Sijasema kuogopa kifo. Siwezi ogopa haki yangu ya asili kama kuzaliwa.
Hoja hapa ni "iweje watu wafurahie Kifo" cha binadamu mwingine ilhali wao pia watakufa? Mwenye akili jibu ashalipata!
Uongozi mbovu hupelekea taifa kuwa na watu wenye maadili ya ajabu.
Kufurahia kifo cha mtu yeyote, sembuse rais, ni maadili ya ajabu. Maadili duni.
Waliofurahia uvumi wa kifo wamepungukiwa na maadili.
Lakini, wamefikaje huku kwenye kupungukiwa na maadili? Mbona viongozi wetu tuliwaheshimu sana mpaka heshima ikapitiliza?
Ukweli ni kwamba, jamii yetu imepungukiwa na maadili kuanzia chini kwa wananchi mpaka juu kwa viongozi.
Ndiyo maana mtu kama rais Magufuli anakuwa na kauli za ajabu zisizo na maadili.
Na kwa mfumo wetu wa "top down", mtu kama rais Magufuli alikuwa na nafasi kubwa ya kuonesha mfano wa maadili na kuirudisha nchi kwenye mstari, hata kwa kauli zake tu. Hafanyi hivyo. Anatukana tukana ovyo, anaropoka ovyo kwa namna ambayo haimfai rais, anachochea siasa za kugawa watu mafungu kivyama.
Sasa watu wanaona kama huyu rais tunayetakiwa kumuona ni mfano wa maadili anaongea ovyo hivi, basi kuongea ovyo ni ruhusa kwa kila mtu.
Kama mtu kazuia mikutano ya kisaiasa ambayo imeruhusiwa na katiba, wanasema bora afe wapate uhuru wao.
Kwa hiyo kuna tatizo kwa wananchi kukosa maadili, lakini pia kuna tatizo kubwa zaidi kwa viongozi kutoweka kipaumbele kwenye kuonesha mfano wa uongozi wenye maadili.