Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Tumejifunza nini kama Taifa kuhusiana na uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli?

Nimejifunza kwamba utamaduni wa Watanzania kumstahi rais na kumuheshimu sana, siyo tu unaisha, bali unaelekea kwenye utamaduni wa ajabu wa kumtakia mtu, tena rais, kifo.

Hii ni tabia mbaya kwa upande wa wananchi wenye mawazo hayo.

Lakini tabia mbaya hii imepaliliwa na kutiliwa mbolea na ubabe wa rais Magufuli.

Watu waliwakejeli Kikwete na Mwinyi kwa udhaifu wao, lakini haikufikia watu wengi hivi kusheherekea uvumi wa kifo cha rais.
Mwambie ajirekebishe vitendo vyake anajibiwa kama vitendo vyake vilivyo.
 
I thought it that way. Unapokuwa mpinzani na agenda ikawa kufa kwa Rais, wewe ndio umekula? Au chama chenu kinawakilisha Gamboshi?
Sisi sote kama binadamu yanayotuzunguka yanafanana. Sijapenda kabisa baadhi ya wana siasa na walivyochukulia haya mambo.
Sisi waumini, Rais ametupa Mwenyezi Mungu. Inakera sana mambo aliyozushiwa

Mtajifunza jambo. Hapendwi wala hawamtaki.
Huo ndio ujumbe, mengine ni mambo ya kibinadamu tu.
 
hata adui yake angeelezwa hayo angesympathize. very tedious. ana washauri na daktari wake. wote wanalipwa kwa kazi hiyo. nilishangaa sana niliposikia daktari wake ni daktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya akina mama!yaleyale ya mahiga sheria na kabudi diplomasiauzushi a sio kukosa ushauri. uenda ikawa sishauriki itokanayo na sipangiwi. anayaweza - much know!
all in all ingesemwa. rumourmongers wasingechipuka. walipewa uwanja wa kutosha. that's in case I buy your reason of nonappearance ya rais. membe confirms the devastating effects occasioned by the rumours! nani alaumiwe? victorie, nyani, etal kwao ni sahihi kutokujibu uzushi. logically hii inaruhusu uzushi kutamalaki. which is too bad!
Tabia ya kupenda "Yakusikia" ni tabia ya mtu mvivu kutafakari. Upepo wa Rumour mongers utakuteka tu. Ati daktari wa Rais ni bingwa wa wamama ni kutania Taasisi ya Urais na sina uhakika kama unajua taaluma ya Mahiga, usiwe mvivu tafuta. Rais hakuwa peke yake ziarani, Waandishi kibao hakuna aliyeandika wala kuripoti madhira ya Rais, achia mawaziri, wabunge hadi wa upinzani, achia mbali madereva, walinzi na wananchi. Leo uamini ya Kisiki ati moshi umemuua Rais.
 
Toka Jumapili jioni leo ni jumatano siku ya Tatu hajainekana tena hadharani alafu kuna watu hapa hawataki watu wawe na mashaka ; mashaka ni hisia hazizuiliki!!
Kwani tabu iko wapi kusema yuko mapumzikoni au mgonjwa au ana uchovu ???

Wote waliopita haikuawahi kuwa ajabu
Nyerere alikua anachukua off hadi mwezi Mzima anakaaa Butiama ; au ikulu za Lushoto ; Arusha ;Kituli ; Mwanza au chamwino
The same Mwinyi ;Mkapa na Kikwete ambaye kabisa mnaambiwa yuko Serengeti anakula “bata” kupumzika

Let’s kill romours
 
Mtajifunza jambo. Hapendwi wala hawamtaki.
Huo ndio ujumbe, mengine ni mambo ya kibinadamu tu.
Ukiona kila mtu anakupenda ujue una kasoro. Na ntashangaa kama mtu amepewa uongozi ili kutafuta kupendwa
 
Tabia ya kupenda "Yakusikia" ni tabia ya mtu mvivu kutafakari. Upepo wa Rumour mongers utakuteka tu. Ati daktari wa Rais ni bingwa wa wamama ni kutania Taasisi ya Urais na sina uhakika kama unajua taaluma ya Mahiga, usiwe mvivu tafuta. Rais hakuwa peke yake ziarani, Waandishi kibao hakuna aliyeandika wala kuripoti madhira ya Rais, achia mawaziri, wabunge hadi wa upinzani, achia mbali madereva, walinzi na wananchi. Leo uamini ya Kisiki ati moshi umemuua Rais.
nimecheka sana. yakusikia kwako ni yapi? imani huja kwa kusikia na kusoma. nilipokuwa shule nilikuwa nasubiri ya mwalimu na kidogo naangalia kwenye ziada. sasa hivi nakuwa bombarded by news of all sorts. nina system of sorting the news - fake inclusive. hunitendei haki kuniweka kundi la mvivu. kama vile umeambukizwa na unayemtetea arrogance na much know. very sad. i don't claim to be omniscient, God forbid. kuna ninalojua. nikisema najua hakika najua!
kutania taasisi ya urais siwanii. nijuze kuhusu ngwale. kuhusu mahiga hata akiwa injinia, kwa uhakika ni seasoned diplomat. huthubutu kusema in the address of kabudi. na kuna mambo yameishaanza kuonekana siyo. even by nature he's not diplomatic. diplomats evade evasiveness. there lies his failure!
hakuna aliyeandika wala kuripoti. that's the irony of the whole saga! hata wewe ulikuwa wapi kutujuza haya kwa wakati. kama mchezo wa kupokezana kijiti wa aina ya ajabu sana. mliacha wakimbie siku tatu. mlipopokea kijiti mnakimbia kwenda walikotokea- opposite direction. damage done. walisema kuipiga iraq na kuijenga. what rationale? wameshindwa miserably! the same fate awaits you. naona kwa siku tatu haikuwa sensorship but restriction of news from your side. kukumbuka shuka kumekucha!
r
 
