njasulu
New Member
- Jul 18, 2022
- 4
- 8
Kwa wafatiliaji wengi wa Habari za ulimwenguni swala la mporomoko wa kiuchumi wa dunia utakua haujakupita. Unaweza usiwe mfatiliaji wa Habari hizo lakini mathwahibu yake ukayasikia hata unapokunywa kikombe cha chai asubuhi.
Chanzo chake
Kwa kawaida uchumi unakua na mzunguko, ambao tunasema unaanza na hali nzuri ambapo watu huwa na amani, ajira zikiwepo za kutosha, mishahara mizuri, sekta binafsi ikifanya vizuri na ikiwa inakopesheka kwa urahisi. Baada ya miaka kadhaa mzunguko wa fedha ukizidi kwenye uchumi ambapo kwa mtazamo wangu ndio kisabibisha maarufu wa kudorora kwa uchumi husababisha ongezeka la bei katika masoko mbali mbali, aidha iwe ya chakula, au masoko ya malighafi za uzalishaji, sasa hapo ndipo inaingia kipindi cha mporomoko wa uchumi.
Serikali inaamua kupunguza mzunguko huu wa fedha na mara nyingi kwa kupitia benki kuu inaanza kupandisha riba, ili kudhoofisha ukopaji. Ni ngumu kwa watu binafsi kuliona hili, lakini kwa biashara kubwa ambazo zinategemea kwenye kukopa ili kusababisha upanuzi ikiwemo uwezo wa kuajiri unaathiriwa. Sasa hapo umeshafikiwa, maana mwaka unaofuata hakutakua na ajira kama ilivyo kawaida, gharama za kukopa ziko juu kupita kiasi na wakati mwingine biashara inabidi ipunguze watu waliopo kwenye ajira, au kusitisha baadhi ya marupurupu ili kuhimili upungufu wa fedha kwenye biashara. Baada ya miaka kadhaa sasa tunaweza tukawa tayari tumefikia kwenye unyogovu wa uchumi, hapa mara nyingi ajira hamna kwa Zaidi ya asili 70, bei ya kila kitu kinapanda kwa Zaidi ya asilimia 100 na serikali pia inaweza ikaingia kwenye shida ya kulipa madeni yake. Hili litakwenda hadi pale kutakapo tokea suluhisho la msaada wa kifedha kutoka mashirika yenye nguvu Zaidi ambayo yataingiza fedha kwenye mzunguko au serikali ibadilishe mienendo ya nchi ikiwemo kutotegemea bidhaa kutoka nje na kuhamasisha uzalishaji wa ndani hadi pale uchumi utakapo imarika tena na kurudi kwenye uchumi wa hali ya wastani.
Uviko 19
Mwaka 2019 janga la uviko lilipotokea hakuna aliekua tayari, lilitusomba wote masikini kwa matajiri. Nchi zote duniani ziliinga kwenye hatua ya kujihami na zikasitisha shughuli zote za kiuchumi ili kukabiliana na janga hili. Hadi hapa tayari unaona shida inaanza, maana kama hamna uzalishaji kwenye nchi ni swala la muda tu hadi kibao kikageuka.
Baada ya miezi kadhaa kwa nchi zenye uwezo zilionia ni busara kutoa msaada kwa biashara zake kubwa ili zisife kutokana na kusimama kwa shughuli za kibinadamu. Nchi kama Marekani na Uingereza zilikiua za kwanza kutoa misaada ya kifedha za moja kwa moja kwenye makampuni ambayo kwao waliona yanauhitaji wa kunusuriwa. Ila pesa zote hizi zilikua zinatoka wapi? Utaseam nchi hizi ni Tajiri sana kwaio zitakua na fedha zimekaa zikisubiria kutolewa, hapana.
Zilikopwa kwenye mashiriki ya benki ya dunia na IMF. Unaambiwa asilimia Zaidi ya 70 ya fedha za makaratasi zilipo kwenye mzunguko hivi leo zilichapishwa kipindi cha uviko 19, na hili si jambo jema kwa uchumi wa dunia. Hawakuishia hapo, wakaenda na kugawa fedha kwa wanachi wao, mtu mmoja mmoja alipokea fedha kutoka serikalini cha wastani wa shilingi milioni 2 kwa awamu 2 au 3.
