Tuseme ukweli, Watanzania wengi tuna Asili ya Wizi/Upigaji. Kuanzia House Girl mpaka Cheo cha juu cha Nchi. Kwa mantiki hiyo bila kuwa na Rais MKALI/ASIYEFUMBIA MACHO.Matokeo yake ndiyo haya Maji hakuna, Bidhaa zinapanda bei Ovyo, Ajira kwa Kujuana, Madini yanatoroshwa, Uharamia Umerudi, Umeme wa Mgao, Bandarini kutoa mzigo ni mbinde mpaka utoe kitu, TBS Kukagua gari ili lipate stika ya ubora ni mpaka kitu, Mafuta bei imepanda pamoja na tozo baadhi kuondolewa, Michango mashuleni iko full Swing, NGOs za Ushoga zimerejea, Wahujumu Uchumi woote wakubwa akina Ruge wameachiwa ili waendelee kusababisha mgao mitambo yao ifanyekazi, Viongozi Wazuri wasiopenda janjajanja wapigwa chini kuweka magarasa akina Jmakamba, Huko kwenye Mizani Malori yaliyozidi Uzito yanapeta, Bodi ya Mikopo HESLB Wanafunzi hewa Kibao, Wawekezaji wameanza kusainishwa Mikataba Marekani nk, Ukiuza toa Risiti ukinunua Dai Risiti TRA chali, Halmashauri ukusanyaji mapato hoooi, mashirika ya Umma kushindana ubunifu wa kujiiingizia kipato ili wapate gawio ziiiiiiiii!
Yupo Rais anakuja kuokoa Nchi hii tuendelee kumuomba Mungu.