Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Uzushi ulioshadadiwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuwa Rais Magufuli yupo hoi taabani ama amefariki dunia ni aibu nyingine kubwa.

Imesikitisha zaidi kwamba hata viongozi wakubwa wenye dhamana za uongozi waliingia katika upuuzi huu. Na wala sio jambo la kuficha kiongozi kijana kama Zitto Kabwe kushabikia upuuzi huu ni aibu kubwa kwake na ni kuwadhalilisha wananchi wa Kigoma Mjini waliomchagua kuwa Mbunge, ni aibu kwa familia yake, wanachama wa chama chake cha ACT na wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakishirikiana nae katika upuuzi kama huu.

Zitto ameandika sana kwenye mitandao akishabikia upuuzi huu, tena akipost picha ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride kwamba huyo ndiye Rais wa Tanzania baada ya Magufuli kufa. SHAME
Hata kama ameomba radhi lakini haiondoi kuwa yeye ni mpuuzi.

Zitto na wenzake akina Godbless Lema wa CHADEMA na vijana wao akina Yeriko na wengi wakaona wamepata pa kufanya majigambo ya siasa.

Nimejifunza nini?

1. Watanzania wengi wanampenda sana Rais Magufuli. Hapa mtaani kwangu baada ya Rais Magufuli kutokea kwenye TV mubashara akiwaapisha viongozi, kuliibuka shangwe kana kwamba Yanga au Simba imefungwa bao. Lakini pia katika mitandao ya kijamii unaweza kuona jinsi Watanzania wengi walivyofurahi baada ya kuthibitika taarifa za kuwa Rais Magufuli yupo hoi na kakimbizwa nje ya nchi hazina ukweli.

2.Tuna wanasiasa wa upinzani wa hovyo nchi hii haijapata kutokea. Wamekosa hoja za msingi ili wawe mbadala wa CCM na wamebaki kuokoteza uvumi na uzushi usio na mashiko. PUMBAFU KABISA.

3. Watanzania wamewajua wasioitakia heri nchi yao. Makatili na wenye uchu wa madaraka.

4. Huyo Kigogo wa kwenye Twitter amegeuka kuwa Kipimbi, muongo, mzushi, mchanganishi na hafai. Anaelezwa kuwa ni Zitto Kabwe kwa hivyo ndivyo thamani yake ilivyoanguka na wengi sasa wamejua kuwa ni mpuuzi.

5. Tuna Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo imekosa maarifa kabisa. Haiwezekani watu wanacheza na mitandao, wanayumbisha nchi na TCRA imekaa kimya tu. Wameshindwa hata kukemea tu. Nchi nyingine TCRA zao zinakuwa na ubunifu wa hali ya juu wa kuhakikisha hakuna loopholes za watu kutumia mitandao kupotosha ukweli na kuvuruga amani na utulivu. Ni ama akaunti zao zinafungwa ama wanatumia sheria za mitandao walizonazo kuwadhibiti. Lakini hapa kwetu ndio kwanza wapotoshaji akaunti zao zinapata verification na wanatamba wanavyotaka.

Makamu wa Rais waliyekuwa wanamtangaza kuwa anajiandaa kuingia Ikulu kwa zuria jekundu kaishia kugawiwa sambusa na JPM. Nae siku nyingine ajifunze kuwakemea watu wanaomgombanisha na Mkuu wa Nchi. Vinginevyo kwa uzoefu wa nchi nyingine mambo kama haya husababisha mtafaruku mkubwa kwa sababu huaminika wanaomchafua Rais wanatumwa na Makamu wake ambaye amepewa mpenyo wa kuwa Rais pale Rais aliyopo madarakani anapofariki dunia kwa mujibu wa Katiba.

Mama Samia Suluhu Hassan usikubali upuuzi huu wa akina Zitto Kabwe, usipoyaamini maneno yangu ipo siku utanikumbuka.

Mwisho, naungana na Watanzania wote kufurahia kushindwa kwa akina Zitto Kabwe na genge lake la akina Kigogo. WAMESHINDWA, WAMELEGEA NA WAMETEPETA.

