Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Andika maneno ambayo meko aliyasema juu ya tundu lissu kisha rudi umetete.

Kubali kwamba meko amewagawa watanzania na kuwaambukiza roho mbaya.

Watumishi wa umma kwa kiwango kikubwa hawampendi mtukufu magufuli
 
Hapana hauko sahihi...wasiompenda ni wale walimuamin mpambavu yule...hakuna siku nimeona live chat nyingi sana za kumfurahia raisi kama leo pale youtube. Kwani raisi si binadam kama binadam wengine?? Kwani akiugua ni shida? Mungu aendelee kumlinda na kumpa afya njema!!
 
Hukujifunza lolote mbali na umbea
Mimi nimeng'amua uyu jiwe amechukiza watu kiasi kwamba wanamtamani afe hii sio dalili nzuri kwa Taifa.
Mfano Kikwete alipougua dushe akapelekwa Marekani wengi tulimwombea apone sasa uyu kwanini wengi wanataka afe?
Kumbuka uyu anayejiita jiwe sio jiwe ni binadamu kama mimi na wewe anaweza kuugua nakufa pia.

Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 1.2 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji na Godbless Lema wakiamini uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli ni kuwa viongozi wa vyama vya upinzani hawajui linaloendelea Ikulu. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu!

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
 
Nadhani mleta uzi ndiye ana matatizo, watz wanakuaje wajinga kujali afya ya mkuu wa nchi wao, hebu atuambie pia kuhusu ile clip ya Ruangwa na ukomo wa ziara kwann wananchi wasiwe na hofu. Sio kila jambo kimya ni suluhisho. Watanzania wengi tunaomjali Rais tuliishi kwa hofu kinyume na wewe usiyejali au uliyedokezwa kutoka Ikulu kuwa hakuna shida.
Kama hapakuwa na haja ya press release nadhani asubuhi hata Mh Rais leo angetokea kanisa, siku nzima ya speculation ni muda mrefu sana.
Kuna siku wananchi watapuuzia na kutojali matukio ya kweli. Kuna haja ya kujali wananchi ambao mioyo yao ina nia njema kinyume na wabezaji.
 
Nimejifunza kuwa kuna kundi la wapigaji ambalo lamwombea JPM mabaya ili turudi zama za kupiga
 
Mkuu mbona una conclude kwamba Rais ni mgonjwa, umejuaje? Kigogo kadanganya watu hadi kufikia kutaja chumba ambacho ati Mh Rais alilazwa huko Ujeremani! Bado unasema Kigogo siyo muongo kwa 100%!! Ajabu
Kigogo anaishi na kufanya kazi ikulu ya magogoni, na wewe upo Magomeni, sasa wapi na wapi?
 
1.Watu wengi tena waliosoma bado wanaamini tatizo linaweza kutatuliwa kwa kumtakia mtu jambo baya, hatufahamu dhana ya kuwa sisi ndio nahodha wa maisha yetu na maisha tunayoyaishi ni uamuzi wa machaguo tuliyochagua na sio bahati nasibu wala mtu mwengine kusababisha tuwe tulivyo.

2.Upinzani bado hawajakua, bado hawajawa mbadala wa CCM, Wengi wanamchukia Magufuli kwasababu ya kuminywa mirija yao na sio wana uchungu na Watanzania.

3.Serikali imefanya jambo lililosahihi, kwa wakati sahihi katika namna sahihi kabisa.

4.Inawezekana kukawa na mageuzi makubwa ya vyombo vyetu vya usalama na ile mianya ya kuvuja kwa siri ambazo wengine hatupaswi kujua imeanza kuminywa kimya kimya, watu wenye kazi zao wapo kazini.

5.Watanzania tunapenda sana umbeya na Majungu, zamani tulikaa katika vijiwe vijiwe sasa hivi Teknolojia imeturahisishia kuendeleza tabia zetu za umbeya na Majungu.
No. 2 kwa hiyo tuamini kwamba kina Seth Rugema na hao wengineo walikuwa wakifisidi nchi kwa baraka za upinzani na si chama twawala?
 
Wanaomuombea mabaya rais ni wapinga dili, vyeti feki, waliotumbuliwa pamoja na rafiki zao ambao walikiwa wanapata za bure
 
No. 2 kwa hiyo tuamini kwamba kina Seth Rugema na hao wengineo walikuwa wakifisidi nchi kwa baraka za upinzani na si chama twawala?
Point yangu ya pili haimaniishi CCM haina mapungufu, Yes CCM ina Mapungufu yake Je hawa ambao ni mbadala wa CCM vitendo vyao vinatuthibitishia kuwa wapo tayari kuwa mbadala wa CCM? Wanasema heri zimwi likujualo kuliko lisokujua huu msemo ndo huwa tunautumia tunapopiga kura tu
 
Nenda YouTube leo wakati anaapisha viongozi uone live chart zaidi ya 10k walichangia positively ni record ya mwaka! Usihangaike na hawa wa tweeter na JF mawakala wa mafisadi.
Binafsi nimefurahi kumuona leo, nimeona kuna ujumbe Ikulu nzima ilikua inautuma kwa wananchi haswa wale wambeya, mfano kitendo cha uwepo wa viongozi wa dini, chakula cha pamoja vyote vilikua na meseji fulani.
 
Back
Top Bottom