Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Nimeshangaa sana hoja zinazoendelea, mara Zito mara Kangi. Kangi alichofanya ni kukengeuka kwake tu. Alifikiri kukata mauno kuliko Mond basi Mkulu atamlegezea tu na kupiga dili la kisawasawa. Ona Zitto naye - barua yake dhahabu lkn wanataka kumchonganisha na wana wa nchi. Serikali inambwelambwela kwa wenye mahela.
Yaani huku idukilo kwa kweli wanachi hawana hata habari ya mambo ya Kikangikangi na Kizitozito. Tunagugumia na njaa. Nilipoacha kazi na kuja kufanya ujasiriamali huku basi nikafikiri zitakuwa zinanipitia. Wapi bhana! Watendaji wa Sirikali na hata sisi wafanyabiashara tunakiona cha moto. Juzi juzi mwenzangu mfanyabiashara ya kukopesha ameanza kupeleka walimu polisi sababu wameshindwa kumlipa marejesho. Dogo mmoja alipewa baiskeli kwa mkopo hajaweza maliza mkopo kawekwa ndani polisi na baiskeli haijulikani ilipo. Kuna familia hapo Mwigumbi na Buchambi na Luhumbo wanakula mlo mmoja. Nasikia Maganzo familia moja imechukua familia zingine mbili wawafanyie kazi za mashamba kwa ujira wa chakula. Maganzo wachimbaji almasi wanang'ang'ania kwa matajiri ili kujinusuru na njaa na huku almasi nazo zimegoma.
Mhhh, hali ni ngumu usawa huu kwa kweli. Nimechunguza Diwani wetu naye analialia njaa - yule wa Chadema kule jirani bwana Ngosha Kanogu ndiyo usiseme alivyomaliza mahela kwa wachimbaji. Kuna uwezekano akahamia CCM. Wanasiasa wanalia njaa haswa. Kabla hajaenda bungeni Mbungeni wangu alishauriwa na Msaidizi wake awape wale wanaCCM hata shilingi elfu 20 tu na wao wapo 150 pale ili atoe milioni 3 akataka kunitukana mimi wkt nilimwambia itampatia mailage kwenye uchaguzi. Amesema akiukosa mwaka huu basi tena. Mafuta ya kwendea Dodoma yenyewe akasema amekopa akifika huko atamrushia aliyemkopesha mahela. Najua Mbunge wangu ni mkweli, hanidanganyi, hali ngumu sana.
Jinsi mkazo ulivyo na awamu hii kuna uwezekano mkubwa sana wengi watamgeuka huyu Rais itapofika kuanzia Juni. Wengie wanamlaumu lkn wakiwa wamoja wanajifanya hamna tatizo. Siku zote waficha magonjwa misiba huwaumbua. Rais huyu anakosea, watu hawawezi kula miradi yake aliyoanzisha. Miradi haiwezi kumtibu bibi yangu ambaye alikuwa anategemea vibarua, miradi hiyo haiwezi kunieleta furaha - haiwezi na haitaweza kamwe kwa mimi ambaye nikitaka kwenda Darisalama nadunduliza nauli ya lori kwa miezi sita. Ooooohhh tunatetewa watu maskini, tunatetewa wapi sasa? Watumiaji wakuu wa bidhaa nchini ni tabaka ajiriwa. Hata bia na kujirusha wao hufanya zaidi hata kuliko wafanyabiashara kama mimi. Hadi kuacha kazi niliamua kwa shikizo la hali ngumu. Sasa hata ndugu zangu wanaofanya kazi siku zote imekuwa vilio hawana fedha Mifukoni.
Labda tu nimalizie hivi, Hivi Magu ni kweli kabisa umewasahua watumishi wa Umma amabao ndiyo tegemeo kubwa kwenye biashara zetu sisi tunaotuitwa wanyonge. Hivi kweli kabisa umeamua kufanya hivyo! Hakika kura zao na zetu tunaooona machungu wanayopitia, hutozipata. Uchaguzi ujao sio wa Serikali za Mitaa, huu hapa utatuona vizuri. Subiri tu! Mweeeeeeee!