Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Watu wa Soka,
Tunaendelea na taarifa kuhusu usajili tulioufanya na maboresho yanayoendelea kwenye benchi la ufundi na kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.
Baada ya mshambuliaji Habib Kyombo na kiungo Aziz Andabwile, sasa tumefanikiwa kuinasa saini ya beki wa klabu ya Yanga Paul Godfrey "Boxer" ambaye kuanzia sasa ataitumikia timu yetu kwa miaka miwili.
Tutaendelea na utambulisho wa vifaa vipya mpaka pale dirisha la usajili litakapofungwa.
#TukutaneLigiKuu
#TukutaneMsimuUjao