Tuchape kazi Watanzania, kupata mtu wa aina ya Dk John Pombe Magufuli kwenye kitu cha Urais sio rahisi, ndio maana huyu tuliyenae anasifiwa kila mahali. Tushtuke jamani. Tumuombee afya njema na mafanikio katika jukumu tulilompa. Ni kwa faida yetu sisi.

Asalaam Aleikhum

Salim Said Makate
Dar es salaam
20 Oktoba, 2019
 
Uongozi mbovu hupelekea taifa kuwa na watu wenye maadili ya ajabu.

Kufurahia kifo cha mtu yeyote, sembuse rais, ni maadili ya ajabu. Maadili duni.

Waliofurahia uvumi wa kifo wamepungukiwa na maadili.

Lakini, wamefikaje huku kwenye kupungukiwa na maadili? Mbona viongozi wetu tuliwaheshimu sana mpaka heshima ikapitiliza?

Ukweli ni kwamba, jamii yetu imepungukiwa na maadili kuanzia chini kwa wananchi mpaka juu kwa viongozi.

Ndiyo maana mtu kama rais Magufuli anakuwa na kauli za ajabu zisizo na maadili.

Na kwa mfumo wetu wa "top down", mtu kama rais Magufuli alikuwa na nafasi kubwa ya kuonesha mfano wa maadili na kuirudisha nchi kwenye mstari, hata kwa kauli zake tu. Hafanyi hivyo. Anatukana tukana ovyo, anaropoka ovyo kwa namna ambayo haimfai rais, anachochea siasa za kugawa watu mafungu kivyama.

Sasa watu wanaona kama huyu rais tunayetakiwa kumuona ni mfano wa maadili anaongea ovyo hivi, basi kuongea ovyo ni ruhusa kwa kika mtu.

Kama mtu kazuia mikutano ya kisaiasa ambayo imeruhusiwa na katiba, wanasema bora afe wapate uhuru wao.

Kwa hiyo kuna tatizo kwa wananchi kukosa maadili, lakini pia kuna tatizo kubwa zaidi kwa viongozi kutoweka kipaumbele kwenye kuonesha mfano wa uongozi wenye maadili.
Yeye alifurahia Tundu Lisu aangamie sasa watumishi wake nao wamemuonyesha kuwa hawapo pamoja naye ingawa humzuka machoni lakini moyoni hawapo pamoja naye
 
Me i fully eleive that magufulis health is not RIGHT NEITHER IS IT OKAY, infact if you follow very carefully what he has been saying when going around the country you will discover that his MENTAL STATE IS UNSTABLE. have you heard what he has been talking at those places, times sacking people simply coz they are not in his convoy (like takukuru boss of mtwara, without first finding out if this boss is either sick or) telling a certain water engineer do you want this people to drink your urine? telling a certain woman who asked for water that she should go and request water from her husband, the list is endless, truth be told, MAGUFULI IS SICK BOTH MENTALLY AND HEALTH WISE PERIOD, i support those who share my views,
Acha uke.ge andika kiswahili. Ama wewe ndio ulie tumbuliwa?
 
Vicky Emmanuel Nchimbi wrote this piece.

"Huyu ni nani? Ni msemaji wa Ikulu au CCM? Ni Daktari au muuguzi wa Rais?"

"Ndio maana hata kwenye mkutano wa AALCO he will be represented by mama Samia."

Hii hoja Ni dhaifu kwakua ipo mikutano mingi sana ambayo amewakilishwa.
 