Utakumbuka tulisema kukiwa na fedha nyingi kwenye mikono ya watu maana yake mfumuko wa bei upo karibu. Sasa utauliza mfumuko wa bei ulitokea wapi kama hakukua na bidhaa zinazozalishwa? Ukweli ni chochote kilichokua kinazalishwa wakati huu sasa kilikua kinagombaniwa na watu walikua na fedha ya kununua kwa gharama yoyote ili wakipate, lakini pia kwenye uchumi zilizoendelea watu walianza kuwekeza kwenye masoko ya mitaji na hatimaye ikazalisha matajiri wakubwa kwa haraka ndani ya muda mfupi, moja ya vipindi ambavyo kiliona matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanakufa kwa njaa ni wakati wa uviko.
Hapa nyumbani
Kutokana na utawala uliokuwepo, ambao ulifanya maamuzi ya kubatilisha uwepo wa uviko na Maisha yakaendelea kama kawaida inaweza ikaonekana kama tulitakiwa kupona na hali hii. Ila sasa utaelewa kwanini wanasema duniani sasa kama Kijiji, kwa wafatiliaji wa mambo watajua kwamba tunaagiza asimilia kubwa sana ya vyakula vyetu kutoka nchi za nje, ikiwemo sukari, mafuta ya kula Pamoja na ngano.
Lakini si hivyo tu, kuna mafuta na malighafi zingine ambazo tunategemea kutoka nchi za nje hususani vitu vya teknolojia. Kwetu sisi kusimama kwa uzalishaji wa china kulitugusa moja moja, maana kama tunavyojua kwa sasa wafanyabiashara wengi nchini wanategemea viwanda vya nchi.
Kwa wakati huo serikali yetu ilikua ikijikita katika ujenzi wa miradi na miundombuni mbali mbali, na kuna mkopo ulitoka kwa ajili ya kupunguza makali ya athari za uviko ila zilielekezwa kwenye miradi hiyo. Ikaja serikali nyingine ambayo ikadhamiria kufungua uchumi wetu ikiwemo kuongeza mikopo kwa ajili ya kufufua uchumi ambao ulififia kutokana na kupungua kwa uzalishaji Pamoja na mzunguko wa fedha kwenye biashara
Shida inakuja pale ambapo soko la dunia sasa likafunguka na uhitaji ukawa ghafla, watu walikua na hela kwenye mikono yao ambazo wakiwa na mahitaji yao ya miaka miwili wakiwa wamefungiwa hawakuyaopata. Hii ikapelekea ushalishaji na usambazaji kuonekana dhaifu lakini bado uhitaji ukiwa juu maradufu.
Sasa ndio wakati ambao bei zinaanza kupanda kwa kasi ya ajabu, dunia nzima inawaka moto kwa mfumuko wa bei marekani ikiripoti bei kufikia hatua za juu Zaidi kwa Zaidi ya miaka 40, hivyo hivyo kwa nchi zote za ulaya. Kwa kulinganisha tu, kwa sasa mfumuko wa bei Marekani ni asilimia 8 huku Tanzania ukiwa 4. Natolea mfano Marekani kwasababu ili tufanye manunuzi yoyote yale kwenye soko la dunia tunahitaji tutumie dollar, ambayo kwa sasa imeimarika kutokana na uhaba wake wa ghafla.
Mbaya Zaidi ujio wa vita vya Ukraine na Urusi ikaongezea chumvi kwenye kidonda ambacho bado kibichi. Kwa sasa Ukraine ni mzalishaji namba moja wa ngano duniani huku akifuatiwa na Urusi, pia Urusi ni mzalishaji namba moja wa mbolea duniani pia akiwa kati ya wazalishaji wakubwa Zaidi duniani wa gesi asilia na mafuta ghafi. Ikumbukwe kwa sasa pia Urusi ni nchi iliyowekewa vikwazo vingi Zaidi duniani, maana yake hakuna namna nchi zingine zitaweza kufanya nao biashara kiurahisi.
Kwa nchi kwa yetu ambayo inasema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, tayari inaashiria kizungu mkuti maana tunahitaji mbolea inayotoka urusi na sehemu ya mafuta kutoka kwenye umoja wa OPEC+. Ni gumzo kwetu kama taifa na kati ya yote inabidi tuchukue somo katika yote yanayoendelea ulimwenguni sasa.

Upvote
2