Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa viongozi wetu wa vyama vikuu vya upinzani nchini hawajui kinachoendelea Ikulu. Hii imekuja baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini na kuushadadia uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu na Dkt Mashinji wanatoa mpaka ujumbe wa kuliombea Taifa huku wakiambatanisha mishumaa!

Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Uko sahihi kabisa mkuu.Hata mimi karibu nichukuliwe na huo uzushi,lakini nika stabilize baada ya kumuona Rais Ikulu akiendelea na shuhuli za kuapisha viongozi mbali mbali.Mkuu watu ni lazima wajue kwamba wapinzani na waathirika wa utawala wa Magufuli hawampendi,kwa hiyo wanatumia kila mbinu chafu kum-discredit kwa kusambaza uzushi ambao kwa njia moja au nyingine una nia ya ku-prove kwamba Rais anachukiwa na wananchi.Kwa hiyo ni kweli watu wanapaswa kuwa makini sana.

Kwa wapinzani issue ile,ambayo kama ilikuwa photoshopping sijui,lakini kwa ujinga wao walidhani kwamba ile ilikuwa opportune time ya wao kuonyesha kwamba Rais kweli anachukiwa sana na wananchi,jambo ambalo si kweli.
 
Uko sahihi kabisa mkuu.Hata mimi karibu nichukukiwe na upepo mkuu,lakini nika stabilize baada ya kumuona Rais Ikulu akiendelea na shuhuli za kuapisha viongozi mbali mbali.Mkuu watu ni lazima wajue kwamba wapinzani na waathirika wa utawala wa Magufuli hawampendi,kwa hiyo watatumia kila mwanya kum-discredit na kufurahia na kusambaza uzushi ambao kwa njia moja au nyingine una prove kwamba kweli anachukiwa.So ni kweli watu wanapaswa kuwa makini sana.
Hizi habari za kusema wapinzani ni waathirika wa utawala huu sijui mnazitoa wapi.

Hivi wakulima nao ni wapinzani?
 
Mazwazwa bado hawajaamini kama chuma kipo hai wanasema eti yule ni magufuli yule comedian wa iringa
 
Nenda YouTube leo wakati anaapisha viongozi uone live chart zaidi ya 10k walichangia positively ni record ya mwaka! Usihangaike na hawa wa tweeter na JF mawakala wa mafisadi.
Hahhahahaha unakimbia sehemu ya watu wanaojielewa,
 
Mkuu;
Kumbuka nchi yetu bado ni changa kwenye masuala ya mitandao na kwa sababu hiyo wanachi wengi wanaamini kila wanachokisoma kwenye mitandao.

Weka sawa kwanza,

je, hapakutokea sintofahamu yoyote kule Rwangwa?

Ile video inayoonesha watu wakisukumwa na wanausalama wa rais ni ya kweli au ya uongo?
 
Kiukweli tuache utani rais bdo hajawa katika hali yake ya kawaida.tumuombee watanzania...
Nadhani hii ziara ilikuwa ndefu Sana nadhani wandaaji wamejifunza kitu Kwa binadamu yeyote kusafiri Kwa muda wote huo lazima mwili uchoke ongezea na hotuba za chuma kwenye maeneo aliyopita lazima angechoka tu, nadhani kilichotokea ni uchovu wa safari ndefu ya ziara
 
Tusijisahau kwamba sisi ni wanadamu akiwamo Mheshimiwa Rais, kwamba kama walivyo wanadamu wote huamka hufanya shughuli zote za kila siku, na mwisho wa siku huhitaji kupumzika na kulala. Na huenda ikatokea simu moja au siku kadhaa mtu (Akiwemo Rais) akaumwa, akapata matibabu, akapona na maisha yakaendelea kama kawaida. Hakukuwa na dhambi yoyote kwa wananchi kujulishwa kwamba Mheshimiwa Rais 'hajisikii vizuri' hivyo leo au siku mbili hizi ameshauriwa kupata mapumziko ya kutosha, ni jambo la kawaida kabisa.
 
" Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika."

[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kiukweli tuache utani rais bdo hajawa katika hali yake ya kawaida.tumuombee watanzania...
Usitupe kazi bwana, muombee wewe pekee yako, sisi tuna watu wengi sana wenye mahitaji kama watoto yatima, wajane, waliodhuliwa na uongozi huu wa awamu ya tano, waliodhulumiwa, waliohukumiwa bila makosa, wagonjwa wa kweli, walionyang'anywa haki zao, waliobambikwa makesi.
 
Tusijisahau kwamba sisi ni wanadamu akiwamo Mheshimiwa Rais, kwamba kama walivyo wanadamu wote huamka hufanya shughuli zote za kila siku, na mwisho wa siku huhitaji kupumzika na kulala. Na huenda ikatokea simu moja au siku kadhaa mtu (Akiwemo Rais) akaumwa, akapata matibabu, akapona na maisha yakaendelea kama kawaida. Hakukuwa na dhambi yoyote kwa wananchi kujulishwa kwamba Mheshimiwa Rais 'hajisikii vizuri' hivyo leo au siku mbili hizi ameshauriwa kupata mapumziko ya kutosha, ni jambo la kawaida kabisa.


NDIYO NINI HIYO?
 
Back
Top Bottom