Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 880
- 971
*UZUSHI DHIDI YA RAIS MAGUFULI UMETUACHIA MAFUNZO MENGI.*
Uzushi ulioshadadiwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuwa Rais Magufuli yupo hoi taabani ama amefariki dunia ni aibu nyingine kubwa.
Imesikitisha zaidi kwamba hata viongozi wakubwa wenye dhamana za uongozi waliingia katika upuuzi huu. Na wala sio jambo la kuficha kiongozi kijana kama Zitto Kabwe kushabikia upuuzi huu ni aibu kubwa kwake na ni kuwadhalilisha wananchi wa Kigoma Mjini waliomchagua kuwa Mbunge, ni aibu kwa familia yake, wanachama wa chama chake cha ACT na wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakishirikiana nae katika upuuzi kama huu.
Zitto ameandika sana kwenye mitandao akishabikia upuuzi huu, tena akipost picha ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride kwamba huyo ndiye Rais wa Tanzania baada ya Magufuli kufa. SHAME
Hata kama ameomba radhi lakini haiondoi kuwa yeye ni mpuuzi.
Zitto na wenzake akina Godbless Lema wa CHADEMA na vijana wao akina Yeriko na wengi wakaona wamepata pa kufanya majigambo ya siasa.
Nimejifunza nini?
1. Watanzania wengi wanampenda sana Rais Magufuli. Hapa mtaani kwangu baada ya Rais Magufuli kutokea kwenye TV mubashara akiwaapisha viongozi, kuliibuka shangwe kana kwamba Yanga au Simba imefungwa bao. Lakini pia katika mitandao ya kijamii unaweza kuona jinsi Watanzania wengi walivyofurahi baada ya kuthibitika taarifa za kuwa Rais Magufuli yupo hoi na kakimbizwa nje ya nchi hazina ukweli.
2.Tuna wanasiasa wa upinzani wa hovyo nchi hii haijapata kutokea. Wamekosa hoja za msingi ili wawe mbadala wa CCM na wamebaki kuokoteza uvumi na uzushi usio na mashiko. PUMBAFU KABISA.
3. Watanzania wamewajua wasioitakia heri nchi yao. Makatili na wenye uchu wa madaraka.
4. Huyo Kigogo wa kwenye Twitter amegeuka kuwa Kipimbi, muongo, mzushi, mchanganishi na hafai. Anaelezwa kuwa ni Zitto Kabwe kwa hivyo ndivyo thamani yake ilivyoanguka na wengi sasa wamejua kuwa ni mpuuzi.
5. Tuna Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo imekosa maarifa kabisa. Haiwezekani watu wanacheza na mitandao, wanayumbisha nchi na TCRA imekaa kimya tu. Wameshindwa hata kukemea tu. Nchi nyingine TCRA zao zinakuwa na ubunifu wa hali ya juu wa kuhakikisha hakuna loopholes za watu kutumia mitandao kupotosha ukweli na kuvuruga amani na utulivu. Ni ama akaunti zao zinafungwa ama wanatumia sheria za mitandao walizonazo kuwadhibiti. Lakini hapa kwetu ndio kwanza wapotoshaji akaunti zao zinapata verification na wanatamba wanavyotaka.
Makamu wa Rais waliyekuwa wanamtangaza kuwa anajiandaa kuingia Ikulu kwa zuria jekundu kaishia kugawiwa sambusa na JPM. Nae siku nyingine ajifunze kuwakemea watu wanaomgombanisha na Mkuu wa Nchi. Vinginevyo kwa uzoefu wa nchi nyingine mambo kama haya husababisha mtafaruku mkubwa kwa sababu huaminika wanaomchafua Rais wanatumwa na Makamu wake ambaye amepewa mpenyo wa kuwa Rais pale Rais aliyopo madarakani anapofariki dunia kwa mujibu wa Katiba.
Mama Samia Suluhu Hassan usikubali upuuzi huu wa akina Zitto Kabwe, usipoyaamini maneno yangu ipo siku utanikumbuka.
Mwisho, naungana na Watanzania wote kufurahia kushindwa kwa akina Zitto Kabwe na genge lake la akina Kigogo. WAMESHINDWA, WAMELEGEA NA WAMETEPETA.
Tuchape kazi Watanzania, kupata mtu wa aina ya Dk John Pombe Magufuli kwenye kitu cha Urais sio rahisi, ndio maana huyu tuliyenae anasifiwa kila mahali. Tushtuke jamani. Tumuombee afya njema na mafanikio katika jukumu tulilompa. Ni kwa faida yetu sisi.
Asalaam Aleikhum
Salim Said Makate
Dar es salaam
20 Oktoba, 2019