Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Nduli Idd Amin kabla ya mauti yake kumfika alitubu na kumrudia Muumba wake, Ndugu Magufuli yeye ni nani asifanye hivyo? Huko kaburini atakua na hawa wapambe njaa wanao mtetea huku kwenye mitandao?
Kama hatobadirika, ama kwa hakika kifo chake itakuwa ni sherehe kubwa mno.
Acha upumbavu
 
Na tutambue kifo ni jambo la kawaida! Unazushiwa kifo wengine wanatamka amezushiwa mabaya! Hii akili binadamu tunaitolea wapi?

Ada ya binadamu haishi milele, atakufa tu! Na sote tunajua tutakufa tu! Tutambue hilo. Tuishi tutakavyoishi ila tutambue tutakufa tu.
 
Nduli Idd Amin kabla ya mauti yake kumfika alitubu na kumrudia Muumba wake, Ndugu Magufuli yeye ni nani asifanye hivyo? Huko kaburini atakua na hawa wapambe njaa wanao mtetea huku kwenye mitandao?
Kama hatobadirika, ama kwa hakika kifo chake itakuwa ni sherehe kubwa mno.
Hakuna lolote hapo,ni akili zako na ufahamu wako umekufikirisha hivyo, ikumbukwe kuwa jamaa kawashika vibaya sana watu wengi,Tunampenda Raisi wetu na tutazidi kumwombea
 
Sijasema kuogopa kifo. Siwezi ogopa haki yangu ya asili kama kuzaliwa.
Hoja hapa ni "iweje watu wafurahie Kifo" cha binadamu mwingine ilhali wao pia watakufa? Mwenye akili jibu ashalipata!

Kifo hakifurahiwa bali walioficha ukweli ndiyo waliyataka hayo wa kulaumiwa ni wale waliokaa kimya toka jana mpaka kupelekea waathirika watumishi wa umma na CCM wapinzani wa ndani ya CCM kufurahia kifo
 
Vyombo vya habari vimefungwa midomo. Unadhani watu watapata wapi habari nyeti na muhimu. Si ndio watu wamekimbilia kuamini umbea wa kina Mange, Kigogo and Co.
Yani mtu utamkuata anavyoelezea habari aliyosoma kwa Mange au kigogo utadhani aliiona ITV. Wa kulaumiwa tunamjua.

Siasa za hoja zilishavunjwa watu wanasubiria kipindi cha kampeni, halafu unataka watu wasifanye siasa za propaganda.

Waswahili hawakukosea waliposema utavuna ulichokipanda. Ulipanda bangi ndio utavuna hiyo. Sio unapanda bangi halafu unataka uvune mchicha.
 
We kwa akili zako meco ulomuona akiongea leo ni yule wa kawaida? Hujaona alivyo mpole.
Ukweli ni kuwa anaumwa ila hajafariki. Ila kwa jinsi ilivyoonekana mtandaoni ni kuwa hapendwi kabisaaaaa, hata ajifariji namna gani nguvu ilokuwa mtandaoni inaonyesha waz kuwa hapendwi,
OVER
Inawezekena una ID ishirini humu; kwa mantik hiyo utasema watu 20 hawampendi ?
 
Toba ni Siri kati ya Muumba na kiumbe chake sio kati ya Kiumbe na Kiumbe


Anacheni Rais anyooshe Nchi
 
Hahaaaaa....Kigogo kawaingizeni mjini nyumbu wakubwa nyie

Sijawahi kumuamini kigogo na wala sintokaa, au unadhani kila mtu ni bendera fuata upepo? Au unadhani kwakuwa kuna baadhi ya watu wanamuamini basi kila mtu anamuamini?
 
Magufuli ana tabia ya kutengenezea maadui hata sehemu ambayo hakuna ulazima wa kutengeneza maadui.

Watumishi wa umma kutokupandishiwa mishahara, wanajeshi jwtz kukaa kambini mpaka saa 12 jioni pasipo malipo ya overtime huku wakinyimwa mikopo waliyokuwa wakipata kipindi cha Tawala za nyuma ni Tatizo na hawawezi kumpenda, adui wa magufuli wapo huko huko CCM kwake.
 
Sijasema kuogopa kifo. Siwezi ogopa haki yangu ya asili kama kuzaliwa.
Hoja hapa ni "iweje watu wafurahie Kifo" cha binadamu mwingine ilhali wao pia watakufa? Mwenye akili jibu ashalipata!
Uongozi mbovu hupelekea taifa kuwa na watu wenye maadili ya ajabu.

Kufurahia kifo cha mtu yeyote, sembuse rais, ni maadili ya ajabu. Maadili duni.

Waliofurahia uvumi wa kifo wamepungukiwa na maadili.

Lakini, wamefikaje huku kwenye kupungukiwa na maadili? Mbona viongozi wetu tuliwaheshimu sana mpaka heshima ikapitiliza?

Ukweli ni kwamba, jamii yetu imepungukiwa na maadili kuanzia chini kwa wananchi mpaka juu kwa viongozi.

Ndiyo maana mtu kama rais Magufuli anakuwa na kauli za ajabu zisizo na maadili.

Na kwa mfumo wetu wa "top down", mtu kama rais Magufuli alikuwa na nafasi kubwa ya kuonesha mfano wa maadili na kuirudisha nchi kwenye mstari, hata kwa kauli zake tu. Hafanyi hivyo. Anatukana tukana ovyo, anaropoka ovyo kwa namna ambayo haimfai rais, anachochea siasa za kugawa watu mafungu kivyama.

Sasa watu wanaona kama huyu rais tunayetakiwa kumuona ni mfano wa maadili anaongea ovyo hivi, basi kuongea ovyo ni ruhusa kwa kila mtu.

Kama mtu kazuia mikutano ya kisaiasa ambayo imeruhusiwa na katiba, wanasema bora afe wapate uhuru wao.

Kwa hiyo kuna tatizo kwa wananchi kukosa maadili, lakini pia kuna tatizo kubwa zaidi kwa viongozi kutoweka kipaumbele kwenye kuonesha mfano wa uongozi wenye maadili.
 
Magafuli anatakiwa kujifunza kuwa humble na binadamu wenzake. Ukiona binadamu wenzako wanakuombea kifo ujue kuna mahali unawakwaza.

Kuwa humble na binadamu wenzako haimaanishi kwamba usitekeleza majukumu yako kama Raisi.

Mi nadhani aisikilize ile hotuba ya Kikwete vizur kuna kitu atajifunza.
Ke..nge katika ubora wako
 
Back
Top Bottom