Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Kwanza nimejifunza sasa tumepata Mkurugenzi makini ndani ya TISS,

Alijaribu kuwapa taarifa tofauti tofauti maafisa ndani ya idara ili aweze kugundua ni wapi wanavujisha siri za serikali kwa wakina Kigogo.

Kuna watu wanaenda kupata adhabu kali ndani ya idara.
Kaua tembo kwa ubua, wapo watu wameshikwa pabaya.Na kadiri habari ilivyoenea ikawa rahisi kuwabaini key players,na wengine kwa ujinga wakajiongeza ili wasikoze kuteuliwa kwenye serikali hewa waliobuni au kutafuta misifa.
Bora wangechunguza kwanza habari hizo,na wakajiridhisha ndio watoe unoko wao.
Lakini kiherehere cha kuwa wa kwanza kutoa breaking news wamejichimbia kaburi.
Ghafla wamekuwa wadogo kama pilitoni.
 
Wale wazee walitoka Gamboshi na akina cyprian Musiba adui mkubwa wa membe wakaona njia bora ya kumchonganisha membe na magufuli ni kupiga uchawi kwenye anga za Ruangwa ili magufuli akasirike amkomoe membe na cyprian Musiba apate kuikwepa kesi yake iliyomlemea ingawa Bashite kajitoa mhanga kuigharamia mpaka mwisho kwa siri kubwa
Wale 900 wa gamboshi kama walishindwa zuia upepo wa kisurisuri nini faida yao si bure kabisa
 
Wale mabalozi walioteuliwa na Kapilimba wao wameshaapa?
Wale wanatafutiwa nchi, huyu aliyeapishwa haendi nje ya nchi bali amepewa cheo cha ubalozi ili aweze kuongea na mabalozi akiwa balozi katika kumsaidia Mh Rais. Nilimsikia Mh akidokeza hivyo
 
Natamani baba atoke akamalizie ziara yake mikoani Lindi na Mtwara, kinyume na Hapo uvumi na maneno vitaibuka upya, please!

Binafsi namwombea afya njema, aishi aone maoni ya Watu Juu yake Kama Mtu Binafsi lakini zaidi sana Kama Kiongozi wa Taifa, Amen!

View attachment 1240625
Ah ah mlitarajia haseme nini?? Hamjui kuwa apo ndo kwenye shithole aka bomba aka mrija unaompa salali???
 
Ameolewa huyu Ummy?. Please pleasr ndg zangu mnipe info nataka kufunga safari kuja Dar mapema wiki ijayo.
 
Bado watu mnaendelea na ramli!!? Kama ambavyo watu walipiga ramli kuwa Mh. Rais kalazwa German/kafa,ndivyo wengine wanavyopiga ramli kuwa kuna watu watakiona cha moto!. Kwa nini watanzania mnakuwa na mawazo hasi hasi tu!?
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Yupo Kazini Saa Zote Waliomuombea Mabaya Wanatoka Jasho Mpaka Sasa Hivi Miili Umelowa
 
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa viongozi wetu wa vyama vikuu vya upinzani nchini hawajui kinachoendelea Ikulu. Hii imekuja baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini na kuushadadia uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu na Dkt Mashinji wanatoa mpaka ujumbe wa kuliombea Taifa huku wakiambatanisha mishumaa!

Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Uko vizuri
 
chuma ndio nani?? kwanini wanajipa majina ya kipuuzi?
 
Chuma ni mgonjwa

Aliongea kigonjwa sana ile siku anaapisha kitu ambacho si kawaida yake

Kwanza angekua mzima angejibu mapigo mpenda sifa yule


Kwa hiyo hoja ya kuwa yupo Ujerumani kwa matibabu bado ipo?
 
Back
Top Bottom