Nimpongeze Tundu Lisu, amekaa kimya na hata alipotaka kusema alitamka maneno ya kuomba heri ya Mhe.Rais. Kwamba ameandika kutoka moyoni au la ni Siri yake na Mwenyenzi Mungu.
Niwaombe Watanzania tusivae ukatili mkubwa kiasi hiki, kiongoz anapohisiwa kupata tatizo Taifa linakaa kimya na kumwombea mazuri ila nimeshangazwa kuona mtaani hata wale wanaccm tuliotegemea wamwombee afya njema walibadilika na kuanza kujadili Kama Makamu anafaa au la. Sisemi wanaccm wote bali nasema na wale waliofurahia uvumi uliokuwa unaendelea.
Mawazi na wakuu wa Mikoa, mmeonyesha wazi kwamba upo unafiki ndani yenu na hapendwi mtu inapendwa ajira...mlikuwa na Uhuru wa kupost na kutoa tweet za faraja lakini mlikaa kimya na baadhi yenu mliwaza zaidi kuhusu next prezdaa kuliko kufuatilia afya ya aliyepo. Baada ya kutambua kwamba chuma kipo imara mkaondoka kabisa kwenye imani zenu za dini na kuanza kutengeneza posts za matusi na video zisizo na stahaa mkiamini kuwa maradhi na kifo vinaletwa na Binadamu. Kumbukeni na kaeni mkijua siku zote mtu apatwapo na matatizo au mpendwa wako anapopakaziwa kuwa na matatizo ukabaini huu buheri wa afya ni dhambi kuwashambulia wanaopakaza, yakupasa kumtukuza Mungu.
TBC, ninyi Ni chombo Cha Taifa na kinapaswa kusimama Kama chombo Cha Taifa achaneni na siasa na kujiendesha kishabiki...nyimbo ya Gozbeth haikupaswa kupigwa kwa wakati mliopiga...vipindi vyenu kwa siku tatu havikupaswa kupangiliwa mlivyovipangilia....tambueni wajibu wenu.
Kwa watawala, napenda kuwaomba mjifunze kitu kwenye tukio hili. HAKI IMEONDOKA, UHURU UMEONDOKA,USAWA UMEONDOKA, UBINAFSI UMETAWALA, CHUKI IMETAWALA. TAIFA LETU HALIPASWI KUSHANGILIA MABAYA YAWAPATAYO KIONGOZI WAO, TUJITAFAKARI MAANA IPO SIKU TUTASAIDIANA KWENYE SHIDA KUTOKANA NA VYAMA VYETU.
ADUI WA TANZANIA APASWI KUWA WATANZANIA BALI WATANZANIA WANAPASWA KUWA WALINZI WA TANZANIA.