Mimi nilichojifunza ni kuwa serikali ya sasa imeanza kubadilika kwenye nyanja ya mawasiliano kwa umma hasa namna ya kukabiliana na tuhuma na uzushi wa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia kwenye kuvuja kwa siri za Ikulu.

Kwa jinsi ambavyo serikali/Ikulu imekabiliana na uzushi uliofanyika kwa muda wa siku tatu kuhusu afya ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa sana!

Nakumbuka wakati Rais Magufuli anaingia madarakani alikuwa anapenda kujibu kwa maneno kila tuhuma na uzushi uliohusu yeye au serikali yake bila kujua kwa kufanya hivyo alikuwa anawapa umaarufu wale ambao walikuwa wanatoa uzushi au tuhuma.

Kujibu kila uzushi na tuhuma kwa maneno ndio kulimpa umaarufu Mwana Mama aitwaye Mange Kimambi ambaye alijikuta akipata wafuasi zaidi ya milioni 2.4 kutoka laki 300000.

Kanuni moja ya kukabiliana na uzushi ni kuupuuza na kama ukiona bado unaendelea basi unachofanya ni kuonyesha ukweli kwa vitendo katika muda mwafaka kwa sababu uzushi ukiachwa kwa muda mrefu uendelee kuwepo huanza kuaminisha jamii hata isiyoamini kwa haraka (skeptical).

Uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli imejibiwa kwa muda mwafaka lakini kikubwa zaidi njia ya kitendo iliyotumika katika kujibu imeondoa imani (credibility) yote ya yule aliyeuanzisha na kuushupalia lakini vile vile waliouamini na kuushadadia wameonekana ni wajinga au wapumbavu.

Kitu kingine nilichojifunza ni kuwa viongozi wetu wa vyama vikuu vya upinzani nchini hawajui kinachoendelea Ikulu. Hii imekuja baada ya kuona baadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya upinzani kama Zitto Kabwe, Dkt Vicent Mashinji, Godbless Lema na Lazaro Nyalandu wakiamini na kuushadadia uzushi kuhusu afya ya Rais Magufuli. Kwa maana nyingine, siri za Ikulu kwa sasa hazitoki kwa urahisi. Fikiria viongozi wa vyama vikuu vya upinzani hawajui hata alipo Rais wa nchi achilia mbali afya yake! Yaani Zitto Kabwe wa leo hajui kinachoendelea Ikulu! Lazaro Nyalandu na Dkt Mashinji wanatoa mpaka ujumbe wa kuliombea Taifa huku wakiambatanisha mishumaa!

Haya ni maendeleo makubwa kwa taasisi/watu waliopewa dhamana ya kumlinda Rais na siri za Ikulu.

Nimejifunza pia kama wananchi wengi hawataelimishwa kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kuna uwezekano ''mpumbavu'' fulani kutunga uzushi wa suala fulani linalogusa hisia za wengi na wengi wakaamini na kufanya jambo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.

Mwisho kabisa nimejifunza kuwa inatakiwa kwanza kuchukua muda kabla ya kuamini kile ambacho kimeandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ukweli hukawia kufika.

Nimalizie kwa kuandika, Nimeamini Uongo hupanda kwa lifti. Ukweli hupanda kwa ngazi ili kumfikia mlengwa!
Funzo kubwa ni kwamba taifa limegawanyika. Watu waliopaswa kutuunganisha wanatugawa zaidi.
 
Tatizo ubongo wako haujai kisoda. Hapa siyo mahali pako, nenda kwenye magazeti ya Tanzanite. Hapa panahitajj Great thinkers tu siyo Buk 7 kama wewe. Get out of here asap
Kwahiyo mkuu great thinker ni wale wakazi wa ufipa?
 
Makundi ya kumzushia magufuli kifo ni mengi msiwasingizie chadema tu,watumishi wanaweza Fanya hivyo,wafanya biashara na hata maskini wa kawaida tu.Rais kuna maeneo anapatia ila kuna eneo anaharibu kama rais " kujenga umoja hawezi kabisaaaaa" anaamini mabavu sana
Mkuu;
Ninakubaliana kwa kiwango kikubwa na angalizo lako lakini kwenye suala la kujenga umoja katika nchi za Afrika zenye vyama vingi haiwezekani hasa kama nchi ilikuwa katika utawala wa siasa za kijamaa kabla ya mageuzi ya vyama vingi.
 
Back
Top Bottom