 
Reactions: nao
Nilichojifunza ni upendo wa ajabu walionao watanzania hasa vijana juu ya Jembe letu JPM, maana walikuwa ktk khali ya taharuki uku wakianza kmsifia JPM na kuanza kumwombea kwa Mola,hakika Watu wanamkubali sana jembe letu.

Mimi binafsi naomba Mungu azidi kumpa Afya njema Raisi wetu mpendwa.

Amina,Mwisho

Watanzania tupuuze maneno ya uzushi yanayoletwa na vizandiki na wajinga juu ya mstakabali wa nchi yetu.
" wazushi kanyaga"
 
Wapinzani wamewekeza Sana kwenye mitandao ya kijamii, ukweli ni kwamba watanzania wengi wanampenda magufuli kuliko wachache wa kwenye mitandao,
Eti wanamfundisha raisi namna ya kufanya kazi,
Kumbukeni watu kufanya maovu duniani haimaanishi Mungu Yuko wrong.
 
Wengi kwa kipimo kipi chief?
 
Au ilikuwa ni drill ikilenga kuangalia kiwango cha usiri huko jumba jeupe kwa sasa na kuona mapokeo ya watu kama taarifa ingekuwa ya kweli. Ila kiukweli kupitia mitandao idadi kubwa ya watu walionyesha kufurahia taarifa ya awali. Inasikitisha sana.
Sasa katambua kuwa hata CCM wengi hawampendi
 
ccm wameshaturoga,hata wafanye upumbavu vipi tutawaunga mkono na wapinzani hata wakifanya jema gani hawawezi toboa hadi hapo watanzania wengi watapopata elimu zaidi ya ile ya kuvukia barabara
Sasa hata CCM wakifanya ujinga wao huwasingizia wapinzani ambao hawapo huru wamefungwa miguu na mikono
 
yote kwa yote, kuna kitu hakiko sawa mahali.

tukumbuke tu ya wahenga wetu..... mficha uchi hazai na mficha maradhi kifo humuumbua!
 
Waliuliza kwani alipotea siku ngapi? Ni mjinga mmoja aliwalisha ujinga wake wote wakaamini na ndiyo mwanzo wa kuulizia. Amewapitia kweli kweli na ni aibu kubwa.
 
Nimejifunza kuwa hii serikali imewadhuru wengi mno hadi hao watu wamejawa na roho ya kisasi.
 
Hakuna sehem nimekubali ya kigogo
Mi ni insider mwenyewe zaid ya kigogo,
Habari baadhi kigogo anazipata kwa wenye level ya kwangu hivo sina cha kupata kwa kigogo, labda mi nimpe kigogo


Kama inside, kilitokea maana nilikuona ukipuyanga sana
 
Kwani mkulu mwenyewe yuko wapi kipenzi cha watu?si ajitokeze tu awambie wanangu nipo.
 
Nenda Youtube utaona tukio lote la kuapishwa leo Jumapili 20/10/2019 ndiyo maana wanasaccos wako kimyaa kama wamenyeshewa mvua ya mawe.
Nani yupo kimya? Kwani wapinzani ndiyo waliwatuma CCM kwenda kumtupia Moshi wa kichawi huko Ruangwa?
 
Aaaa ujerumani sasa amerudi?
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…