Ben Saanane na Azory gwanda wapo wapi? Tuanzie hapo kwenye hoja yako.
Me najua wapo wapi? Au unataka kusema nani na ni nani kawaweka wapi? Siitaji ligi na na wewe ila badilika,sito kujibu kitu tena,ila badilika mkuu
 
Ila somo amelipata, time will tell kwan ataishi milele? Anawatesa sana watu. Mseminari mwenzangu, tumesali Rozari, Novena na Antifona ila mimi zimenisaidia sana kuwa na huruma kuliko huyu anayejifanya Mkuu wa malaika.
Alipaswa kusomea upadri kule angeshepika na kuujua utu,nafsi,roho,angejifunza kuhusu Mungu,upendo,kuwathamini na kuwajali wengine na masomo tele yangemuondolea roho ya chuki,visasi,hasira,kiburi,majivuno,kuabudiwa ambavo ni hatari kwa moyo uujaza sumu ipelekayo heart attack mwisho heart failure.Anafanya mazuri mengine lkn hayaonekani yamefichwa na mabaya machache.Dabo std,kubinya Uhuru wa watu,kukandamiza haki za binadamu,lugha chafu zisizostaa kwa nafasi yake,watu wengi sana wameumizwa,wamekufa,familia zimesambaratika,ndoa zimevunjika,wamekatishwa ndoto zao,katishwa masomo sababu ya maamuzi ya uvunjifu wa haki zao kwa kufutwa kazi ghafla,kubomolewa nyumba zao,kubambikwa kesi za uhujumu uchumi,kuzulumiwa mazao yao,kuchukuliwa nyavu na vyombo vyao vya uvuvi, kuporwa pesa zao burea de change,kwenye mabenk,kufuata ushauri si udhaifu heri ufate ushauri usikilize utoanguka maana Biblia yasema taifa lolote pasipo mashauri litaangamia.Maana ya neno taifa ni kiongozi.Dunia imeumbwa juu ya misingi haitakiwi kuikiuka siasa za chuki na visasi ni hatari.
 
TANZANIA

nchi yenye watu wengi wenye AKILI

nchi yenye watu wengi wenye upeo wa kufikiri

nchi yenye Amani

nchi inayoendelea kwa speed ya 4G

nchi inayoongozwa na Kiongozi madhubuti

TANZANIA

nchi yangu
 
IMG-20191020-WA0110.jpg
 
Chadema na ACT vimekuja kuwa vyama vya ovyo haijawahi pata kutokea, vimekua ni vyama vya mihemuko na udaku bila hoja, falsafa au sera za msingi.
 
Nawe ni kapimbi tuu unatafuta udc.. nilidhani ungechambua pande zote mbili.. badala yale unatuletea uccm hapa.

Kwa taarifa yako hata wa ccm walikua wanafurahi boss wao kuugua..

Awamu ya 5 imewagwa sana watanzania na kuwapandikizia roho mbaya.
Uzushi ulioshadadiwa na baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuwa Rais Magufuli yupo hoi taabani ama amefariki dunia ni aibu nyingine kubwa.

Imesikitisha zaidi kwamba hata viongozi wakubwa wenye dhamana za uongozi waliingia katika upuuzi huu. Na wala sio jambo la kuficha kiongozi kijana kama Zitto Kabwe kushabikia upuuzi huu ni aibu kubwa kwake na ni kuwadhalilisha wananchi wa Kigoma Mjini waliomchagua kuwa Mbunge, ni aibu kwa familia yake, wanachama wa chama chake cha ACT na wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakishirikiana nae katika upuuzi kama huu.

Zitto ameandika sana kwenye mitandao akishabikia upuuzi huu, tena akipost picha ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride kwamba huyo ndiye Rais wa Tanzania baada ya Magufuli kufa. SHAME
Hata kama ameomba radhi lakini haiondoi kuwa yeye ni mpuuzi.

Zitto na wenzake akina Godbless Lema wa CHADEMA na vijana wao akina Yeriko na wengi wakaona wamepata pa kufanya majigambo ya siasa.

Nimejifunza nini?

1. Watanzania wengi wanampenda sana Rais Magufuli. Hapa mtaani kwangu baada ya Rais Magufuli kutokea kwenye TV mubashara akiwaapisha viongozi, kuliibuka shangwe kana kwamba Yanga au Simba imefungwa bao. Lakini pia katika mitandao ya kijamii unaweza kuona jinsi Watanzania wengi walivyofurahi baada ya kuthibitika taarifa za kuwa Rais Magufuli yupo hoi na kakimbizwa nje ya nchi hazina ukweli.

2.Tuna wanasiasa wa upinzani wa hovyo nchi hii haijapata kutokea. Wamekosa hoja za msingi ili wawe mbadala wa CCM na wamebaki kuokoteza uvumi na uzushi usio na mashiko. PUMBAFU KABISA.

3. Watanzania wamewajua wasioitakia heri nchi yao. Makatili na wenye uchu wa madaraka.

4. Huyo Kigogo wa kwenye Twitter amegeuka kuwa Kipimbi, muongo, mzushi, mchanganishi na hafai. Anaelezwa kuwa ni Zitto Kabwe kwa hivyo ndivyo thamani yake ilivyoanguka na wengi sasa wamejua kuwa ni mpuuzi.

5. Tuna Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo imekosa maarifa kabisa. Haiwezekani watu wanacheza na mitandao, wanayumbisha nchi na TCRA imekaa kimya tu. Wameshindwa hata kukemea tu. Nchi nyingine TCRA zao zinakuwa na ubunifu wa hali ya juu wa kuhakikisha hakuna loopholes za watu kutumia mitandao kupotosha ukweli na kuvuruga amani na utulivu. Ni ama akaunti zao zinafungwa ama wanatumia sheria za mitandao walizonazo kuwadhibiti. Lakini hapa kwetu ndio kwanza wapotoshaji akaunti zao zinapata verification na wanatamba wanavyotaka.

Makamu wa Rais waliyekuwa wanamtangaza kuwa anajiandaa kuingia Ikulu kwa zuria jekundu kaishia kugawiwa sambusa na JPM. Nae siku nyingine ajifunze kuwakemea watu wanaomgombanisha na Mkuu wa Nchi. Vinginevyo kwa uzoefu wa nchi nyingine mambo kama haya husababisha mtafaruku mkubwa kwa sababu huaminika wanaomchafua Rais wanatumwa na Makamu wake ambaye amepewa mpenyo wa kuwa Rais pale Rais aliyopo madarakani anapofariki dunia kwa mujibu wa Katiba.

Mama Samia Suluhu Hassan usikubali upuuzi huu wa akina Zitto Kabwe, usipoyaamini maneno yangu ipo siku utanikumbuka.

Mwisho, naungana na Watanzania wote kufurahia kushindwa kwa akina Zitto Kabwe na genge lake la akina Kigogo. WAMESHINDWA, WAMELEGEA NA WAMETEPETA.

Tuchape kazi Watanzania, kupata mtu wa aina ya Dk John Pombe Magufuli kwenye kitu cha Urais sio rahisi, ndio maana huyu tuliyenae anasifiwa kila mahali. Tushtuke jamani. Tumuombee afya njema na mafanikio katika jukumu tulilompa. Ni kwa faida yetu sisi.

Asalaam Aleikhum

Salim Said Makate
Dar es salaam
20 Oktoba, 2019
 
shame to them ata kama umpendi mtu usioneshe hisia zako za chuki wali fikia hatua mbaya kumuombea kifo
 
Ivi anaitwa nan kweli yule jamaa jina lake
Kwanza nimejifunza sasa tumepata Mkurugenzi makini ndani ya TISS,

Alijaribu kuwapa taarifa tofauti tofauti maafisa ndani ya idara ili aweze kugundua ni wapi wanavujisha siri za serikali kwa wakina Kigogo.

Kuna watu wanaenda kupata adhabu kali ndani ya idara.
 
Mbona kuna wana ccm walikua wamefurahi sana tuu
Chadema na ACT vimekuja kuwa vyama vya ovyo haijawahi pata kutokea, vimekua ni vyama vya mihemuko na udaku bila hoja, falsafa au sera za msingi.
 
shame to them ata kama umpendi mtu usioneshe hisia zako za chuki wali fikia hatua mbaya kumuombea kifo
Andika maneno ambayo meko aliyasema juu ya tundu lissu kisha rudi umetete.

Kubali kwamba meko amewagawa watanzania na kuwaambukiza roho mbaya.
 
Back
Top Bottom